Rushwa kubwa ni sababu ya upungufu wa dola kwenye mzunguko

Nchi yetu imekumbwa na upungifu mkubwa wa fedha za kigeni hususani dola ya kimarekani na hovyo kuanza kusababisha madhara makubwa iliwrmo kupanda bei za bidhaa hasa inayoagizwa nje kama mafuta. U ukiangalia miamala inayotumika katika malumbano ya ubinafsishaji wa bandari na tetesi zilizopo za watu kulipwa fedha nyingi kutetea au kupinga uwekezaji basi kuna fedha nyingi ipo majumbani kwa watu badala ya kuwa kwenye mzunguko. Ruhusa ya biashara ya fedha za kigeni nje ya mabenki bila kuweka udhibiti wowote vinafanya haya maduka ya kigeni kutumika katika kutoa au kupokea rushwa. Juhudi kubwa za maksudi zinahitajika kabla mambo hayajaharibika zaidi.
Tatizo tuna rais failure
 
Hajamaanisha hatupati kabisa Dola, bali tunazipata kwa kiwango kidogo sana compared to tunavyozihitaji kwa ajili ya importation.

Yaani sisi ni nchi ambayo importations (USD outflow) zimezizidi Kwa kiwango kikubwa exportation (USD inflow) hivyo net flow ni negative kwetu.
Shida ya dola nilianza kuisikia kenya kabla haijakuja kwetu Kenya hawakuwahi kuwa na uhaba wa dola ila mwaka jana iliwakuta hadi Ruto akaanza kupiga mikwara kuwa atahamia kwenye currency nyingine .kuna mdau amewahi kusema hapa kuwa . Us kaamua kupunguza mzunguko wa pess yake duniani ndo huu uhaba.
Looks like Us ataendelea kuwa superpower kwa miaka mingi sana mbele.
 
Magufuli, a visionary leader, aliona uhuni wa wafanyabishara wa fedha za kigeni. Akaweka safeguards kwenye hiyo biashara.

Lakini ndio vile tena kwasasa nchi inaongozwa na mtu aliyeshikwa masikio na wafanyabishara. Watauchezea uchumi kwa kadri wanavyotaka.
Jiwe alikuwa na akili kama zako
 
Tatizo la Tanzania kukosa Dola sehemu kubwa ni kutokana na kutouza nje kitu chochote zaidi ya kununua nje hadi njiti za kuchokonolea meno.
Pamoja na hii sababu,mimi naona kuna sehemu tumejipiga pin wenyewe
mfano,unakuta hapa nchini kuna makampuni ya kigeni ambayo transactions zao zote wanafanya kwa dola au uro au stering pounds n.k
Lakini sheria zetu za nchi zinalazimisha wafanyakazi wazawa walipwe fedha ya kitanzania. Mimi nilidhani ndo uzalendo
lakini kilichonishangaza na kunisikitisha nikasikia mkuu wa nchi mmojawapo wa wastaafu enzi za utawala wake akisema''Fedha ya madafu" akimanisha Tshs,iliniuma sana.Nilitegemea yeye awe wa kwanza kuonyesha uzalendo.

Kama wananchi wetu wenye uwezo wa kulipwa fedha ya kigeni hapa nchi wangelipwa hivyo ingezuia wao kunyonywa at the same time nchi ingeendelea kupata fedha ya kigeni kwa kutumia raslimali watu ya taifa ambayo ni raia wake,
badala ya kutegemea mauzo ya bidhaa nje ya nchi peke yake.

Bidhaa kama dhahabu,almasi n.k,hata zikiuzwa,anayeuza ni wa kigeni(mwekezaji) pesa anapeleka kwao,sisi tunalipwa Tshs.
Sasa kutegemea kuuza mazao ya kilimo,hadi upate fedha nyingi ya kigeni ni leo?
Tujitafakari kwa kina
 
