Rubani wetu Nini kimekupata? Ndege inayumba

Magufuli 05

JF-Expert Member
May 7, 2023
943
1,988
Niende moja kwa moja.
Toka nianze kufuatilia siasa niwe mkweli wewe ni rubani wa kwanza kuwa na wakati mgumu zaidi hasa katika kipindi hiki cha utandawazi. Najiuliza Nini kimekupata? Mbona abiria Hawana Imani na wewe? Je umejikwaa rubani wetu au huna Nia ya kutufikisha salama. Tazama dege letu zuri na la kifahari dream liner 787-8 kwanini linayumba?
Mimi ni mmoja wa abiria. Nilianza kushtuka pale ulipoapishwa tu kuwa rubani wetu kumalizia safari yetu baada ya rubani wetu wa awali kupatwa na dhoruba. Nilishtuka Sana kwani baada ya kuapishwa tu,ulitengua uteuzi wa director wa Ile taasisi ya mawasiliano ya ndege mzima na ukaweka mwingine. Nikajiuliza ndege yetu ni kubwa na Ina mifumo mingi mbona kaanza na mawasiliano? Nikaona hapa inawezekana rubani huyu na yule mtangulizi wake ilikuwa ni pita kulia Mimi napita kushoto. Yawezekana rubani mpya anataka mawasiliano yake ya nyuma yasiwepo kabisa kwenye kumbukumbu ya director huyu na anataka director mwingine atakaye sitiri.
Lakini nikajiuliza si huyu alikuwa ni rubani msaidizi na kwanini analeta director wa mawasiliano haraka hivyo? Mh! Jibu nikagundua kuna viongozi waandamizi wamemshauri hivyo pengine.
Rubani wetu mpya akazidi kunichanganya zaidi nilipoona ananyofoa mmoja mmoja watumishi wa ndege wale waliokuwa na rubani wa mwanzo Tena kwa Kasi. Nikajua hapa kuna kitu si bure lakini nikajiuliza zaidi kwanini wale rubani wa mwanzo aliwatoa kwasababu za udhaifu na uhuni wa kumtukana wanarudishwa Tena?kama yeye na rubani mtangulizi walikuwa Sawa si na yeye Angeli feel maumivu ya mwenzie kutukanwa na akaachana na Hawa mabwana?
Rubani wetu mpya akaja na mipango yake ya uendeshaji dege letu zuri. Yapo mengi aliyweka kando kabisa lakini lililonishangaza ni lile la gharama za kuunga umeme kwa abiria kutoka 27k na yeye kukataa katakata kwamba haiwezekani Tena. Nikajiuliza mbona akiwa rubani msaidizi alipigia chapuo Sana hili.?
Nikapatwa na mashaka na rubani huyu lakini nikapiga moyo konde na kujisemea kimoyomoyo muda utaamua.
Ningali Bado nashangaa mambo mengi tu ya rubani ghafla likaja zimwi la mkataba mbovu wa uwekezaji wa mifumo mhimu ya ndege. Kelele zikaanza kwa abiria. Abiria wakapuuzwa wakaitwa kila aina ya majina mabaya. Wengine walishushwa kwenye ndege wakapelekwa lockup. Wakapewa kesi za kutaka kumpindua rubani ili wao waendeshe ndege.
Baadae wakasoma alama za nyakati wakawaachia.
Sasa abiria wanapaza sauti rubani kama rubani kweli leseni yake ipo Sawa. Mpaka waraka umetoka ukitaka rubani aachane na mkataba mbovu.
Rubani wetu amejichanganya sehemu, kwanza aliingia mkenge kuwarudisha kwa fujo watumishi waliokuwa wameondolewa na rubani mtangulizi. Pili rubani alijaa haraka kwenye ushauri mbaya ambao mara nyingi kwenye ndege yetu hutolewa na watu wa Dili ambao wakikusoma ulivyo rubani wanakuingiza King fasta.
Rubani wetu ndege imeyumba na kuna wakati abiria tunaona pengine ndege yetu inajiendesha yenyewe(auto pilot) Mimi naona ndege yetu kwasasa abiria wanazidi kuelimika na utandawazi unawasaidia. Wakat wako si ule wa rubani wa 1.2.3.4.5. nionavyo Mimi safari yetu ya mji wa 2025 imekaribia Sana kwani ni masaa 2 yamebaki dege litue. Tafadhali tukifika salama kwa uwezo wa mungu pisha rubani mwingine nawe utasitaafu kwa heshima kwa kupokea kijiti cha urubani katikati ya safari na kutufikisha safarini.
Ahsant
 
Utaambiwa una nongwa sababu rubani ni JINSIA ile, Kutoka islands na ni Dini Ile!!
 
Inawezekana Rubani analeseni ya kufoji mana sio kwa mwendo wa kuyumbisha dege kwa style hii. Kusoma ramani kashindwa hajui atue uwanja upi?
 
mawimbi angani ni jambo la kawaida.
Ruban anayeweza kupambana na mawimbi angani na ndege ikatua salama ndio Rubani mzuri
 
Hii vita ishakuwa ya kidini. Watakuja wahafidhina uchwara wanaofikiria kutumia matumbo yao kubisha kwa vigezo vya dini.
 
Back
Top Bottom