Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Kitila,
Ahsante kwa kutuwekea kumbukumbu tena. Hatimae, hata wasiopenda kuamini kuwa mfalme yuko uchi watauona ukweli ulivyo. Tunabaki kuzunguka zunguka tu mbuyu kama wendawazimu, sijui kwa nini!

Kalamu aliyejiuzuru alikuwa waziri Mkuu LOwassa. Ambaye kama sikosei ni wa tatu kutoka juu. na Makamu wetu ameisha tajwa kuwa kati ya watu watakaouona ufalme ni pamoja na yeye sasa amebakia nani huyo?

Tunaweza kumuomba ang'atuke maana maisha bora kwa mtanzania sasa yanakuwa ndotto kwa sababu yake.
 
Duh! Njemba haina chake bora haikuruhusiwa kusema chochote bungeni maana angebwabwaja tu!
 
Kwanini watu wanapenda kudivert attention ya watu,tunazungumzia Mwanahalisi versus RA watu wanaleta mambo ya kesi ya kubenea,kuna thread ya kesi ya tindikali ya kubenea huko fanya uchangie mawazo yako kule badala ya kutubadilisha mawazo na fikra zetu kwenye mapambano dhidi ya hawa madhalimu (mafisadi) wanaotaka wapate utajiri usiomithilika kwa kuwanyonya na kuwatesa wananchi wa kawaida.huwa nasikitika ninavyoona wapinzani wanashindwa kuzibeba hoja hizi na kuzipeleka kwa wananchi walio wengi walioko vijijini ambako ni aghalabu kuona au kusikia habari kutoka katika vyombo vyetu vya habari.sina political affiliation lakini napenda wananchi wafahamu ukweli na wachague mtu kutokana na misimamo yake na uzalendo wake kwa taifa hili na siyo kuchagua madhalimu kama RA,EL na wengineo ambao wanaishia kuwatisha watu wanaojaribu kuwapa habari za mabaya wayatendayo wananchi wa nchi hii. naamini katika vita hii siku moja tutashinda.
 
Mwanahalisi usiogope. Wengi tunakuunga mkono. Kama walitaka kukutoa roho pale walipokumwagia tindikali na bado hukuogopa kuendelea kuwaumbua, nini shs bilioni 3?. Kweli Mwanahalisi halina hizo bilioni 3 lakini sisi maskini wengi tunaotetewa na Mwanahalisi tutazichanga.
UJUMBE KWA ROSTAM: Fanya haraka uende mahakamani maana hata hilo ulilozuiwa kulisema bungeni, utaweza kulisema mahakamani!
 
(Samahani kama mtu ameiweka)....
ndo maana alikatazwa kusema maana ni mavi matupu tu, hana la maana alilotaka kuwasilisha



Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi hii ya kuzungumza mbele ya Bunge lako tukufu ili niweze kutoa maelezo na vielelezo kuthibitisha hoja nilizotoa katika mchango wangu wa maandishi nilioutoa katika kikao kilichopita cha Bunge wakati wa mjadala wa Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi “Richmond Development Company LLC” ya Houston, Texas Marekani mwaka 2006.

Mheshimiwa Spika, wakati akifungua mjadala wa hoja hiyo, Mwenyekiti wa Kamati Teule, Mheshimiwa Dr. Harrison Mwakyembe, siyo tu alinitaka nithibitishe hoja yangu kwamba Kamati Teule hiyo ilikuwa inaendelea kumalizia kazi zake hadi wiki ya kwanza ya kikao kilichopita cha Bunge lakini pia aligusia maeneo kadhaa ya ripoti ambayo yananihusu.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa uniruhusu nitoe maelezo ya kina pamoja na ushahidi wa vielelezo kuhusiana na masuala hayo yote aliyoyazungumzia Mheshimiwa Mwakyembe ili Bunge hili na Watanzania kwa ujumla waujue ukweli, tena ukweli kamili kuhusiana na suala hili.

Mheshimiwa Spika, nianze na hoja ya hati ya wito wa kunitaka nifike mbele ya Kamati Teule kutoa ushahidi.