Nchi yetu imekumbwa na upungifu mkubwa wa fedha za kigeni hususani dola ya kimarekani na hovyo kuanza kusababisha madhara makubwa iliwrmo kupanda bei za bidhaa hasa inayoagizwa nje kama mafuta. U ukiangalia miamala inayotumika katika malumbano ya ubinafsishaji wa bandari na tetesi zilizopo za watu kulipwa fedha nyingi kutetea au kupinga uwekezaji basi kuna fedha nyingi ipo majumbani kwa watu badala ya kuwa kwenye mzunguko. Ruhusa ya biashara ya fedha za kigeni nje ya mabenki bila kuweka udhibiti wowote vinafanya haya maduka ya kigeni kutumika katika kutoa au kupokea rushwa. Juhudi kubwa za maksudi zinahitajika kabla mambo hayajaharibika zaidi.
Tulimsikia mojawapo wa mawaziri kichwamaji wa samia nape akitamba kwamba wanawarudishia waliyofungiwa bureau de change hela zao na pia kuwaruhusu wafungue upya. Utafikiri yeye ndio waziri wa fedha kwa jinsi alikua anatamba au utafikiri yeye ni mtoto wa samia au mkwe. Bila hata kusema kwa nini walifungiwa na kunyang'anywa hela. wala bila kusema utaratibu wa bureau de change kua kwenye mabenki umedhoofisha nini. Yote ili kumnanga jpm. Ona sasa sera zao za ubinafsi nchi haina hela za kigeni. Juzi tu BoT walitamba wana hela nyingi za kutosha za kigeni kuagiza bidhaa kutoka nje kwa miezi minne kama sijakosea, kumbe uongo tu hawana. Hela za kigeni ziko mkononi kwa wafanya biashara wahindi. Wakikubaliana misikiti kwao wanapoweka mikakati wabane hela zao nchi inayumba. Hii ndio tanzania samia anajenga.
 
The Boy Wonder si mlituambia kwa takwimu jinsi dollar imechapishwa sana hadi kuzidi mahitaji, why tena watu wanalia lia kuwa dollar haipatikani kirahisi?

Cc RUSTEM PASHA
Mkuu, Zitto ili kufahamu vizuri kinachoendelea unatakiwa uyafahamu vizuri mambo yafuatayo, siyo tu kukomaa na uchumi ambao tumeusoma daransani:

1. The Banking and International Monetary System.
2. International Trade and Finance.

Mosi, dollar ya Marekani kuchapishwa kwa wingi haimaanishi kwamba itafika nchini Tanzania. Kuna nchi ambazo dola nyingi zilizochapishwa huenda kwao. Juzi nikakuwekea kitu nikategemea utanda kutafuta uone jinsi inavyofanya kazi, lakini inaonyesha hujatafuta. Dollar Liquid Swap Privisions, ndiyo inafanya nchi kadhaa zipate dola na nyingine zikose. Nchi za kama Canada, European Union, United Kingdom, Japan na Switzeland wanachukua dola zote kupitia haya makubaliano kwasababu wana UNLIMITED DOLLAR LIQUID SUPPLY.

Akifuatiwa na Australia, Brazil, South Korea, Mexico, Singapore na Sweden, ambao Dollar Liquid Swap Provision yao ni $ 60 Billion. Hawa nao hufuatiwa na Dernmark, Norway na Newzeland ambao Dollar Liquid Swap Provision yao ni $ 30 Billion. Unafahamu nchi za Africa, hasahasa Tanzania, Dollar Liquid Swap Provision yao ni kiasi gani, kabla hujaniulizia swali, hili, ???

Pili, dollar ya Marekani imeimarika kutokana na marekeni kupandisha riba juu na hili limepelekea masoko yanayokuwa kuathirika. Fedha, za nchi nyingi zilishuka thamani ili kuweza kumudu kununua bidhaa mbalimbali kutoka masoko ya kimataifa. Maana yake basi, nchi nyingi zimekumbwa na DOUBLE BURDEN, yaani mfumuko mkubwa wa bei na gharama za bidhaa kwenye soko la kimataifa. Kungekuwa na Comprehensive Dollar Liquid Swap Stops, kama ilivyokuwa kwingine, kwamba tungeipata dollar tunavyoitaka unadhani haya yangetokea, ???

AU ndugu yangu, nisaidie wewe, unadhani nchi zinavyoenda kununua dollar zinafanyaje, Hebu nisaidie. Maana unauliza maswali na kuendelea kubishana na mimi, ilhali hutui takwimu, wala kunifafanulia, How the Dollar Operates in International Trade. Wewe umekomaa na kanuni zilezile za Uchumi kwamba, Dollar haiwezi kuchapishwa kuzidia bidhaa za masokoni, mara kuna Economic Variables. etc. Yote haya ni muhimu kwenye uchumi, ila wewe ndugu yangu umesahau kuzingatia, How Currencies Affect International Trade and Finance. Kubwa ambalo hujaligusia kabisa ni The Banking and Monetary System. Hapa mimi na wewe ndiyo tunaachana.

