Rosti la nyama bila viungo vingi

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,706
Mahitaji

Nyama kilo moja

Tangawizi na thomu viwe vimesagwa kila kimoja ujazo wa nusu kijiko cha chai

Kitunguu maji kimoja kikubwa kikatwe katwe

Nyanya maji kubwa tano

Limao kiasi

Mchuzi mix masala kijiko kimoja cha chai

Pilipilimbichi ya kusaga kiasi

MAPISHI

Safisha nyama, kamulia limao, weka tangawizi kidogo changanya kisha chemsha hadi iive, bakisha supu kiasi

Weka sufuria jikoni, mimina mafuta kiasi, tia vitunguu maji koroga hadi viwe kama na rangi ya kijani mpauko

Mimina thomu na tangawizi koroga kidogo

Tia rojo la nyanya, tia chumvi koroga funika acha nyanya ziive

Funua kisha tia vipande vya nyama, koroga, tia supu kiasi koroga tia mchuzi mix koroga punguza moto acha mboga ichemke taratibu

Kula kwa wali au kwa ugali na glass ya mtindi laini kisha jenga mwili
FB_IMG_1668232850589.jpg
 
Safi sana umalize hiyo rost ukae nusu saa upige maji halafu utafute grants na ice na ndimu safi kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom