Safari za JK: Matunda yake sasa?

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
Wadau wa JF sasa tunaona matunda ya safari za JK huko majuu.

Bush aliingia bongo , Rais wa kwanza wa Marekani kufanya hivyo katika historia ya Tanzania, na kamwaga mabilioni($700milion).Tukapata free media exposure ikiwa ni pamoja na Bush kumbusu yule bibie mmasai mrefu sana.

Hapa karibuni ameingia mwanaume Hu Jintao wa China.

Mara ya mwisho kiongozi mkuu kabisa wa China kufika hapa Tanzania ni Chou En Lai, mwaka 1965, wengine tukiwa watoto bado tulishuhudia pale uwanja wa Taifa.

Hu akamwaga pochi la $20milioni.

Sasa anaingia worlds Diplomat no 1, Ban Ki Moon, exposure zaidi itaingia na wakuu wetu wa itifaki watapata kauzoefu wa ku rub shoulders na wakubwa ikiwa ni pamoja na pengine miradi kwa ajili ya nchi.

Mwaonaje wakuu, si poa?

Tembea na wewe utembelewe, imekaaje hii wadau?
 
Kwa hiyo hizo safari zilikuwa ni kwa ajili ya kuomba omba misaada tu? Kaswalio ka kizushi unafikiri gharama za safari zake hizo zinaweza kuwa how much in total so far?

Kumbukumbuj yangu inaniambia at one time just a prime minister (Sumaye) alitumia USD 500,000 kwa safari moja. What about a presidoo then?
 
Yaani Nchi inauzwa wengine wanashangiria. Hivi Bill Clinton alikuja wakati wa Nyerere ?
 
Sasa mkuu akitumia $500,000( kama data ni za kweli) na akaleta $500 milioni uwiano huo si safi kabisa.Barabara zajengwa ,zahanati nk.
 
Yaani Nchi inauzwa wengine wanashangiria. Hivi Bill Clinton alikuja wakati wa Nyerere ?

Mkuu Mwiba, wakati Nyerere akiwa madarakani, Bill Clinton hakuwa Rais wa Marekani. Nadhani ulitaka kuzungumzia Ronald Reagan (ambae ndie aliekuwa Rais wakati huo).

Anyway, mimi sioni kuja kwa MaRais au wakuu wa Dunia nchini kunaongeza tija/ufanisi/maendeleo kwa nchi yetu. Maana kama wanataka kutupa misaada, si lazima waje hapa. Maendeleo ya nchi hayategemei nani anakuja nchini. Yanategemea juhudi za kuyafikia maendeleo hayo. Kama hao wageni wetu wanatuunga mkono katika juhudi za maendeleo, ni jambo jema. Ila maendeleo yetu hayawezi kupatikana kwa misaada ya pesa kutoka nje peke yake. Yatatokana na uwezeshaji wa kupata masoko kwenye nchi (jamii) zao, kuweka usawa wa kibiashara pamoja na uwekezaji wa kudumu katika nchi yetu (viwanda, kilimo, elimu, afya n.k.).

Kitu tunachopata kutokana na ziara hizo ni heshima tu. Heshima hii ni muhimu sana katika duru za kimataifa. Ila heshima ukiwa na njaa inapungua maana yake.
 
sijui,,,,, lakini hii dhana ya kuomba omba mi siipendi hata kidogo, kama lengo ni kuzurura huku na huko kwa lengo la kuomba wakati nyumbani kwako hakuna hata mwelekeo wa kutaka kujitegemea,hao wanaokupa hizo pesa wanakudharau. Je ni kweli hii kitu ya huyu kuja kumwaga mabilioni ya pesa na yule kumwaga mamilioni ndio itakayotuinua kiuchumi??? je ni kweli hivi ndivyo watanzania tunataka???hivi wewe kama baba unajisikiaje kwenda majumbani mwa watu kuomba omba kila kukicha?? I just dont like my country playing the"matonya" role. Let matonya do his job and let Tz be independent. What ever happened to independence and self reliance?? can anybody point out anything that tz is independent, and is proud of?? tumesomesha wakandarasi wa kila aina,, tell me ni barabara zipi tunazojivunia bongo ambazo zimetengezwa na wakandarasi wazalendo?? what happened to us kwamba nchi inaanza kukodi marubani ufaransa tena marubani wanafunzi na kwa gharama kubwa??hivi tumeishiwa marubani wazalendo?? kama ni hivyo kuna "strategy" gani za kuhakikisha tunawapata marubani hao wa kizaleondo within a time frame?? tuna madaktari wazaleondo wenye ujuzi wa kila aina lkn angalia wht they did to dr. ferdinand massawe, je kweli tuna nia thabiti ya kutaka kuwa na madaktari wetu wa magonjwa ya moyo na kuepuka utegemezi wa huduma hiyo toka india ambapo serikali inatumia pesa nyingi kupita maelezo?? hebu gusa kila kona na jiulize kweli sisi tunataka kweli kwa dhati kabisa kujitegemea siku moja?? hebu fikiria tu hili la mwananchi gold,, kama nia na lengo lake ni vile tulivyoelezwa na jaji warioba, imekuaje tumeiua kwa mikono yetu wenyewe,na badala yake tumewaacha wageni hawa wafanye watakavyo na dhahabu zetu?? kweli tuna nia thabiti ya kutaka kujitegemea sisi?? hivyo ninapoangalia haya yote na kumsoma rais wangu na ziara zake na haya matokea yake bado nashawishika kusema ,hatupo kwenye mwelekeo sahihi. correct me if i'm wrong!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
sijui,,,,, lakini hii dhana ya kuomba omba mi siipendi hata kidogo, kama lengo ni kuzurura huku na huko kwa lengo la kuomba wakati nyumbani kwako hakuna hata mwelekeo wa kutaka kujitegemea,hao wanaokupa hizo pesa wanakudharau. /QUOTE]