Tatu, kuna kukua kwa deni la taifa katika kiwango kisicho cha kawaida. Deni la taifa huwa na kaiwada ya kukaisha hifadhi ya fedha za kigeni kama Dollar. Hivi unadhani deni letu la taifa tunalilipaje. Mbona, hili wewe mchumi hujalizingatia, ukakubaliana moja kwa moja na kila tuhuma unayoisikia mtandaoni, ???

Kumbuka, mbali na kukopa kutoka nje, mwaka jana serikali imefanya, Foreign Debt Restructuring (FDR) kwa mashirika makubwa ya kiserikali kama TPDC na TANESCO, ambapo madeni yao yamehamishiwa kwenye deni la serikali kuu. TPDC na TANESO wana ujumla wa deni lisilipungua Trilioni moja. Mambo kama haya inabidi tuyazingatie sana kabla hatujakimbilia kubishana au kutoa tuhuma.

Nne, kuna suala zima la BALANCE OF TRADE (BOT), ambalo wewe mchumi hujalizingatia. Nchi yetu ya Tanzania ni NET IMPORTER, bidhaa inazoziingia ni nyingi kuliko zile ambazo inaziuza nje kwenye soko la dunia. Ukizingatia na mfumuko wa bei ulivyo kwenye soko la dunia lazima tutumie dola nyingi tu kufanya manunuzi. Hata Nigeria ilikumbwa na tatizo kubwa mno la uhaba wa dollar (Dollar Liquid Crisis) mwaka jana, unadhani tatizo ni rushwa peke yake, ??? Hebu tusaidiane, hapa ndugu mchumi..

Tano, nakubaliana kwa sehemu na ndugu LUS0MYA kasema rushwa ni moja ya sababu kubwa ya kuwepo kwa uhaba wa dollar, lakini kusema ndiyo sababu kuu, hilo siwezi kukubaliana nalo hata kidogo. Ndiyo, rushwa ina madhara makubwa lakini hiyo rushwa ambayo inaweza kusababisha uhaba wa dola nchini, inabidi iwe ya kiwango kama kile cha TEGETA ESCROW au EPA, ikiambatana na utakatishaji wa pesa. Kama utakumbuka kilichotokea mwaka 2014.

Binafsi, mwaka 2014 Mkurugenzi wa PCCB alishaniambia kwenye kikao fulani kwa mdomo wake kwamba, uhaba wa dollar na kushuka kwa thamani ya fedha ya Tanzania kumesababishwa na ufisadi wa ESCROW. Watu walianza kubadilisha mabilioni ya fedha na kuyabadilisha kwenye dola ili wayakimbizie nje ya nchi, jambo ambalo lilisababisha uhaba mkubwa wa fedha za kigeni na kushuka kwa thamani ya fedha yetu. Mtoa mada, LUS0MYA anaposema rushwa inafanyika kwa kiwango kikubwa inabidi atuonesha hiyo mianya hiyo.

Sita, vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi vimepelekea uhaba wa dola duniani, hasa kwenye mataifa yanaendelea. Marekani amehodhi fedha ili kumkomesha Urusi asifanye malipo kupitia dola kumbe anajikomoa na yeye. Nimekuwekea takwimu kwamba, mwaka 2022 baada ya vita kuanza mzunguko wa dollar ya Marekani duniani umepungua kutoka asilimia 75% hadi kufika 59%. Alihisi kwamba angeiumiza Urusi ndani ya muda mfupi na mambo yatarudi kuwa kama hapo mwanzo, kumbe ndiyo hivyo tena, imeshindikana na kuachilia anashindwa.

Maumivu kimya kimya tu, ilhali wenzake kama Urusi na Uchina wamesaini CURRENCY SWAP AGREEMENTS na mataifa mengine duniani, mbinu ambayo inaziunganisha benki kuu za nchi husika ili waweza kutumia fedha nyingine kufanya manunuzi kwenye soko la dunia. Uchina peke yake amesaini CURRENCY SWAP AGREEMENTS 60, hapa anakwepa hadi mifumo kama SWIFT, unadhani utamshinda kirahisi mzee, ???

