Vancomycin
Senior Member
- Jan 7, 2011
- 171
- 111
CHADEMA nayo imeionya CCM kuacha kupandikiza mbegu za udini kwa kuwatumia waumini wa dini ya Kiislamu katika kampeni za jimbo la Igunga.
Onyo hilo lilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Zanzibar), Saidi Issa Mohamed, akisema CCM imeanza kuwatumia baadhi ya viongozi wa Kiislamu kueleza kuwa chama hicho kimemdhalilisha mkuu wa wialaya ya Igunga kwa kumvua Hijab, hivyo wananchi wakikatae.
Alisema viongozi wa dini, kwa bahati mbaya bila kutafakari, wamejikuta wakiwa sehemu ya timu ya kampeni za CCM ambacho hivi sasa kina hali mbaya katika kampeni hizo.
Naliomba Baraza la Maulamaa kuwa makini na wanasiasa, alisema na kuwaomba wavute subira juu ya jambo hilo kwa kuwa liko mahakamani.
Naye Mwenyekiti wa CHADEMA, Mkoa wa Tabora, Kansa Mohamed, alisema serikali ya CCM imekuwa ikizitumia taasisi za dini na viongozi wake kufanikisha ushindi wake kwenye chaguzi mbalimbali.
Alisema mwaka 2000, CCM ilieneza propaganda kuwa CUF ni chama cha kidini lakini hakuna hata kiongozi mmoja wa Kiislamu aliyesimama na kupinga kauli hiyo.
Alisema mwaka 2010 CCM ilikuja na propaganda kuwa CHADEMA ni chama cha kidini na Waislamu wakahimizwa kumchagua Kikwete ambaye leo hii amebainika kuwa aliwahadaa juu ya Mahakama ya Kadhi na shule zilizotaifishwa. CCM inataka kuwagawa Waislamu na Wakristo ili iendelee kutawala; Watanzania wawe makini na jambo hili, alisema.
Source : Tanzania Daima