SABABU ZA USALITI KWENYE UHUSIANO

Emmanuel Zao

Member
Mar 8, 2015
6
16
USALITI ni kitu kibaya sana ambacho kimsingi hudhoofisha kama sio kuharibu kabisa uhusiano, vilevile hupoteza mali na muda wa mtu. Kibaya zaidi usaliti unaweza kusababisha ulemavu au Vifo.

Tafsiri hasa ya neno USALITI inaweza kutofautiana kutegemea na maada ya mazungumzo au mtazamo wa mtu. Lakini usaliti nitakaozungumzia ni ule wa kwenye uhusiano wa kimapenzi au ndoa.

USALITI huu kwa mtazamo wangu una maana ya “kutoa siri, kufuja mali na nguvu ya mwenza wako kwaajili ya mwingine, napia kushiriki tendo la ndoa na mtu tofauti na mwenza wako”.

Sitaki nizunguke sana, hizi ndio sababu za kwanini wapenzi/wana-ndoa wanasalitiana:

1. TAARIFA KABLA (KUJUANA)
Kabla ya kumpenda nakuanza kujihusisha kimapenzi na mtu, kunatakiwa kuwa na mazungumzo ili kuwa na uhakika na aina ya mpenzi unaemtaka. Mfano hutaki kuoa/kuolewa kwa wakati huo ila unataka mtu wakujiburudisha nae tu Kwasababu sote tunajua MUNGU kazuia tendo la ndoa kabla ya ndoa(Kwa mujibu wa dini) lakini alisahau kuondoa hamu ya tendo la ndoa kabla ya ndoa(mtazamo wangu). Hivyo basi kutokuwa na taarifa kabla kuhusu mwenza wako mtarajiwa kunaweza kuwa chanzo cha usaliti ambapo mwisho wa siku kutakuwa na maneno kama “Ooh! Sasa mbona hukuniambia mapema”

2. MTAZAMO SAWA
Hoja hii inaweza kuwa inafanana sana na ya kwanza ila kuna utofauti kidogo kama utazingatia. Unatakiwa kuwa muwazi kwakubainisha vema aina ya mahusiano unayotaka mfano:
•Unataka mahusiano ambayo yataelekea kwenye ndoa.
•Unataka au hutaki mtoto kwa wakati huu.

•Pengine unatarajia ngono zaidi, pesa sana nyingi, chakula kizuri, vitu au mavazi.
•Unataka kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja,
•Uhusiano ya siri N.k

•Unataka mtu wa kushiriki nae kinyume na maumbile(Mtanisamehe hapa ila hili tunalo kwenye jamii na watu wanatoka inje ya ndoa sababu hawezi kumwambia mwenzi wake amfanyie maana amemficha toka awali).

Wapenzi wanapokuwa na mtazamo/matarajio tofauti kwenye uhusiano wao, usaliti unaweza kutokea kirahisi, mfano mwanaume kamshawishi mwanamke kwa pesa, kwahiyo hapa pengine lengo la mume ni Ngono huku la mke ni pesa. Mwanamke akipunguza kutoa tendo(kwa wakati) jamaa hatosema badala yake atamsaliti, hivyo hivyo kwa Mwanaume akipunguza kutoa pesa. Kumbe basi angesema mapema angekatiwa kisha akaenda kutafuta atakaemkubalia.

3. MAISHA DUNI
Ugumu wa maisha pia huwa chanzo cha usaliti, kiasi kwamba hata yule mwenye msimamo na imani imara ya dini au miiko yake, kuna muda inabidi abadiri msimamo tu. Chukulia una kazi inayokupa kipato cha laki 150,000/kwa mwezi halafu mahitaji yako ni 250,000. Anatokea mtu wa nje anataka akupe milioni mbili kwaajili ya penzi. Uamuzi ni wako kupokea mshahara wako wa miaka miwili ndani ya nusu saa au usubiri mpaka hiyo miaka.

4. TAMAA YA PESA/MALI
Kuna watu wameumbwa na/au basi tu wanaendekeza tamaa ya maua ya Dunia, ukiwa na mtu kama huyu hata umpe nini hawezi kuridhika, kwahiyo ni kazi kwako kufanya maamuzi ya kuachana nae au kumbadiri tabia kama utaweza.