NB: Nimekuuliza zaidi ya mara nne, kuhusu AUSTRALIA, lakini ukakwepa kunipa majawabu. Nikatagemea utaenda kujitaabisha walau ufanye tafiti kidogo. Nchi ile imeweza kukwepa tatizo la mdororo wa uchumi kwa miaka 30 mfululizo na wala hawajawahi kukumbwa na tatizo la uhaba wa dollar. Mwaka 2008, hawakukumbwa na tatizo la uchumi duniani, ambalo lilitukumba wote. Hivyo basi, AUSTRALIA is a great economic model to be emulated by developing Markets. And from studying the AUSTRALIA model I can give you the following observations:

1. Large and Unsustainable National Debt leads to Liquid Crisis (Dollar Shortage).
2. There's a Trade Imbalance, if a country is A NET IMPORTER, this also leads to Liquid Crisis.
3. Political acts like sanctions, terrorism and corruption, may lead to Liquid Crisis, eg. Qatar in 2017.

Mwisho, unasahau kwamba dollar ya kimarekani mbali na kuuzwa kwa mataifa mengine ya nje, huishia kurudi Marekani. Mataifa mengi huwa hayashikilii akiba za fedha zao za kigeni (Foreign Reserves) kwenye benki kuu zao. Mataifa mengi huzipeleka fedha hizo kwenye soko na mabenki ya Marekani kama njia ya uwekezaji ili kukuza hifadhi zao. Soko la Marekani la mitaji na dhamana (Capital Markets), ndiyo kubwa hapa duniani.

Marekani peke yake anamilikia asilia 46% ya hilo soko ambalo mabenki mabenki kuu duniani kote huwekeza. Fedha ambayo inatumika kwenye hilo soko, ni Dollar ya kimarekani. Fikiria, taifa kama mataifa ya EU, China, Canada, India yanapeleka hifadhi zao kwenye soko la Marekani, hiyo dola itapatikanaje kirahisi wewe mzee, ??? Hebu, hapa pia nisaidie...

Foreign Debt Restructuring (FDR)
Kabla sijaendelea restructuring sio necessarily kwamba deni linakuwa la serikali kuu Bali Kuna financier anaingia katikati mfano kama deni ni USD 1 Billion na linalipwa kwa equal installments kwa miaka 10 kwa interest ya 10% basi financier anakulipia Hilo deni ila anakudai wewe USD 1 Billion kwa equal installments ndani ya miaka 20 kwa riba ya say 15% kwahiyo inaokoa liquidity ya serikali maana deni unalilipa kidogo kidogo kwa miaka mingi so restructuring kamwe haiwezi leta shortage ya dollar in fact inaongeza surplus ya dollar maana short term obligations are transferred to long term obligations.
Mosi, dollar ya Marekani kuchapishwa kwa wingi haimaanishi kwamba itafika nchini Tanzania.
Na ndio hapa mzizi wa mjadala, kama Dollar haifiki Tanzania ilihali Bado demand ipo then kamwe hauwezi sema dollar imezidi mahitaji. Okay utasema Kuna nchi Zina threshold kubwa ya kuhodhi dollars nyingi ila hizo nchi hazifanyi spending? Hatukopi benki zao? Hawana miradi au uwekezaji huku Tanzania? Hawaji kufanya utalii? Ili pesa iwe excess ni lazima supply of money (Currency in circulation na demand deposits na Forex reserves) ziwe zinazidi mahitaji ya dollar au local currency sokoni. Yaani watu wengi Wana dollar kuliko demand ya wauzaji hivyo ndio inflation etc hutokea Sasa huwezi sema inflation ipande ilihali demand for dollar ipo juu nchi nyingi.
Kungekuwa na Comprehensive Dollar Liquid Swap Stops, kama ilivyokuwa kwingine, kwamba tungeipata dollar tunavyoitaka unadhani haya yangetokea, ???
Ndio maana kumewekwa hizo regulations maana Kila mtu akizipata ndio inflation huanzia hapo. Hata Tanzania tu bonds za serikali hauziwi tu Kila mtu maana in future wenye Hela watakua wengi so unakuta beneficiaries ni always wachache Ili maintain value ya pesa.
Dollar Liquid Swap Privisions, ndiyo inafanya nchi kadhaa zipate dola na nyingine zikose
Hii ni kama mkopo mwingine wowote tu lazima uangalie credit worthiness ya mtu Sasa nchi kama Japan kweli utai rank sawa na Cambodia? Ni kama Moody's wakifanya rankings. So lazima tu utawapa wachache wanaweza chochea soko Zima (Spillover/multiplier effects) Ili fedha zishuke huko chini. Sasa kama huko chini hazijafika hyo supply haiwezi kuwa excess kuliko demand

Several African countries have a shortage of US dollars - why this happens and how to fix it

Hii article ya the citizen inaeleza how scarcity ya dollar Africa inachangiwa na low supply of dollar which is contrary to your stance. That's if at all we assume you tend to consider the citizen credible.
 
