makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,218
Wana JF na Watanzania wote,
Nimetafakari kwa kina sana na kugundua kuwa CCM walianza mapema sana kuweka mbinu za kimkakati za kuchukua Dola kwa awamu hii ya 5. Kuna sababu kadha wa kadha lakini zilizo muhimu sana ziko kama 4 na nitaziainisha hapa chini. Kuna watu watajaribu kupinga kwa interest zao lakini ubaki utabaki kama ulivyo na historia itakuja kuhukumu siku moja. Nitazitaja hapa chini na kutolea maelezo mafupi.
1. SHERIA YA CYBER CRIME ILIYOWASILISHWA KWA HATI YA DHARURA BUNGE LA MWISHO NA KUPITISHWA.
2. SHERIA YA TAKWIMU ILIYOWASILISHWA SAMBAMBA NA HIYO YA KWANZA.
3. MATUMIZI MABAYA YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUWATIA HOFU NA KUWATISHA WAPIGA KURA.
4. MATUMIZI MABAYA YA TAKUKURU(PCCB) KWA KUFUMBIA MACHO RUSHWA KWA WAGOMBEA WA CCM.
1. Sheria ya Cyber Crime. Kwa Mtanzania yeyote mwenye akili timamu kwa sasa anajua kwanini sheria hii
iliwasilishwa kwenye Bunge la mwisho kwa Hati ya dharura kana kwamba nchi ilikuwa inaelekea kwenye
kiyama kwamba sheria hiyo ilikuwa lazima itungwe, ipitishwe, isainiwe na Rais na ianze kutumika mara
moja.Sheria hii ilitungwa maksudi ili kuisaidia CCM kwa kudhibiti wale wote ambao wangeweza kutoa
taarifa tafauti na matokeo ya Tume yaliyokuwa yamekusudiwa(Uchakachuaji)! Tumeshuhudia matokeo ya
kwenye vituo vya kupigia kura yakipokelewa na Tume tofauti na matokeo halisi ya vituoni na hapohapo
Tume ikishirikiana na Serikali kuwadhibiti wengine wote wasifanye TALLYING(Majumuisho) ili kuficha siri hiyo.Pamoja na Wabunge wa upinzani kuipinga na baadhi ya wale wa CCM ilipitishwa.
2. Sheria ua Takwimu: Sheria hii ya Takwimu kama ilivo ile ya kwanza hapo juu ilitungwa kwa mtindo uleule kwa
masksudi maalumu ili kulinda maslahi ya CCM na Serikali iliyoko Madarakani. Sheria hii ilipitishwa kwa
lazima ili kuhakikisha kwamba Takwimu za Tume kwa maana ya idadi ya wapiga kura na matokeo
vinadhibitiwa na sheria hii. Kwamba mtu mwingine yeyote asije na matokeo tofauti na yale ya Tume
hata kama ni ya uongo! Hili wamefanikiwa kwa vile tumeona idadi ya Kura zilizopigwa vituoni haindeni
na kile Tume ilikuwa ikiwsilisha kwenye Majumuisho yake. Yote hii ilikuwa ni kuhakikisha Wapinzani
hawaji na takwimu zile za ukweli toka Vituoni ili kuficha kushindwa kwa CCM.
3. Matumizi mabaya ya vyombo vya Ulinzi na Usalama:
Tangu mwanzo kabisa wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2015 tulianza kuona mazoezi ya Ndege za Kivita,
Wanajeshi, Polisi na Watu wa Usalama wakifanya mazoezi makali kana kwamba nchi ilikuwa inaenda
kuingia vitani. Kuna jamaa yangu mmoja aliniambia kabla ya Uchaguzi kuwa Jeshi la Wananchi(JWTZ)
lilikuwa limewekwa katika hali ya tahadhari kana kwamba chochote kingeliweza kutokea kabla au baada ya Uchaguzi. Alisema kwamba wakubwa wa Jeshi walikuwa wanajua zaidi nini kilikuwa kikiendelea! Hali hiyo ilipelekea baadhi ya watu kutoenda kupiga kura na kuna waliokimbilia nchi za jirani mpaka Uchaguzi uishe salama.
4. Matumizi mabaya ya TAKUKURU (PCCB):
TAKUKURU kikiwa ni chombo chenye kupambana na Kuzuia Rushwa kilionywa kisiingilie kabisa mtandao wa Wapiga Kura wa CCM tangu kura za Maoni mpaka Upigaji kura ili kuwapa nafasi Waheshimiwa wenye nchi wafanye vitu vyao pasipo bughudha. Ndicho kilichotokea, hakuna asiyejua kuwa Watia nia wa Urahisi na Wagombeaji wote wa Ubunge waliachwa watembeze rushwa pasipo kuguswa ili washinde kiulaini. Mpaka sasa hakuna kesi yoyote ya Kigogo wa CCM kwa kosa la kutoa rushwa au kupokea
rushwa pamoja na matukio kama hayo kuwepo!!!
Hiyo ndiyo itakayokuwa Serikali ya Magufuli awamu ya 5 ambayo imeinga kwa mizengwe, wizi wa kura na kamatakamata ya Watanzania hasa wale wote waliokuwa wanaonyesha dalili za kutaka mabadiliko kupitia UKAWA/CHADEMA na LOWASSA.
Mungu ibariki Tanzania nchi yangu. Nina hakika kuna siku utaondokana na minyororo hii ya Watawala na Makaburu weusi wa CCM. Amina.