5. TAMAA ZA MWILI
Huyu yeye hana haja na chochote bali ngono tu, ukiwa karibu nae hatamani mtu mwingine lakini ukiondoka tu, kama ni mwanamke atatembea na majirani zako, ndugu, wafanyakazi na yeyote atakaye bahatika kuwa karibu nae, Hivyo hivyo kwa mwanaume yuko tayari kufanya hata na dada wakazi wengine hufanya mpaka na wanyama.
Wasaliti wa namna hii huwa hawaangalii uzuri au ubaya wa mtu wa kufanya nae kikubwa awe anaweza kufanya tu.

6. USHAMBA NA ULIMBUKENI WA VITU NA WATU
Hapa nimewenga wanaowasaliti watu wao kisa tu katongozwa na mtu maarufu, au pengine kaahidiwa kupandishwa ndege, kulala kwenye hotel nzuri.
Unakuta mwanamke analala na mwanaume kisa tu ana gari, yaani yeye wala hana haja na gari wala pesa au chochote, shida yake ni kulala na mwanaume mwenye gari.
Au Mwanaume kulala na mwanamke mwingine kisa ni Mzungu au mwarabu.

7. KUISHI KWA MAZOEA
Kama umewahi kuwa na wapenzi wengi kabla ya huyo mume/mke basi hoja hii inakuhusu.
Ndio maana kuna baadhi ya wanaume hutaka kuoa mwanamke bikra maana ex- wake pekee atakaemkumbuka ni huyohuyo mume wake.
Wapenzi wengi wa nyuma husababisha uone mapungufu kwenye uhusiano uliopo, kuhisi kuna kitu hakipati na hivyo analazimika kukitafuta nje.

Lakini pia wapo watu hasa wanaume, wanaishi kwa mazoea kwakuamini kuwa wanawake wanatofautiana, wanawachukulia kama ilivyo kwa chakula kwahiyo atataka kuonja kila chungu. Hata umpe nini au umpe mtindo gani wa mapenzi akipata nafasi atakusaliti kwakutaka kujua utofauti wa Mtanga na mzanzibari, Mnyiramba na Mnyaturu, Mzungu na mwafrica N.k

8. RUSHWA YA NGONO
Kuna wakati Usaliti unatokea kwaajili kujipatia ajira,haki au nafasi ambayo haustahiri kwakua huna sifa na vigezo vinavyohitajika, pesa, au tamaa ya uongozi.

9. MCHANGO WA SERIKALI KWENYE USALITI
Serikali kutoshughurikia ipasavyo kesi za udharirishaji na usiliti pindi zinapo-arifiwa kunafanya usaliti uonekani ni kitu cha kawaida tu na kwamba mtu hufanya akiamini linaweza kutatuliwa kiungwana endapo itagundulika.
Serikali yetu (JMT) inatambua hasahasa uhusiano wa ndoa rasmi, kuna haja yakutambua hata uchumba na mapenzi ya kawaida na pindi tu kesi ya usaliti inapojitokeza haki na adhabu kali zitolewe kwa wakosaji. Tofauti na ilivyo sasa kesi ya usali kwenye uchumba hushughulikiwa endapo tu kuna uhalifu au kosa la jinai limehusika.

HITIMISHO:
Usaliti ni kitu kizuri na kitamu sana ikiwa unakifanya wewe, ila kinyume chake ni uchungu na maumivu makali sana. Kwa aina yoyote ya uhusiano utakayopendelea LAZIMA huwa kuna watu pia wanafikra au mtazamo/Matarajio kama yako kwahiyo ni wewe sasa kumtafuta unaeendana nae.

Hata hivyo, ni vigumu kumpata mkamilifu, kubali mapungufu machache ya mwenzio na umfanye ajivunie kuwa na mtu kama wewe. Na Ikiwa uaminifu sio mambo yako, baki mseja, usipoteze muda, mali, bahati za wengine kwakuchezea hisia na kuvunja mioyo yao.

Ahsanteni!
 
GOOD ANALYSIS THOUGH
 
Ukiona unasalitiwa ujue kwa upande wako , mwenzi wako alishaumaliza mwendo.
 
Back
Top Bottom