Safari ya Spika Sitta Urambo baada ya NEC August 2009

Kwa mtazamo wangu....Sitta ni shujaa na anastahili kuungwa mkono na wana Urambo pamoja na wachukia ufisadi wote.
 
karibuni wabaya wa Sitta, hapa linapendwa Taifa siyo chama na kuchukiwa mafisadi. wote.

Kweli ndugu.

Jamaa yangu mmoja ananikumbusha kuwa aliyekubali kufa kwa ajili ya watu alikuwa yesu peke sijui kama sita ataweza kuvaa viatu vya yesu, any way lets wait and see!

Kama nimekuelewa unataka kusema ufisadi ni sawa na kwamba dhana ya mtu kupigania haki za watu anaowawakilisha haifai. Inaelekea hayo ya Yesu pia hukuyasoma sawa sawa kwani alise ukitaka kuiokoa nafsi yako shart ujikane mwenyewe, ujitwike msalaba wako na kisha umfuate. Kumbe tunatakiwa kujaribu ya yesu. Vinginevyo hakuna haja ya kuwa waamini.

"Lets wait and see" gani umekata tamaa wewe, unatakiwa sio ku-wait bali kushiriki. Mungu Ibariki Tanzania izae watoto wasio na mawazo kama yako.
 
Nazidi kushangaaa.......hapa cha kufurahia ni nini sasa? Huyo six, maandamano au ufujaji wa pesa kwa kukodi mapikipiki ambapo zingeweza kutumika kwa masuala mengine ya maendeleo ya wananchi? Embu tuamke wa TZ siyo kushabikia kila jambo.........

Ukitaka kujua kinachotokea, waulize wanasiasa. Ukitaka kuyajua haya yote wakati wewe siyo mwanasiasa, utaona kioja.

Jiulize kwa nini Mwenyekiti wa CCM hupigiwa makofi aingiapo ukumbini kabla hata hajasema lolote ktk kikao. Wanaoandamana na Rais pia hucheka au kushangilia kila wakiona bosi wao anafanya hivyo.

Binafsi naona hao wananchi wanaonyesha defiance. Kwamba NEC lolote ifanye wao wako upande wa pili wa maamuzi.
 
Wadanganyika mtaandamana kweli kweli mwaka huu.

Huyu mtu ambaye ameshindwa kutetea haki na ukweli, mnaandamana ili iweje?

Ningeelewa kama Sitta angewaambia CCM kwa hili chukueni kadi yenu lakini mimi nitaendelea kutenda haki na kutetea ukweli mpaka kieleweke.

Sasa huyu mtu ambaye kapiga magoti na kuomba asilubiwe, mnampongeza kwa lipi?

Spika mzima unaburuzwa na wenyeviti wa mikoa?

Nakubaliana na FMES, mwanaume alikuwa Mrema. Pamoja na mapungufu yake yote lakini yeye alikuwa tayari kusimamia mambo aliyokuwa anayaamini.

Hawa wengine waganga njaa tu; wanaogopa kuondoka CCM kwasababu wana madudu yao mengi, wakiondoka, CCM na serikali yake itawamaliza mara moja.
 
Wao mashabiki wa Mheshimiwa Sitta Urambo jamani wangetumia hizo pesa kuboresha vituo vya afya huko Urambo haya matumizi mabaya ya pesa kwa ajili tu yakuhakikisha kunakuwa na mbwembwe za kisiasa hayatatusaidia kwenye nchi hii ambayo ni maskini sana
 
Watanzania tulilaaniwa. Tunapoteza sana nguvu na raslimali zetuu kwa mambo ya kijinga tu.
 
  • Mafisadi papa wanadaiwa kuwa wana CCM na aliyewataja hadharani ni mwana CCM.
  • Mtu wa vijisenti ni mwana CCM na waliomwandalia mapokezi ya nguvu Bariadi ni wana CCM.
  • Waziri Mkuu wa zamani ni mwana CCM na waliompokea Monduli baada ya kujiuzulu ni wana CCM.
  • Spika Sita ni mwana CCM na wanaopanga kumpokea huko Urambo ni wana CCM.
  • Wanaodai wanapiga vita ufisadi ndani ya CCM na wanaotetea ufisadi wote ni wana CCM.
  • Kikao kilikuwa cha CCM na mijadala iliendeshwa kiCCM na maazimio yoyote yaliyotolewa ni ya CCM.
  • Hili zimwi CCM linawezaje kuwa safi na chafu kwa wakati moja ?
  • Sisi wananchi tunawezaje kupenda na kuchukia ufisadi kwa wakati moja ?
  • Watanzania tuna utajiri mkubwa lakini twaogelea kwenye umasikini.
  • Tuna utulivu na amani lakini twatumia FFU kuwazima tusiokubaliana nao.
  • Tuna demokrasia ya vyama vingi lakini tuna udikteta wa chama kimoja.
  • Tuna Bunge linalowakilisha wananchi milioni 40 lakini lalinda maslahi ya watu milioni 4.
Talk of a land paradoxes, Tanzania is in a league of its own !
 
