SAIKOLOJIA YA SOKA: Bingwa wa mapinduzi cup ajae ni MLANDEGE FC!?, tutegemee makosa ya kibinadamu mengi zaidi upande wa SIMBA SC!

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,652
9,243
Boss wako akikufokea, akikunyanyasa au kukutukana mbele ya wafanyakazi wenzio kwa makosa ambayo unaamini hujayafanya utakaa kimya na kumvumilia kwa vile ni boss wako na yeye ndiye anayekufanya upate riziki ili mkono uende kinywani, upate ada za watoto waende shule n.k, kimsingi hasira hubaki moyoni. Umefika nyumbani na hasira zako umemtuma mtoto maji kachelewa kidogo unajikuta unamshushia kipigo kizito, hasira zote unazimalizia kwa watoto na roho yako inasuuzika. Kitakachowakuta SIMBA SC ni hicho hicho hapo juu kwenye mfano, hawa ndugu zetu wa ZANZIBAR wamekuwa wakiulalamikia sana muungano kwa kuwa unawaumiza hawautaki na uwezo wa kuuvunja, waamuzi nao ni binadamu kama sisi, hukasirika pia hupata hasira kama sisi, waamuzi ni marefa wa ZFF, vipi kama wakiamua kushusha hasira zao kwa mtindo wa mfano tajwa hapo juu? kwa maoni yangu kinacho enda kutokea ni kama kwenye huo mfano hapo juu kwa hoja kuu mbili 1. wachezaji wa mlandege ni wazanzibar watacheza kwa kujituma zaidi kwa hasira zaidi 2.waamuzi watawabeba
 
-324959523.jpg
 
Back
Top Bottom