SoC02 Sababu saba (07) za kwanini unapaswa kukabiliana na msongo wa mawazo kwenye maisha yako

Stories of Change - 2022 Competition
Jul 13, 2021
19
35
Msongo wa mawazo ni hali ya kuwa na mawazo mengi kichwani kwa lugha rahisi ni mawazo ambayo yamerudhikana kwenye akili na kufanya uone unashindwa kuamua au kufanya maamuzi nini ufanye kutokana na changamoto, vikwazo, magumu na matatizo ambayo unapitia kwenye maisha ya kila siku.

Inawezekana una msongo wa mawazo kwa kuwa mahusiano yako yapo kwenye danger zone, huna fedha, maisha ni magumu, biashara imefeli, masomo ni magumu, umekataliwa na mtu fulani, umepoteza mtu wa muhimu kwenye maisha yako n.k na msongo wa mawazo usipochukua hatua mapema kukabiliana nayo kupelekea kuwaza sana na hii huitwa SONONA.

Je, nini kimefanya wewe uwe na msongo wa mawazo?

Msongo wa mawazo unapelekea mtu kujiua, kupata vidonda vya tumbo, kuishi wa wasiwasi na hofu kupitia kiasi, kupata shinikizo la damu, kuwa mchovu kupita kiasi, kuishi kwa kujitenga na kuwa mpweke muda mwingi.
Kabla ya kuendelea...

Msongo wa mawazo hauna faida yeyote zaidi hasara zake ni mbaya kama ambayo nimetaja hapo juu.

Kwa maana hiyo mimi na wewe tuna wajibu wa kupambana na msongo wa mawazo ambayo kwa namna moja au nyingine hauepukiki kabisa unamkuta mtu yeyote mahali popote.

Upo tayari kujua ufanye nini pale unapotia hali ya msongo wa mawazo kwenye maisha yako?

Fanya mambo yafuatayo kukabiliana na msongo wa mawazo;



1. Tafuta watu ambao unawaamini tatizo au changamoto ambayo unapitia

Kuna tatizo au changamoto ambayo imefanya wewe uwe na msongo wa mawazo inaweza kuwa mpenzi wako kakusaliti, umefeli masomo, biashara imefeli, unapitia kipindi kigumu cha kifedha n.k.

Unapowaeleza watu wenye hekima watakupa ushauri na mawazo mapya ambayo yatafungua akili yako.
Na kupata kuona kumbe siyo mwisho inawezekana kuvuka kwenye kipindi kigumu unachopitia pia wahenga wanasema “Nyakati ngumu maishani hazidumu”.

2. Fanya mazoezi,
Inawezekana unashangaa ni kwa namna gani si ndiyo? Ni kwamba mazoezi yanasaidia mwili kuwa active na mzunguko wa damu kuwa mzuri kwa maana hiyo unapofanya mazoezi inasaidia.

Ni hivi....

Mfano zoezi la kukimbia au kufanya mazoezi ya viungo linasaidia ubongo kupata kufikiri kwa upya na kupata majawabu yale ambayo unapitia.
Fanya mazoezi inasaidia usiwe mtu wa kuwaza sana badala yake unakuwa umakini wako unakuwa kwenye mazoezi.

3. Chukua Muda wa kujifunza/kusoma.

Unakubaliana na mimi kuwa kujifunza hakuna mwisho?

Kujifunza kunasaidia kujenga mtazamo chanya ambao utasaidia kufikiria suluhu ya kutatua tatizo lako au changamoto yako na siyo kufikiria tatizo tu kuona ndiyo mwisho.

Jifunze kwa kusoma vitabu, sikiliza Podcast au audbooks, kuhudhuria semina na kutazama video youtube.

Kujifunza kunakupa fursa ya kuona kwa upana zaidi ya tatizo na namna ya kulitatua na kukutoa kwenye janga la kuwa mtu wa kuwaza sana matatizo na changamoto ambazo unapotia.

4. Mwamini na kumshukuru Mungu.
Mungu alituumba kwa kusudi fulani na tumezaliwa kuwa washindi na siyo kushindwa. tumshukuru Mungu na kusonga mbele.
Msongo wa mawazo ambao unakuja mbele yako hakikisha unaushinda na siyo kukushinda wewe.
Una nguvu kubwa ambayo pengine usingeijua bila tatizo ambalo limefanya wewe uwe na msongo wa mawazo.
Shinda msongo wa mawazo kwa kuamini Mungu amekupa nguvu hiyo ya kushinda.

5. Tumia muda na marafiki wa kweli,
Marafiki wa kweli wanakusaidia kuona unapendwa, unathaminiwa na wanakupa nguvu zaidi ya kuona unaweza kushinda hali ambayo inafanya uwe na msongo wa mawazo.

Marafiki wa kweli wanakupa faraja na kukusaidia kukupa majibu ya tatizo au changamoto na namna gani unaweza kupita na kusonga mbele.

Je, marafiki zako wa kweli ni wakina nani?

Epuka sana kuwa mpweke na kukaa pekee yako muda mwingi kwa sababu unaweza kupata mawazo mabaya pengine kujiua au kujidhuru.

6. Tafuta suluhu ya tatizo au changamoto yako.
Huwezi kutatua tatizo kwa kuongeza matatizo badala yake unaweza kutatua tatizo kwa kutafuta suluhu si ndiyo eeh!

Basi tafuta suluhu kwa kuomba msaada kwa marafiki wa kweli pia ushauri kwa watu wenye hekima na busara.
Tafuta suluhu ambayo itakusaidia kutatua kisababishi cha wewe kuwa mtu mwenye msongo wa mawazo.

Je ni suluhu gani unadhani itakusaidia kutatua tatizo hilo linalofanya uwe na msongo wa mawazo?

7. Ondoa takataka zote kwenye akili yako.
Msongo wa mawazo unafanya mtu kujifunga gerezani yeye mwenyewe kwa kujenga chuki moyoni.

Acha kuishi kwa kinyongo moyoni na kubeba kumbukumbu mbaya za zamani ambazo zinakufanya uwe mtu wa kuwaza kila wakati hiyo ipo nje ya uwezo wako usijisumbue.

Ondoa takataka moyoni na akili kwa kutoa chuki, uwivu mbaya, kinyongo, hasira n.k ambazo zinafanya uwe mtu wa msongo wa mawazo.

Jifunze kusamahe kisha uendelee kuishi kwa amani ya moyo na afya nzuri ya akili.

Na imani umejifunza ni kwa namna gani unapaswa kukabiliana na msongo wa mawazo kabla ya kuwa sonona na kuwa kazi kukabaliana nayo, nakutakia utekelezaji mwema.

Umejifunza nini kwenye makala hii?
 
Kuacha msongo wa mawazo ni ngumu mtu unakuta ni mtendaji wa kijiji kijiji kimewekewa million 25 ,ya kujenga zahanat mtu anakula
 
Back
Top Bottom