Ruto asema Majaji ni Wala Rushwa wakubwa na wanaendeshwa na Wanasiasa, asema Wananchi waamue atupa kule Hukumu ya mahakama!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,036
Dr Ruto amewaambia live Majaji kwamba wao ni Wala Rushwa wakubwa na wanaendeshwa na Wanasiasa

Rais Ruto ni kama amerudia kauli ya Mwanasiasa Maarufu nchini na Africa Mashariki Rostam Aziz kwamba Majaji huamua kwa Rushwa na kupigiwa Simu Moja tu

Ruto amemtaka Katibu mkuu wa Ujenzi kuendelea na Ujenzi wa barabara pamoja na Uwepo wa Zuio la mahakama, Ruto amesema Wananchi ndio mahakama ya Haki

Source: Citizen TV
 
Mie nilidhani ni Tanganyika tu

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Dr Ruto amewaambia live Majaji kwamba wao ni Wala Rushwa wakubwa na wanaendeshwa na Wanasiasa

Rais Ruto ni kama amerudia kauli ya Mwanasiasa Maarufu nchini na Africa Mashariki Rostam Aziz kwamba Majaji huamua kwa Rushwa na kupigiwa Simu Moja tu

Ruto amemtaka Katibu mkuu wa Ujenzi kuendelea na Ujenzi wa barabara pamoja na Uwepo wa Zuio la mahakama, Ruto amesema Wananchi ndio mahakama ya Haki

Source: Citizen TV
Safi kabisa....tabia ya kuchekeana ni very irritating..
We miss you JPM.
Pumzika kwa amani mwamba.
 
Sasa hapo anaonyesha mfano mbaya kwa Taifa lake.maana kushindwa kuheshimu na kuamini mahakama za nchini mwake anatoa mwanya kwa watu wengi zaidi na maafisa wengi zaidi wa serikali yake na matajiri wengi na wenye pesa zao kufanya maamuzi bila hofu wala uoga kwa kutambua kuwa hata hukumu ikitoka basi hawataiheshimu .

Lakini pia hakuna muwekezaji anayeweza kupenda kuwekeza mahali ambapo mihimili kama mahakama haiheshimiwi.kauli hiyo maana yake inawakimbiza wawekezaji na kuwakosesha imani kwa mifumo ya ndani ya utoaji haki kama vile mahakama. maana yake anataka yeye ndiye kuwa mahakama mwenyewe na muamuzi mwenyewe.jambo ambalo kwa wenye akili hawawezi kuliunga mkono maana anataka kuendesha nchi kibabe kama nyampara.

Pia kauli hiyo inaweza kuchochea Vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na kujichukulia sheria mkononi kwa wananchi kwa kutambua kuwa maamuzi ya mahakama hayaheshimiwi na yanaweza kupuuzwa na kutupiliwa mbali na hivyo dawa ni kumalizana tu.

Kama anaona wananchi ndio watoa haki basi asimamishe mfumo wa mahakama ili kesi zote na mashitaka yote yawe yanapelekwa kwa wananchi wasio juwa hata vifungu vya sheria.lakini pia kauli hiyo ni shambulizi dhidi ya mahakama na mifumo yote ya utoaji haki.

Lakini pia kauli hiyo itawaumiza zaidi wanyonge na maskini kwa kukosa kimbilio la kupata haki zao,hasa pale kesi inapokuwa inawahusu wakubwa na wenye pesa zao au matajiri kwa kuwa watazichezea na kuzidharau hukumu na amri za mahakama na hivyo kuwafanya masikini kuishi kwa kukata Tamaa huku mioyo yao ikiwa inabubujikwa na machozi kwa kukosa mahali pa kukimbilia.jambo Ambalo Ni la hatari sana kwa usalama wa Taifa na utulivu maana watu wanaweza kuingia barabarani kwa kujitoa mhanga bila uoga kwa kusema bora kifo cha heshima cha kupigania haki zao kuliko kuishi kwa mateso ya kuonewa na kudhulumiwa haki zao.
 