Ni lazima nikiri nimesikitishwa sana ingawa sikushangazwa na maelezo marefu ya Mheshimimiwa Mwakyembe aliyoyatoa kueleza jinsi hati ya wito ilivyofikishwa nyumbani kwangu Oysterbay na kupokewa kwa dispatch na mtu aliyedaiwa kuwa ni ndugu yangu.

Sikuona umuhimu wala haja ya maelezo hayo kwa sababu katika mchango wangu wa maandishi nilioutoa katika mjadala ule, hakuna sehemu yoyote niliyosema kuwa hati ya kiapo haikufikishwa nyumbani kwangu tarehe waliyoitaja.

Kwa hivyo, ule utungo mrefu wa kufikia kulieleza Bunge lako kwamba Kamati Teule ina hata hati ya kiapo ya mtumishi wa Bunge aliyefikisha summons (wito) hiyo nyumbani kwangu ilikuwa na muendelezo tu wa kipaji cha usanii cha Mheshimiwa Mwakyembe.

Mheshimiwa Spika, nilichosema mimi, na ambacho Mheshimiwa Mwakyembe amekikariri vizuri katika maelezo yake, ni kuwa hati hiyo iliandikwa tarehe 24 Desemba, 2007 ikinitaka nifike mbele ya Kamati Teule tarehe 27 Desemba, 2007 na kwamba mazingira ya tarehe hizo ni magumu kwa barua kuwafikia walengwa kabla ya sikukuu kupita.

Mheshimiwa Spika, kupokelewa hati ya wito nyumbani kwangu ni suala moja na hati kunifikia mimi ni suala jengine.

Sidhani kama Mheshimiwa Mwakyembe anapofikishiwa barua nyumbani kwake wakati yeye akiwa nje ya nchi, basi wanafamilia yake husafiri kumfuata aliko ili kumfikishia barua hiyo kwa hivyo, wala haikuwa ajabu kama Kamati Teule ilivyotaka ionekane kwa mimi kupokea barua hiyo baada ya kurejea kutoka safari yangu nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza katika mchango wangu wa maandishi, mimi nilikuwa nje ya nchi kuanzia tarehe 17 Desemba, 2007 hadi 3 Januari, 2008. Nawasilisha kwako nakala ya photocopy ya Paspoti yangu ikiwa na mihuri ya Idara ya Uhamiaji inayoonyesha kutoka na kurejea kwangu hapa nchini kama kielelezo kinachothibitisha maelezo yangu hayo.

Mheshimiwa Spika, naendelea kusisitiza kuwa Kamati haikuwa na nia ya kweli na ya dhati ya kutaka maelezo yangu maana kama ingetaka kufanya hivyo, ingeniita katika siku yoyote kabla ya Desemba 24, 2007. Lakini kwa kusubiri siku 7 tu kabla ya kumalizika kwa muda ambao walipaswa wawe wamekamilisha kazi yao, tena ikiwa ni kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka ambapo familia nyingi zisizo na kazi za serikali huchukua likizo, kunaonyesha wazi kuwa kulikuwa na malengo ya kutaka kuchafuana tu kwa kujua kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kutopatikana yule anayehitajika kutoa ushahidi. Iwapo Mheshimiwa Mwakyembe hapendi kuona nina siku za mapumziko, ni bahati mbaya sana kuwa mimi sina cha kumsaidia katika hilo.

Mheshimiwa Spika, narudia kusema kwamba kama Kamati Teule ilikuwa na nia ya dhati ya kutaka maelezo yangu basi wangeweza kufanya hivyo hata baada ya mimi kurejea kwa sababu kama nitakavyothibitisha kwa ushahidi Kamati iliendelea na kazi hadi baada ya Desemba 31, 2007.

Mheshimiwa Spika, kabla ya kuliingilia hilo, napenda pia nieleze ukweli kuhusu hoja nyingine ambazo Mheshimiwa Mwakyembe alijaribu kuzipotosha akitumia usanii wake wa kuwasilisha na kujibu hoja. Nianze na ile inayohusu kuitafutia Richmond kampuni ya ushauri ya uandishi wa habari (G&S Media Consultancy) ili Richmond iandikwe vizuri na vyombo vya habari Tanzania.