Wadanganyika mtaandamana kweli kweli mwaka huu.

Huyu mtu ambaye ameshindwa kutetea haki na ukweli, mnaandamana ili iweje?

Ningeelewa kama Sitta angewaambia CCM kwa hili chukueni kadi yenu lakini mimi nitaendelea kutenda haki na kutetea ukweli mpaka kieleweke.

Sasa huyu mtu ambaye kapiga magoti na kuomba asilubiwe, mnampongeza kwa lipi?

Spika mzima unaburuzwa na wenyeviti wa mikoa?

Nakubaliana na FMES, mwanaume alikuwa Mrema. Pamoja na mapungufu yake yote lakini yeye alikuwa tayari kusimamia mambo aliyokuwa anayaamini.

Hawa wengine waganga njaa tu; wanaogopa kuondoka CCM kwasababu wana madudu yao mengi, wakiondoka, CCM na serikali yake itawamaliza mara moja.

Engineer,

Mhe. Sita kafanya mambo makubwa saba ndani ya Bunge haijawahi kutokea na hata akiondoka leo itabaki kuwa historia.

Kwenye mapambano ukiona unazidiwa lazima hurudi kwanza nyuma ukienda kichwa kichwa kama Lowasa unakwisha rafiki yangu, ameelezea MMJ

Naomba tumpe muda anapigana hii vita na watu wenye siraha kali tena kubwa yeye akiwa na rungu peke yake. Huu ufisadi uliojijenga tokea Nyerere amekufa hadi leo hii hauwezi ukauondoa haraka haraka kama unavyofikiri mwishowe utaishia kuwa Sokoine. (Lejea walaka ule wafanyakazi wa Bunge) hii yote ni vita.

Tumpe Muda na Nguvu pia Tumuombee kwani na mimi ni maskini mmojawao.
 
Maane,

Hicho kitabu cha Mwalimu Nyerere, UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA, ambacho unasema unakitafuta kwa udi na uvumba, na ambacho Sitta amekemewa na Mwalimu Nyerere kwa unafiki wa kisiasa kuhusu suala la Tanganyika, hakipatikani kwenye maduka ya vitabu, labda maktaba za umma na za watu binafsi, kama ya kwangu! Ninacho cha Kiswahili na Kiingereza chake! Labda nenda "Mwalimu Nyerere Foundation", kwa Mzee Butiku, upatiwe nakala na ufanye "photocopy" kurasa unazozihitaji au chote. Mna mambo mengi sana muhimu humo na ukikisoma kwa makini utaona mijadala mingi ya humu JF ya watu wanaojifanya "Wanamgambo" wa ufisadi, ni POROJO na UNAFIKI mtupu!
Bwassa
Bwassa
 
Nji hii ipo kwenye hatari ya kuingia kwenye janga la njaa! tayari sehemu nyingine kumepatwa na janga hili...........hawa watu wa kutoa pesa za kukodi pikipiki za kichina na kulisha watu ubwabwa kwa siku moja, si wangesaidia kununua magunia kadhaa ya mahindi wawasaidie wakina mama, wakina babu na wadogo zetu walio katika njaa?

au basi hata wajenge nyumba nne za walimu kwenye shule mbili za kata huko jimboni kwao.
 
RA & EL ... might be in good position to explain this!!
 
Mafisadi na wanaounga mkono ufisadi wana nguvu ndani ya CCM, wanaopinga ufisadi wanungwa mkono na wananchi masikini. Labda CCM ife tena salama
 
Kwenye mapambano ukiona unazidiwa lazima hurudi kwanza nyuma ukienda kichwa kichwa kama Lowasa unakwisha rafiki yangu
Na hilo ndilo analolifanya Sitta. Maadui zake wameshaanza kuwa matumbo moto kwa sababu hawajui anapanga kufanya nini ifikapo Novemba
 
Naona hicho watakachofanya wana Tabora ni kizuri. Waionyeshe NEC kwamba maamuzi yake hayakubaliki kwa wanachama walio wengi ambao ni walala hoi. Maamuzi hayo yakubalika kwa mafisadi tu.
Keep it up Sitta; kuna umma mkubwa nyuma yako. Kaza buti nenda taratibu.
 
