Jeshi linaongozwa na washikaji wa Kikwete ambaye amechagua wasani wenzake sasa ndio tunaonyeshwa usanii wa hali ya juu. Ntamani kulia nchi ilivyotekwa na Mafisadi
Mabomu hayakulipuka Kwa sababu za usanii wa mtu au ushikaji Kwa sababu zifuatazo
(1) mabomu huwa yana expiry date.inawezekana mengi yalikuwa yame expire
(2) Mabomu yaliyo expire Kama hayakupata usumbufu Wa aina yeyote nimedokezwa kuwa hayalipuki unless kutokee catalyst kama moto. Hivyo kuna uwezekano kuwa shoti ya umeme imetokea ikazua moto na ndipo chain reaction ikaendelea.
(3) jeshi Kama taasisi inayo take stock ya silaha zake inapashwa kuwa inajua mabomu na makombora ualiyo expire na kuyateketeza
(4) kuteketeza mabomu na makombora kuna gharama zake ambazo zinapashwa ziwe kwenye bajeti
(5) Kwa sababu ni tukio la pili katika kipindi cha chini ya miaka miwili na katika Jiji moja naelekea kuamini kuwa kulikuwa na uzembe wa hali ya juu katika ngazi za utekelezaji kwamba hiyo item aidha haikuwekewa bajeti au ilikuwa katika bajeti lakini vitu vingine vilaonekana kuwa muhimu zaidi Kwa anayeamua sasa pesa hii itumike hivi.hiyo tume itujuze.