Mbonea
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 640
- 20
Utafanyaje kama ukiwa kwenye ndege halafu rubani anawatangazia ndege imepata hitilafu angani na kisha kuwataka muanze kusali.
Huku akiwa na wasiwasi wa kutua salama kwa dharura, rubani wa ndege aina ya Boeing ya shirika la ndege la Iran la Aseman Airlines aliwaambia abiria wake kuwa ndege hiyo imepata hitilafu na abiria waanze kusali sala za mwisho.
Ndege hiyo ilikuwa imepaa toka uwanja wa ndege wa Tehran na ililazimika kugeuza na kurudi uwanjani hapo baada ya dakika 45 angani.
Zengwe la ndege hiyo lilianza hata kabla ya ndege hiyo kupaa wakati safari ya ndege hiyo ilipochelewa kwa takribani masaa sita kutokana na hitilafu kwenye ndege hiyo.
"Rubani aliwatangazia abiria, ndege imepata hitilafu na inatubidi turudi Tehran, kwahiyo tafadhali anzeni kusali", alisema abiria mmoja wa ndege hiyo.
Iran imekuwa na rekodi mbaya ya ndege zake kuanguka ndani ya miongo michache iliyopita na ajali nyingi za ndege nchini humo huhusisha ndege zilizotengenezwa nchini Urusi.
Vikwazo vya kiuchumi walivyowekewa Iran na Marekani vimesababisha Iran ishindwe kununua spea za ndege zao za zamani aina ya Boeing na Airbus na kusababisha wategemee zaidi ndege zinazotengenezwa nchini Urusi.
Mwezi julai mwaka huu, ndege ya shirika la ndege la Iran la Caspian Airlines ilianguka na kuua watu wote 168 waliokuwemo kwenye ndege hiyo.