Russia kuiuzia Uganda mafuta kwa bei rahisi, Museveni ataka nafaka na ngano

Nicolaus Trac

Member
Dec 21, 2012
5
3
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov amesisitiza kwamba Russia haihusiki kwa vyovyote vile na ongezeko la bei ya bidhaa muhimu kote duniani, na kwamba taarifa hizo zinaenezwa na nchi za Magharibi ili kueneza chuki dhidi yake.

Amesema hayo akiwa Kampala, Uganda katika ziara yake ya nchi nne za Afrika.

Uganda ni nchi ya tatu kwenye ziara yake Afrika. Sergey Lavrov ameendelea kusisitiza kwamba Russia haihusiki kwa vyovyote na ukosefu wa nafaka, ngano, mafuta na kupanda kwa gharama ya maisha kote duniani, kama inavyoripotiwa kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine.

Lavrov amedai kwamba mataifa ya Magharibi yamekuwa na hulka ya kuilaumu Russia kwa kila baya, akisema kwamba gharama ya maisha ilianza kupanda kabla ya vita vya Ukraine, kwanza kutokana na janga la virusi vya Corona.

Licha ya kudai kwamba Russia haihusiki na hali mbaya ya uchumi duniani, amedai kwamba vikwazo vya mataifa ya Magharibi dhidi ya Russia ndiyo vimechangia hali hiyo, kwa kuvuruga usafirishaji wa bidhaa muhimu.

Mafuta kwa Uganda kutoka Russia
Amesema kwamba Russia ipo tayari kuiuzia Uganda mafuta kwa bei rahisi.

“Tunauza mafuta kwa nchi ambazo zipo tayari kushirikiana nasi. Kama kuna nchi inataka kununua mafuta yetu, iwe India au Afrika, hatuna kizuizi chochote.” Amesema Lavrov, akiongezea kwamba “siyo tu kwamba tunauza mafuta, lakini pia tunatoa msaada katika sekta nyingine za maendeleo katika sekta ya mafuta. Tupo tayari vile vile kufanya mazungumzo na Uganda kuhusu swala hili.”

Russia ilikuwa inauza mapipa milioni 2.5 ya mafuta kila siku kabla ya kuwekewa vikwazo kutokana na vita dhidi ya Ukraine kuanza. Kufikia sasa, Mafuta ya dizeli kutoka Russia kuelekea Afrika imefikia tani milioni 1 tangu kuanza kwa mwaka huu. Kiasi kikubwa cha mafuta hayo kinaingia Senegal na Togo.

Museveni anataka maelezo kuhusu usafirishaji wa nafaka
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema kwamba anataka maelezo kutoka kwa Lavrov sababu zinazopelekea nafaka na mbolea kutofika soko la kimataifa kutoka Russia na Ukraine licha ya kwamba
havijawekewa vikwazo.

Amesema kwamba maelezo ya Lavrov ni kwamba mataifa ya Magharibi yamezuia meli za Russia kuingia katika bandari kadhaa duniani na hivyo bidhaa hizo haziwezi kusafirishwa.

“Ameniambia kwamba mataifa ya Magharibi yamezuia meli za Russia kusafirisha nafaka katika bandari mbalimbali duniani kwasababu ya vikwazo.” Amesema rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Tani milioni 22 za ngano zimekwama katika bandari za Ukraine tangu kuanza kwa vita vya Ukraine.

Russia iliishambulia bandari kwa mabomu baada ya kusaini mkataba wa kusafirisha nafaka
Russia na Ukraine zilisaini makubaliano ya kusafirisha nafaka baada ya mazungumzo yaliyoongozwa na Uturuki Pamoja na umoja wa mataifa.

Hata hivyo Russia ilishambulia bandari ya Odessa, saa chache baada ya mkataba kusainiwa. Uganda inasisitiza kwamba haitajiingiza katika mgogoro kati ya Russia na Ukraine, na kwamba Russia imekuwa Rafiki wa mda mrefu na itaendelea na ushirika wao kwa kila hali licha ya vikwazo vya nchi za magharibi.

Umoja wa ulaya unasema ziara ya Lavrov ni ya kueneza uongo
Balozi wa Umoja wa ulaya nchini Marekani Stavros Lambrinidis, anasema kwamba ziara ya Sergei Lavrov Afrika ni ya kueneza propaganda na uongo baada ya kujua vizuri kwamba uvamizi wa Russia nchiniUkraine unaendelea kuathiri duniani kwa jumla.

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika, Lambrinidis amesema kwamba Russia inaendelea kuvuga kanuni zote za amani duniani, na ni lazima iwajibishwe na kuheshimu sheria ya kimataifa.

Mataifa ya magharibi yanasisitiza kwamba vikwazo dhidi ya Russia vimeanza kuiumiza nchi hiyo na hivyo Lavrov anatafuta soko kwa bidhaa zake.

Lavrov anatarajiwa mjini Addis Ababa, Ethiopia, makao makuu ya umoja wa Afrika, ambapo wachambuzi wa siasa za Afrika wanasema kwamba ziara yake nchini Ethiopia ni ishara kwamba ametembelea nchi zote za Afrika kabla ya kuwa mwenyeji wa kongamano la viongozi wa Afrika mjini Moscow, mwaka ujao.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

kagutamuseveni_295959599_631376458406534_8635293936630796353_n.jpg

Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kulia) akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov katika ikulu ya rais ya Entebbe, Uganda. July 26, 2022. PICHA: Ofisi ya rais wa Uganda
 
Ok sio shida atajijua

Urusi imewekewa vikwazo hadi vya usafiri zikiwemo.meli zake

Hiyo ngano au mafuta yatafika Uganda kwa kutumia meli zipi? Au ndege zipi
 
Ok sio shida atajijua

Urusi imewekewa vikwazo hadi vya usafiri zikiwemo.meli zake

Hiyo ngano au mafuta yatafika Uganda kwa kutumia meli zipi? Au ndege zipi
Huyo Waziri wa mambo ya kigeni wa Russia amekuja Uganda kwa miguu?
 
Back
Top Bottom