Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Thursday, July 02, 2009 8:32 AM
Rubani wa ndege ya shirika la ndege la Arkefly la Uholanzi ametoa kali ya mwaka kwa kuwashusha abiria wote kwenye ndege na kuendelea na safari ndege ikiwa tupu baada ya kukasirishwa na baadhi ya abiria ambao waligoma kufunga mikanda. Tukio hilo lilitokea ijumaa kwenye uwanja wa ndege wa Schiphol wa jijini Amsterdam, Uholanzi wakati ndege hiyo ilipokuwa ikijiandaa kupaa kutoka Uholanzi kuelekea Uturuki.
Wakati ndege ikiwa iko kwenye hatua za mwisho za kupaa huku taratibu za usalama kwenye ndege zikitolewa, abiria wapatao 10 walikataa kukaa kwenye viti vyao na pia walikataa kufunga mikanda yao.
Tukio hilo lilimkasirisha rubani wa ndege hiyo raia wa Uholanzi ambaye aliamua kuirudisha ndege hiyo kwenye terminal na kuwashusha abiria wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo na kuanza safari ya kuelekea Uturuki ndege hiyo ikiwa tupu haina abiria hata mmoja.
Abiria walioachwa uwanja wa ndege walipandishwa ndege nyingine siku iliyofuatia na kuendelea na safari zao.
Shirika la ndege la Arkefly halijasema chochote juu ya rubani wao huyo ambaye amekuwa gumzo kutokana na hatua yake hiyo.
Source: nifahamishe.com