Safari za mabasi za usiku zimepunguza rushwa na wala rushwa hawapendi hilo

Ustaadhi 22

JF-Expert Member
Sep 5, 2021
762
1,426
Safari za MABASI Kwa Usiku Ni Nzuri na salama Zaidi Kwa sababu madereva wa Magari Mengi Hasa malori na Gari ndogo zenye Malena Wengi wanakuwa hawapo barabarani.

Lakini kimekuwa kilio kwa wala Rushwa maana usiku polisi na tasisi zingine zinazopenda Hela wanakuwa wachache saana.

Hili limepinguza ajali sana, dereva anakuwa na amani ya moyo pia anakuwa na Uhuru Zaidi Kwa sababu hapishani na Gari Nyingi zenye Malena,, Usiku Malena hawapo wanaogopa kugonga Au kugongana.

Lakini Kuna Watu wanataka wahujumu Maana Kula kwao kumekata. Serikali kuweni NAO makini Hasa Hizi Tasisi za Serikali. Dili Nyingi zimekata.
 
Kuna ambayo unaweza kuwa sahihi na mengine siyo. Kwa mfano ajali. Uzoefu unaonyesha kuwa safari za mabasi za usiku ndiyo zenye ajali nyingi na mbaya. Kwa vile ndiyo safari zimeanza siku si nyingi, tusibiri kwanza kabla ya kufanya conclusion.

Jingine: haya yote uliyoelezea kuwa yamepungua, ni mambo yanayoweza kumalizwa bila kutegemea safari za usiku. Yanaweza kumalizwa kwa kuwa na serikali nzuri yenye mfumo mzuri wa uongozi.

Nasema hivyo kwa sababu tukitegemea safari za usiku kudhani tunayamaliza, basi tutakuwa tunajidanganya kwa sababu wahusika watatafuta njia nyingine ya kuyafanya wakati wa usiku. Motive yangu ni kuwa: tusilihamishe tatizo bali tuliondoe.
 
Tuendelee tu kusafiri muda wote. Maana basi zote zina taa kali tu.

Isiruhusiwe tu kusafiri usiku basi ambayo haina taa tu (kama ipo😆)
 
Shida zina tabia ya kukupeleka kwa maadaui zako

Shida inae tabia mbaya sana
 
Waliambiwa Na Rais Wataongezwa Kwenye Malindo Tu
Barabarani Waondoke
 
Kuna syndicate kubwa sana inapinga hili swala.
1. Askari wa usalama barabarani
2. Askari wa mali asili
3. Wamiliki wa nyumba za kulala wageni
4. Wamiliki wa hotel na migahawa
5. LATRA
6.
 
Back
Top Bottom