Saikolojia na maumivu ya mapenzi

proton pump

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
5,363
6,901
Katika hekaheka za mapenzi kuna utamu na uchungu wake. Wanaoteseka sio wanaume tu bali wanawake nao sio mchezo.

Licha ya nyuzi kama zile za kula tunda kimasihara. Kuna wakati unaweza kumwinda mtu umpendae kwa namna zote lakini humpati kabisa.

Wapi utamu wa mapenzi unaanzia? Ni pale ambapo umewekeza kwa mtu umpendaye na mkapendana pia kuonesha mapenzi halisia.

Sehemu ugumu unapoanzia ni pale ambapo unampenda mtu, wakati yeye hana muda na wewe, na unakuta unawekeza nguvu fulani hata kifedha anatumia lakini holaa. Vivyo hivyo sio kwa mwanaume tu hata kwa mwanamke. Omba yasikukute. Ukishaona dalili fulani we acha tu huyo sio chaguo lako.

Uhalisia wengi wamekutana na watu ambao sio chaguo lao ama mtu kapenda kitu fulani kwako tu na sio mapenzi halisi (fake love). Hapa ndipo watu wanakua watumwa kila siku uchungu na vilio visivyoisha.

Ni nin matokeo hasa baada kukutana mtu asiyekupenda kisawasawa? kutukanwa, kudhihakiwa, mahusiano kuvunjika (hapa uhuru binafsi).

Ufanye nin sasa? Hapa ndio mziki kidogo hasa mtu ameamua kuganda. Uzuri wa kitu upo macho mwa mtazamaji " the beaty is in the eyes of the beholder".

TUKIO LENYEWE SIO TATIZO BALI TATIZO NI NAMNA UNAVYOTAFSIRI AKILINI MWAKO " The event itself is not a problem, but the way you interprete the event in your mind is the problem." Hapa ndipo mtu anapata msongo.

kwa maelezo zaidi kwenye msongo wa mawazo, sonona, njoo PM.
 
Back
Top Bottom