Sababu za Kutoipigia Kura yangu CCM

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
Wana Jamii, nimefikiri nimeona hakuna haja ya kuipa kura yangu CCM, sababu zangu za msingi ni hizi

1. Chama kisichokuwa na lengo la kuwakomboa wananchi wake kutokana na
ujinga, maradhi.

2. Chama kinacholea mafisadi na wezi wa mali za umma

3. Chama kisicho na dira wala mwelekeo wa maendeleo ya taifa letu

4. Chama kinachosema uwongo juu ya utekekeleza ilani yake ya uchaguzi.

5. Chama kilichoshidwa kukemea Rushwa, Ufisadi na bado kinawalea mafisadi
ndani yake.

6. Chama cha Udikteta kisichokubali kukosolewa

7. Chama Kilichoshidwa kuleta maendeleo kwa wananchi wake - hali ya maisha
ya wananchi inazidi kuwa duni kila kukicha.

8 . Hakina mkakati wowote wa kukuza elimu tangu ile ya msingi hadi vyuo vikuu

9. kimeshindwa kuweka sera bora za uwekezaji nchini - kila kitu ni hovyo hovyo

10.Kimeshindwa kuwa na Sera nzuri za Kuendeleza Miji, Miundombinu mibovu

11. Kimeshindwa Kutoa dira kwa wananchi wake katika kujitafutia maendeleo

12. Kimeshindwa kuweka misingi ya Utawala bora -

13. Chama kilichoshindwa kukidhi matakwa na wananchi wake - kinaenda
kinyume kabisa na uongozi bora

14.Hakina utaratibu wa kuchukuliana hatua kwa watendaji na makada wake
wanapofanya makosa, badala yake ni kufichiana siri ili wananchi wasijue kipi
kinachoendelea ndani yake.

15. Kimefikia hatua ya kuingilia uhuru wa Bunge na Mahakama as if chenyewe ndiyo kimepewa ridhaa ya kusimamia mihimili hii muhimu ya taifa letu

16. Hakitaki kusikiliza ushauri toka kwa wasomi wa nchi hii kuhusu mambo ya
Kisiasa, Kiuchumi, Kijamii na kisayansi ya Technologia kwa ujumla ili kusaidia
maendeleo ya nchi yetu.

17. Chama kinachotoa sera za uwongo kwa wananchi wake kuzidi kuwadanganya
- mfano kilimo kwanza, elimu kwa wote etc..

18. Chama kisichowajali wasiojiweza na vilema kuweka mikakati ya kuwasaidia.

19. Kimewasahau Vijana, watoto na badala yake kinawalea wazee walikwisha
pitwa na wakati

20. Chama cha wanyanganyi kisicho na uchungu na mali asali za nchi yetu tulizorithi kutoka kwa mababu zetu
 
kwa ujumla sema CCM kimepoteza mwelekeo. Hatimaye akina Yahaya ndio wanaongoza serikali kwa mlango wa nyuma
 
kwa ujumla sema CCM kimepoteza mwelekeo. Hatimaye akina Yahaya ndio wanaongoza serikali kwa mlango wa nyuma
Thanks Kingi, ila ukisema " kimekosa dira na mwelekeo" its too general ni vigumu mtu mtu wa elimu ya kawaida kuelewa mwelekeo upi? kuelekea wapi? na ndiyo maana nimeweka kwenye very simple details ili wote tuwe tuongee kwa kutumia frequency moja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom