Silent Burner
Member
- Feb 25, 2012
- 92
- 30
@Bobuk, tusichanganye mambo, sheria ya Tanzania haitoi UBAGUZI. Hakuna mahali sheria inasema kuwa anayetakiwa kuapa ni yule ambaye amezaliwa kwenye nchi ambayo haikumpa uraia. hakuna. Ili mradi umezaliwa nje ya territorial za Republic unatakiwa ama uape au utoe evidence(uthibitisho) kuwa hauna uraia wa nchi nyingine yoyote. Mbele ya sheria za Tanzania aliyezaliwa Kenya na aliyezaliwa USA wote wanakuwa kwenye kundi moja. Foreign citizen until proven otherwise.
Kwa ruhusa ya mdau Jagermaster naomba niweke ufafanuzi wake ili uone exactly tatizo liko wapi.
"Tanzania tuna uraia wa aina tatu,
(1) Uraia wa Kuzaliwa (citizenship by birth)-Huu napatikana kwa mtu yoyote aliyezaliwa Tanzania with a condition that, mzazi mmoja wapo au (wote) awe either raia wa kuzaliwa au raia wa kwandikishwa.
(2) Raia wa kuandikishwa (citizeship by naturalisation)- Huu hupatikana kwa kuomba, ikiwa raia yoyote wa kigeni anayeishi Tanzania kwa muda usiopungua miaka kumi, au pungufu ya hapo kama waziri ataona inafaa, ambaye anania kubaki Tanzania kwa muda wote wa maisha yake. Huu ndio mara nyingi tunauona kwenye magazeti watu wakiomba
(3) Uraia wa kurithi (citizenship by descent)- Huu ni uraia mtu yoyote aliyezaliwa nje ya Tanzania huku wazazi wake wakiwa Watanzania raia wa kuzaliwa au wa kuandikishwa. Watu wanaozaliwa ikiwa wazazi wao wanafanya kazi kwenye balozi hao watu wanahesabika wamezaliwa Tanzania. Pia ileweke kuwa mtu ukizaliwa kwenye chombo cha usafiri (ndege, meli.e.t.c) unahesabika umezaliwa kwenye nchi ambayo hicho chombo kimeandikishwa
Ileweke kuwa sheria ya uraia ya Tanzania, haitambuwi uraia wa nchi mbili au tatu, with exception kwa mtu mwenye uraia wa kurithi. Raia wa kurithi anaruhusiwa kuwa na uraia wa nchi mbili mpaka pale atakapofikisha umri wa miaka kumi na nane (18) anatakiwa kukana uraia wa nchi nyingine na kubaki na uraia wa Tanzania pekee. Hiki kitendo watu wengi hawakifanyi na price yake wanaipata pale wanapotaka uongozi wa kisiasa
Pia hakuna mahara popote pale ambapo sheria ya uraia ya Tanzania inatoa exception katika kukana uraia kwa mtu mwenye uraia wa kurithi, kwamba either kama huyo mtu kazaliwa kwenye nchi ambayo inatoa automatic citizeship kama US au conditional citizeship kama Kenya kwamba aukane uraia wake wa awali au hapana. Sheria ya Tanzania inawataka watu wote wenye uraia wa kurithi kuukana uraia wa nchi walizozaliwa pale wanapofikisha umri wa miaka kumi na nane, without exception kama Mh Mchemba unavyotaka tuamini. Naona hapo Mh umetumia common sence na sio sheria unavyosema, ni vizuri kama ukaweka ushahidi wa hayo mnayoyaamini. Pia sheria inatoa mwanya wa mtu kupewa uraia hata kama hajakana uraia wa nchi nyingine, ikiwa atathibitisha tu kuwa ni vigumu au haiwezekani kukana uraia wa nchi nyingine ambayo inamtambuwa au haimtambui kuwa ni raia wake
What about SIYOI?
Kwa kesi ya Siyoi ilivyo, yeye anafall katika category ya tatu yaani raia wa Kurithi kwa kuwa alizaliwa Kenya na wazazi watanzania. Wazazi wake walikuwa hawafanyi kazi za ubalozi huko Kenya wakati jamaa anazaliwa.
Pasipo kujali kuwa either Kenya walikuwa wanamtabua kuwa raia wao au hapana, Tanzania ilikuwa inamtambua Siyoi kama raia wa Kurithi yaani alikuwa na uraia wa Kenya na Tanzania na alivyofikisha umri wa miaka 18 kama alishindwa kuukana uraia wa Kenya alipoteza sifa za kuwa raia wa Tanzania. Kwa mazingira yake kama inaonekana ilikuwa ni vigumu kwa yeye kukana uraia wa Kenya kwa kuwa Kenya walikuwa 'hawamtambui' kama raia, alipaswa kupeleka maelezo hayo idara ya Uhamiaji ili wamwelewe kuwa kwa kesi yake hawezi kukana uraia na wa mpe uraia wa Tanzania
Kwa jinsi nilivyosoma sheria ya uraia ya Kenya, Siyoi pia hana sifa ya kuwa raia wa Kenya kwa umri alionaona. Swali sasa linakuja Siyoi ni raia wa aina gani?
Jibu ni jepesi SIYOI SUMARI hana Uraia wa nchi yoyote ile Duniani (Stateless). Watu wa aina hii wapo wengi tu duniani ambao wanaishi kwa kutokuwa na uraia wa nchi yoyote kisheria. Ila kwa Tanzania I know anything can happen
NB
Issue hii ni tofauti na Kesi ya Ulimwengu, licha ya mwamba wote Siyoi na Generali wanajikuta wanakuwa sio raia wa nchi yoyote ile Duniani, Siyoi anapaswa kuukana uraia wa Kenya, kwa kuwa yeye alishawahi kuwa raia wa kurithi mpaka alipofikisha umri wa miaka 18 ndipo uraia wake ulikoma, Ulimwengu hakuwahi kuwa raia wa Tanzania kwani hata Wazazi wake hawakuwahi kuwa raia wa Tanzania, ndio maana yeye aliambiwa aombe uraia wala hakuambiwa aukane tu uraia wa Rwanda.
Kwa maoni yangu sheria ya Uhamiaji ya Tanzania inamapungufu mengi. Ikifika stage kama hizi ndio mapungufu yake yanaonekana. Kwa mfano mpaka sasa raia yoyote wa kurithi, mwenye mke au mume ambaye sio raia wa Tanzania au ni raia wa kurithi, akizaa mtoto nje ya nchi huyo mtoto anakuwa sio raia wa Tanzania, wala uraia wa kurithi haupati. Itampasa huyo mtoto amuombee uraia wa kwandikishwa kama anataka awe Mtanzania.
Wito kwa Watanzania wote wenye uraia wa kurithi nendeni mkakane uraia wa nchi mlizozaliwa, maana kwamtindo huu mkekalia kuti kavu bila kujiju" (MWISHO WA KUNUKUU).
Mkuu FJM, shukrani kwa maelezo ya kina ambayo yametuelimisha wengi juu ya mambo ya uraia na sheria zake.
Hii ndo raha na faida ya JF, ni kisima cha elimu.