Pongezi sana wana tabora na wana urambo kwa jambo jema mnalopanga kufanya...endeleeni kumtia moyo baba yenu ili alete chachu ya mabadiliko katika nchi hii.

Ila huku kwenye jf kuna wati bongo lala au watoto wa rostam na lowassa ambao macho na fikra zao zimefungwa....wanaendeleza vita vyao dhidi ya mpigania nchi yetu. Hivi hakuna uwezekano wa kufuta maoni yao humu.....hebu wadau wenye akili tuwajadili hawa ili waache kutoa uchafu wao humu kwenye jf..........
 
ambaye haoni alichofanya Sitta kustahili kupokelewa kwa maandano awaulize CCM kwa nini wanataka kumzuia asifanye kazi yake ya uspika.
Jamani tukubali,kufanya aliyoyafanya katika mazingira ambayo bunge limetawaliwa na chama kimoja halafu chama chenyewe kikiwa kimedhibitiwa na mafisadi mafanikio sio haba. Anayebisha hajui kuwa CCM imedhibitwa ipasavyo na mafisadi au ni mawakala wa mafisadi
 
watu wa Urambo ndio wameamua sita hawezi kuwazuia wasiandamane, so tusubiri tuone labda nao wote wanaweza kuamriwa warudisha kadi zao za SISIEM
 
Wadanganyika mtaandamana kweli kweli mwaka huu.

Huyu mtu ambaye ameshindwa kutetea haki na ukweli, mnaandamana ili iweje?

Ningeelewa kama Sitta angewaambia CCM kwa hili chukueni kadi yenu lakini mimi nitaendelea kutenda haki na kutetea ukweli mpaka kieleweke.

Sasa huyu mtu ambaye kapiga magoti na kuomba asilubiwe, mnampongeza kwa lipi?

Spika mzima unaburuzwa na wenyeviti wa mikoa?

Nakubaliana na FMES, mwanaume alikuwa Mrema. Pamoja na mapungufu yake yote lakini yeye alikuwa tayari kusimamia mambo aliyokuwa anayaamini.

Hawa wengine waganga njaa tu; wanaogopa kuondoka CCM kwasababu wana madudu yao mengi, wakiondoka, CCM na serikali yake itawamaliza mara moja.
Mkuu wangu tujifunze kutokana na makosa.. Mimi nasema hivi toka Mrema aondoke CCM ndipo Maadili na miiko ya Uongozi ilipoanza kufa..
Leo tupo wapi, kurudisha kadi kwa Mrema na mashujaa wengine waliojaribu kutishia, kufa au kuondoka, hizo nafasi zao zikajazwa na kina Lowassa, Ra na wengineo, haya yote tusingekuwa tukiyazungumza..Kwa wapiganaji, akirudisha kadi mzee Sitta ndio tumefanikisha kitu gani? maanake hatujawashinda bado Mafisadi..
 
Habari zilizotapakaa kwa siku mbili tatu hapa Tabora ni juu ya mapokezi makubwa kwa mheshimiwa SS! lakini kwa kadri muda unavyozidi kwenda hali inaanza kubadilika sijui ni kwa SS kuwaambia wapambe wake wasimpokee au vinginevyo kwani maandalizi yote yaliyokuwa yamepangwa sasa yamebadilika na badala ya kupokelewa na baadhi ya viongozi CCM ambao ni maswaiba wake sasa atapokelewa na viongozi wa kanisa la Anglikana ambao kimsingi ndio waliomwalika rasmi kwenye tamasha la kidini.

Aidha baadhi ya wana CCM ambao ni wapenzi wakubwa wa SS sasa wanafanya maandalizi hayo kwa mgongo wa Kanisa na vikao vyote vinafanyika kanisani Anglikani Tabora, niandikapo hapa vikao vinaendelea Anglikani hasa baada ya ratiba ya ndege kubadilika ghafla ni kwamba ndege hiyo yatarajiwa kuland Tabora Air Port saa 6 dkk 20 mchana waleo badala ya muda wake wa kawaida saa tatu na nusu asbh.

Nipo nje ya jengo la kanisa nikisikilizia kinachoendelea, I ll keep you informed
 
M-bongo

Tunakusubiri kwa hamu na habari ya Mzee Sitta leo hapo Tabora,na tafadhali kama atalizungumzia suala la kubanwa na NEC-CCM uje utueleze kama ama amekiri kama alifanyiwa vimbwanga na akina Chilligati au na yeye anajiuma-uma kuelezea ukweli kwa watz!

Then,kama una kitu cha kurekodia itakuwa vyema kumnasa akieleza mwenyewe yaliyotokea NEC-Dodoma!
 
Back
Top Bottom