Dola haipatikani kwa urahisi karibia nchi nyingi afrika
Hata huyo magu unayemsifia asingeweza kufanya chochote ili dola ipatikane labda apore tena pesa za bureau de change .
Wengi wanashindwa kujua hili. Wanadhani ni tz pekee no it's all over Africa. USA wanajaribu kuokoa hela yao maana wanaona iko njiani kudondoka. Na ndio maana hata wameanzisha Digital reserve currency ili mambo yakishindikana waamie huko jumla.
 
Kabla sijaendelea restructuring sio necessarily kwamba deni linakuwa la serikali kuu Bali Kuna financier anaingia katikati mfano kama deni ni USD 1 Billion na linalipwa kwa equal installments kwa miaka 10 kwa interest ya 10% basi financier anakulipia Hilo deni ila anakudai wewe USD 1 Billion kwa equal installments ndani ya miaka 20 kwa riba ya say 15% kwahiyo inaokoa liquidity ya serikali maana deni unalilipa kidogo kidogo kwa miaka mingi so restructuring kamwe haiwezi leta shortage ya dollar in fact inaongeza surplus ya dollar maana short term obligations are transferred to long term obligations.

Na ndio hapa mzizi wa mjadala, kama Dollar haifiki Tanzania ilihali Bado demand ipo then kamwe hauwezi sema dollar imezidi mahitaji. Okay utasema Kuna nchi Zina threshold kubwa ya kuhodhi dollars nyingi ila hizo nchi hazifanyi spending? Hatukopi benki zao? Hawana miradi au uwekezaji huku Tanzania? Hawaji kufanya utalii? Ili pesa iwe excess ni lazima supply of money (Currency in circulation na demand deposits na Forex reserves) ziwe zinazidi mahitaji ya dollar au local currency sokoni. Yaani watu wengi Wana dollar kuliko demand ya wauzaji hivyo ndio inflation etc hutokea Sasa huwezi sema inflation ipande ilihali demand for dollar ipo juu nchi nyingi.

Ndio maana kumewekwa hizo regulations maana Kila mtu akizipata ndio inflation huanzia hapo. Hata Tanzania tu bonds za serikali hauziwi tu Kila mtu maana in future wenye Hela watakua wengi so unakuta beneficiaries ni always wachache Ili maintain value ya pesa.

Hii ni kama mkopo mwingine wowote tu lazima uangalie credit worthiness ya mtu Sasa nchi kama Japan kweli utai rank sawa na Cambodia? Ni kama Moody's wakifanya rankings. So lazima tu utawapa wachache wanaweza chochea soko Zima (Spillover/multiplier effects) Ili fedha zishuke huko chini. Sasa kama huko chini hazijafika hyo supply haiwezi kuwa excess kuliko demand

Several African countries have a shortage of US dollars - why this happens and how to fix it

Hii article ya the citizen inaeleza how scarcity ya dollar Africa inachangiwa na low supply of dollar which is contrary to your stance. That's if at all we assume you tend to consider the citizen credible.
Mkuu, umesoma kuhusu Restructuring ya deni Tanzania, ???
Unaweza ukatuambia chochote ukilinganisha na hichi unachokisema hapa, ???
 
Mkuu, umesoma kuhusu Restructuring ya deni Tanzania, ???
Unaweza ukatuambia chochote ukilinganisha na hichi unachokisema hapa, ???
Nachoelewa international financing Ina hizo options. Mfano kuna kampuni kubwa za factoring and avalizing so wananunua madeni is either kwa mdeni au mdaiwa ila wanaongeza interest or kupunguza deni Ili Ile difference ndio iwe faida Yao so I believe hata Tanzania Ina exercise hizo options za kuuza madeni kwa financiers wa kimataifa. So in fact restructuring inapunguza demand ya dollars in the short term implying a low dollar demand thus reducing dollar shortage.
 
Back
Top Bottom