Mkuu Princedy, unayosema ni kweli kabisa lakini lazima tuendane na mwelekeo wa kidunia hivi sasa.
Dhana kuwa unakopa ou kupewa grant basi hustahili kuwa katika dunia si sahihi.
Historia inatukumbusha kuwa baada ya vita kuu ya pili nchi zilizoongoza kwa kupewa misaada ni pamoja na Japan, na Ujerumani.Uingereza vilevile ilipewa mikopo/misaada mizito ya kuinua uchumi wake na wanalipa mikopo hii hadi leo.
Suala ni hiyo misaada inatumika vipi katika kuendeleza uchumi.
Dhana ya masikini jeuri ilipitwa na wakati!
Leo kopa na fedha ufanyie maendeleo ya kuchochea uchumi wetu.
Kwa sasa hivi inabidi tuamke, kuna wengi huko nje wanaotaka kuwekeza hapa kwetu ila hawapati local partners.
Wenye "akili" wote wako kwenye siasa-kigezo tosha cha kutowapenda kuwa local partners.
Pamoja na exposure hizi za safari za JK na wageni kuja ni kuitambulisha Tanzania duniani, na wengi wanashangaa kuwa kumbe sio Rwanda/Burundi!
Watanzania TUAMKE na huu usingizi mzito.
 
Wadau wa JF sasa tunaona matunda ya safari za JK huko majuu.

Bush aliingia bongo , Rais wa kwanza wa Marekani kufanya hivyo katika historia ya Tanzania, na kamwaga mabilioni($700milion).Tukapata free media exposure ikiwa ni pamoja na Bush kumbusu yule bibie mmasai mrefu sana.

Hapa karibuni ameingia mwanaume Hu Jintao wa China.

Mara ya mwisho kiongozi mkuu kabisa wa China kufika hapa Tanzania ni Chou En Lai, mwaka 1965, wengine tukiwa watoto bado tulishuhudia pale uwanja wa Taifa.

Hu akamwaga pochi la $20milioni.

Sasa anaingia worlds Diplomat no 1, Ban Ki Moon, exposure zaidi itaingia na wakuu wetu wa itifaki watapata kauzoefu wa ku rub shoulders na wakubwa ikiwa ni pamoja na pengine miradi kwa ajili ya nchi.

Mwaonaje wakuu, si poa?

Tembea na wewe utembelewe, imekaaje hii wadau?

In a competitive world like ours today with insatiable resources, qualitative analysis should not form argumentative basis unless weighed quantitatively. In other words one needs to come-up with cost-benefit analysis to support some argument. However, caveat to the same is, the whole decision making for justifying president trips shouldn't be based on gambling.
 
Na mkutano wa Sullivan, na Walid Bin Talal (mfadhili mkuu wa Chuo Kikuu kipya cha Dodoma), na, na, na,... Hongera Jakaya, kazi zako tunaziona, wenye usongo wacha walalame.
 
Nakusoma bwana Gwakisa, mimi ugomvi wangu sio kupewa misaada, sikatai kwamba granting aids and assistance to poor countries is absolutely necessary. Ugomvi wangu ni huu, wa sisi kuwa kwenye mwelekeo wa kuwa tegemezi mpaka ukamilifu wa dahari.Hakuna mkakati ninaouona kwamba ipo siku tutaacha kuwa tegemezi na ndio maana naichukia dhana nzima ya misaada. Laiti ingalikuwa tunaomba misaada au mikopo kisha tunawekeza kwa dhati, na walau tunaanza kujitegemea japo katika maeneo machache niliyoyataja kwenye post yangu iliyopita,nakuhakikishia ningekuwa mmoja wa advocates wa kuomba misaada. kwa sasa hakika hatuna tofauti na akina matonya.
 
In a competitive world like ours today with insatiable resources, qualitative analysis should not form argumentative basis unless weighed quantitatively. In other words one needs to come-up with cost-benefit analysis to support some argument. However, caveat to the same is, the whole decision making for justifying president trips shouldn't be based on gambling.

You see BM21, also the spirit of entrpreneurship is something the the best of consultants will never evaluate.When to make a kill, how to make a kill is someting that can only be attained by intuition.
After all the evaluation and analysis , gamble ,yes gamble is the nature of the game.
The best education in the world will not sharpen your mind on seeing the silver lining on any business andertaking , it is experiencing it.
Thats why we have proffesors in the govt who make some of most obvious economic mistakes.
But in these trips by JK, funds have started flowing and beleive you me those sharp and hard nosed business men are already here!!
 
Back
Top Bottom