Dr Ruto amewaambia live Majaji kwamba wao ni Wala Rushwa wakubwa na wanaendeshwa na Wanasiasa

Rais Ruto ni kama amerudia kauli ya Mwanasiasa Maarufu nchini na Africa Mashariki Rostam Aziz kwamba Majaji huamua kwa Rushwa na kupigiwa Simu Moja tu

Ruto amemtaka Katibu mkuu wa Ujenzi kuendelea na Ujenzi wa barabara pamoja na Uwepo wa Zuio la mahakama, Ruto amesema Wananchi ndio mahakama ya Haki

Source: Citizen TV
Asijidanganye, anaweza akawajibishwa kisheria na inaweza ikamgharimu yeye mwenyewe binafsi pamoja na Urais wake. Katiba ya Kenya ni nzuri, hairuhusu huo Udikteta wake anaotaka kuufanya.
 
Naona Mh kapiga chini ya MKANDA,angeomba kesi zenye MASLAHI makubwa kwa nchi ,ziwe zina amriwa ndani ya MUDA mfupi ,mfano mchakato wa kupinga/ kuhoji Matokeo ya Urais Kenya
 
Sasa hapo anaonyesha mfano mbaya kwa Taifa lake.maana kushindwa kuheshimu na kuamini mahakama za nchini mwake anatoa mwanya kwa watu wengi zaidi na maafisa wengi zaidi wa serikali yake na matajiri wengi na wenye pesa zao kufanya maamuzi bila hofu wala uoga kwa kutambua kuwa hata hukumu ikitoka basi hawataiheshimu .

Lakini pia hakuna muwekezaji anayeweza kupenda kuwekeza mahali ambapo mihimili kama mahakama haiheshimiwa.kauli hiyo maana yake inawakimbiza wawekezaji na kuwakosesha imani kwa mifumo ya ndani.hapo maana yake anataka yeye ndiye kuwa mahakama mwenyewe na muamuzi mwenyewe.

Pia kauli hiyo inaweza kuchochea Vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na kujichukulia sheria mkononi kwa wananchi kwa kutambua kuwa maamuzi ya mahakama hayaheshimiwa na yanaweza kupuuzwa na kutupiliwa mbali na hivyo dawa ni kumalizana tu.

Kama anaona wananchi ndio watoa haki basi asimamishe mfumo wa mahakama ili kesi zote na mashitaka yote yawe yanapelekwa kwa wananchi wasio juwa hata vifungu vya sheria.lakini pia kauli hiyo ni shambulizi dhidi ya mahakama na mifumo yote ya utoaji haki.
Sahihi Kabisa

Ukiweka Uchawa pembeni unakuwaga na Hoja Kiasi fulani 😂
 
Dr Ruto amewaambia live Majaji kwamba wao ni Wala Rushwa wakubwa na wanaendeshwa na Wanasiasa

Rais Ruto ni kama amerudia kauli ya Mwanasiasa Maarufu nchini na Africa Mashariki Rostam Aziz kwamba Majaji huamua kwa Rushwa na kupigiwa Simu Moja tu

Ruto amemtaka Katibu mkuu wa Ujenzi kuendelea na Ujenzi wa barabara pamoja na Uwepo wa Zuio la mahakama, Ruto amesema Wananchi ndio mahakama ya Haki

Source: Citizen TV
Mahakimu wa Tanganyika ndio wenye njaa kali kuliko wa Kenya. Rostam Aziz yupp sasa.
 
Sasa hapo anaonyesha mfano mbaya kwa Taifa lake.maana kushindwa kuheshimu na kuamini mahakama za nchini mwake anatoa mwanya kwa watu wengi zaidi na maafisa wengi zaidi wa serikali yake na matajiri wengi na wenye pesa zao kufanya maamuzi bila hofu wala uoga kwa kutambua kuwa hata hukumu ikitoka basi hawataiheshimu .

Lakini pia hakuna muwekezaji anayeweza kupenda kuwekeza mahali ambapo mihimili kama mahakama haiheshimiwa.kauli hiyo maana yake inawakimbiza wawekezaji na kuwakosesha imani kwa mifumo ya ndani.hapo maana yake anataka yeye ndiye kuwa mahakama mwenyewe na muamuzi mwenyewe.

Pia kauli hiyo inaweza kuchochea Vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na kujichukulia sheria mkononi kwa wananchi kwa kutambua kuwa maamuzi ya mahakama hayaheshimiwa na yanaweza kupuuzwa na kutupiliwa mbali na hivyo dawa ni kumalizana tu.

Kama anaona wananchi ndio watoa haki basi asimamishe mfumo wa mahakama ili kesi zote na mashitaka yote yawe yanapelekwa kwa wananchi wasio juwa hata vifungu vya sheria.lakini pia kauli hiyo ni shambulizi dhidi ya mahakama na mifumo yote ya utoaji haki.
Hivi Comment hii kweli imeandikwa na Lucas Mwashamba ninayemfahamu au simu yake leo amemuachia mtu mwingine??????????!!!!!!!!!!!!!???
 
Sasa hapo anaonyesha mfano mbaya kwa Taifa lake.maana kushindwa kuheshimu na kuamini mahakama za nchini mwake anatoa mwanya kwa watu wengi zaidi na maafisa wengi zaidi wa serikali yake na matajiri wengi na wenye pesa zao kufanya maamuzi bila hofu wala uoga kwa kutambua kuwa hata hukumu ikitoka basi hawataiheshimu .

Lakini pia hakuna muwekezaji anayeweza kupenda kuwekeza mahali ambapo mihimili kama mahakama haiheshimiwa.kauli hiyo maana yake inawakimbiza wawekezaji na kuwakosesha imani kwa mifumo ya ndani.hapo maana yake anataka yeye ndiye kuwa mahakama mwenyewe na muamuzi mwenyewe.

Pia kauli hiyo inaweza kuchochea Vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na kujichukulia sheria mkononi kwa wananchi kwa kutambua kuwa maamuzi ya mahakama hayaheshimiwa na yanaweza kupuuzwa na kutupiliwa mbali na hivyo dawa ni kumalizana tu.

Kama anaona wananchi ndio watoa haki basi asimamishe mfumo wa mahakama ili kesi zote na mashitaka yote yawe yanapelekwa kwa wananchi wasio juwa hata vifungu vya sheria.lakini pia kauli hiyo ni shambulizi dhidi ya mahakama na mifumo yote ya utoaji haki.
We fukara unaongea nini?...
Kenya sio level yenu elewa hilo kwanza sawa chawa?..
Endelea na ajira yako ya uchawa ..
 
Dr Ruto amewaambia live Majaji kwamba wao ni Wala Rushwa wakubwa na wanaendeshwa na Wanasiasa

Rais Ruto ni kama amerudia kauli ya Mwanasiasa Maarufu nchini na Africa Mashariki Rostam Aziz kwamba Majaji huamua kwa Rushwa na kupigiwa Simu Moja tu

Ruto amemtaka Katibu mkuu wa Ujenzi kuendelea na Ujenzi wa barabara pamoja na Uwepo wa Zuio la mahakama, Ruto amesema Wananchi ndio mahakama ya Haki

Source: Citizen TV
Mahakama hiyo hiyo ndio ilipelekea yeye kua rais maana Ni kweli Ruto aliiba kura. Anyway sitamshangaa màana hata rais wa Undengestan aliye wekwa kwenye kiti Cha urais na katiba baadaye aliiponda katiba hiyo hiyo akisema katiba Ni kijitabu tu.
 
Majaji ni kweli Wala rushwa Wakubwa ila kauli kama hiyo haikutakiwa kutolewa na Rais wa nchi naona haijakaa sawa
 
Back
Top Bottom