Sakata la Dr Ulimboka lisituondoe kwenye suala la vigogo wezi sita walioweka hela Uswisi

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Hofu yangu ni hiyo, pengine serikali ilituondoa kidogo kwenye kashfa yao kuu iliyoibuka siku wakati mgomo wa madokta unatokota.

Hawa mafisadi sita vigogo wa serikali tayari wameuza gesi yetu aliyetupa wenyezi katika pwani yetu ya Bahari ya Hindi. Wameuza kwa wageni na kuwekewa mabilioni huko Uswisi na kilichobaki ni kwa wageni hawa kuweka offshore rigs zao na kuchota gesi (na mafuta?) na kuingiza katika meli za tanker zitakazokuwa zinaegesha kule baharini bila ya sisi kujua.

Baadhi ya vigo hawa ni bado wako serikalini na majina yao yaweza kujulikana wakati wowote na bila shaka wanahaha.

Hakika serikali imebanwa mbavu hapa. Jee safari hii watamuuwa nani?
 
Umesema Kweli, unakumbuka la dowans lilivyohafifishwa na Babu wa Loliondo? Sirikali sirikali bwana!
 
Umesema Kweli, unakumbuka la dowans lilivyohafifishwa na Babu wa Loliondo? Sirikali sirikali bwana![/QUOT
Tutarudi baadae huko uswizi lakini marekani wapo watasaidia kuwabana, acha sis tushughulike na hawa manyang'au hadi kieleweke tunasubiri kimbunga cha waalimu na sisi wengine tutajiunga kuondoa serikali hii dharimu.hawafiki 2015
 
Hilo nalo neno!! Lakini watanzania hatudanganyiki tena tutadeal na wote wawili. Pinda atakoma mwaka huu ajiandae kutoa kauli na kuiondoa.
 
Kwa namna ya ufanisi wa kimafia nchi inavyoonekana kuendeshwa tumeshuhudia spin offs nyingi za namna hii. inawezekana kabisa kudirect attention za watu kutoka kwenye another equally burning issue hii ya mabiioni, tumeona kwenye matukio mengi tu...chezea nguvu ya pesa nyie??
 
Kwa kuwa wahusika ni vigogo wa kisiasa na serikali ya CCM suala hilo limekwishazimwa!
 
Back
Top Bottom