Rukwa: Kufikia Mwaka 2035, kabila la Wafipa litakuwa limepoteza "Identity" yake kwa kumezwa na Wasukuma

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Hapa ndipo unaweza kuelewa Kwa nini Wazanzibari Wamekataa kuwa na Muungano wa Taifa Moja na Tanganyika,lengo ni kulinda identity Yao Kwa sababu wao ni minority hivyo wanachelea Kumezwa na kupoteza kabisa na watu wa Bara.

Kabila la Wafipa linalopatikana Mkoa wa Rukwa ambao ndio wenyeji inaelekea litapoteza Utambulisho wake ndani ya miaka 15 ijayo Kwa probably by 2035 Kwa sababu ya Kumezwa na Wasukuma ambao wanahamia na kuzaana Kwa Kasi sana Mkoa wa Rukwa.

Makabila madogo ya Wapimbwe na Wabende ambao ndio wenyeji wa Mkoa wa Katavi wakiwakilishwa na kina Pinda,Kamwelwe na Suleiman Kakoso Kwa Sasa kizazi Chao kimepotea kabisa Kwa Wasukuma.

Ukija Leo Katavi ni kama tuu uko Geita,Simiyu au Misungwi maana ni nadra kuwakuta hao wenyeji.Uhamiaji na Kasi kubwa ya kuzaana ya Wasukuma imepoteza utambulisho wa hayo makabila.

Kilichotokea Katavi ndicho kinaenda kutokea Mkoa wa Rukwa.Mathalani Kwa Wilaya ya Nkasi Kwa Sasa Wasukuma ni wengi kuliko makabila wenyeji.Kwa Wilaya zingine za Mkoa wa Rukwa idadi ya Wasukuma ni kama wako sawa na Wenyeji tofauti kabisa na miaka 10 Iliyopita.

Kwa mujibu wa matokeo ya isensa ya 2022,Kasi ya Ongezeko la watu Mkoa wa Rukwa imeongezeka kutoka wastani wa 3.2% Hadi kufikia growth rate ya 4.3% Kwa sababu ya Wasukuma.Likewise Kwa Katavi Ina growth rate ya 7.1%.

Uhamiaji na Kasi ya kuzaana ya Wasukuma imewafanya Wafipa kuwa mateka na Vibarua maana wameuza maeneo Kwa Wasukuma na Wasukuma kama mnavyowajua ni watu wa kubebana/Kushirikiana na wachapa kazi.

Pamoja na athari hizo za kupoteza Kwa hayo makabila Maarufu Kwa utaalamu wa Radi ila ujio wa Wasukuma umeleta maendelea kama ilivyo Kawaida Kwa Wahamiaji.Wamefungua biashara Mpya,Miji imechangamka,wanalima na kuvumbua maeneo mapya ya Kilimo na wanafuga yaani wameleta mifugo Kila mahala kwenye Mkoa wa Rukwa.
Screenshot_20231031-061536_1.jpg

Swali.
Je nini kifanyike Ili kutunza Utambulisho wa kabila Fulani na kuondoa dominance ya makabila makubwa?

Maana tunakoelekea msije kushangaa Morogoro,Lindi,Pwani na Ruvuma ikawa ni Mikoa ya kabila Moja la Wasukuma.
Screenshot_20231031-064737_1.jpg
Screenshot_20231031-070446_1.jpg
 
Hii ni habari njema sana, ukabila unapaswa ufutike kwa 100% kwa kuwa hauna faida yoyote kwa sasa. Kadri ukabila unavyofutika ndio maendeleo yanaongezeka kwenye maeneo husika.

Kama wachaga na wapare wamejazana kanda ya ziwa, wakimiliki maeneo, wakijenga nyumba, wakiendesha biashara mbali mbali wakioa na kuzaana hiyo maana yake ni utambulisho wa wasukuma inapotea kwa kasi kanda ya ziwa lakini maendeleo yakiongezeka.
 
Hivo vi kabila vya wezi na mataperi haviwezi kamwe kufuta identity ya SUKUMA
 
Back
Top Bottom