Mheshimiwa Spika, hoja hii inaonekana imeibuliwa kutokana na ushahidi wa Ndugu Salva Rweyemamu alioutoa mbele ya Kamati Teule. Nimepata nafasi ya kupitia Hansard za Bunge zinazohusu shughuli za Kamati Teule na nilichokiona ni kuwa Ndugu Salva Rweyemamu mwenyewe hakuwa na uhakika wa kile alichokisema pale alipoulizwa juu ya nani aliyemtambulisha kwa kampuni ya Richmond na yeye akajibu, “Nadhani ni rafiki yangu Rostam Aziz”.

Mheshimiwa Spika, ni juu ya Ndugu Salva mwenyewe kuweka sawa kumbukumbu zake na kujua kwa uhakika ni nani aliyemtambulisha na Richmond badala ya kusema “anadhani”. Inawezekana kama binadamu alichanganya mambo kwani mimi sikuwahi kumtambulisha kwa Richmond, maana mimi mwenyewe siwajui hao akina Richmond hata niweze kuwatambulisha kwa mtu mwingine. Mimi nilimtambulisha Ndugu Salva kwa kampuni ya FFT inayoshughulika na utoaji wa mizigo bandarini (clearing and forwarding) ambayo ndiyo ninayoitumia katika shughuli za kibiashara za kampuni zangu ili kuweza kujitangaza yaani kufanya promotion. Kuthibitisha hilo, nawasilisha mbele ya Bunge lako hati ya kiapo, affidavit ya Ndugu Hassan Dhala, mmiliki wa kampuni ya FFT, ambayo imesainiwa na kamishna wa viapo inayobainisha ukweli huu.

Mheshimiwa Spika, hoja ya pili ambayo mheshimiwa Mwakyembe katika maelezo yake alisema Kamati Teule ilitaka nieleze ni ile inayohusu uhusiano kati ya kampuni yangu ya Caspian na kampuni ya Dowans. Kamati Teule imehoji kwanini barua pepe na anuani ya posta ya kampuni yangu ya Caspian pia ilitumiwa na Dowans na kwamba baadhi ya wafanyakazi wa Caspian wanadaiwa, naomba nirejee wanadaiwa, kuifanyia kazi pia Dowans.

Mheshimiwa Spika, kabla ya kuzijibu hoja hizo, napenda nimfahamishe mheshimiwa Mwakyembe kuwa mimi, tofauti na labda alivyo yeye, sina wapambe eti wa kunisimulia yaliyoandikwa katika Ripoti ya Kamati Teule aliyoiongoza. Nataka nimhakikishie kuwa nimesoma ukarusa hadi ukurasa wa ripoti waliyoiandaa pamoja na kwamba haikuwa kazi nyepesi ukitilia maanani kwamba ripoti hiyo imepotosha na kupindisha mno hoja zinazohusu masuala ya fedha, uchumi na biashara.

Mheshimiwa Spika, hakuna hata mfanyakazi mmoja wa Caspian anayeifanyia kazi Dowans. Isipokuwa narejea tena maelezo niliyoyatoa katika mchango wangu kwamba watumishi wa kampuni yangu wanaweza kushirikiana na kampuni yoyoye ambayo kampuni yetu ina nia ya kufanya nayo biashara. Na hilo lilifanyika kama ambavyo pia ni kweli kuwa kampuni ya Caspian ambayo mimi ni Mwenyekiti wake iliruhusu Dowans kutumia anuani ya posta na barua pepe yake kwa sababu tulikuwa tunatarajia kupata kazi ya ukandarasi wa ujenzi kutoka kwao, ambayo ndiyo biashara kuu ya kampuni ya Caspian.

Mheshimiwa Spika, hiki si kioja kama ambavyo Mheshimiwa Mwakyembe na Kamati Teule alitaka ionekane. Ni taratibu za kawaida kabisa katika shughuli za biashara kuwa na kitu kinachoitwa “hospitality arrangement” yaani kupeana fursa za kutumia baadhi ya huduma baina ya kampuni zinazokusudia kufanya biashara au kupeana kazi. Hili linaweza likaonekana ni jambo kubwa la kuzua maswali kwa watu wasio na uelewa wa uendeshaji biashara lakini ni jambo la kawaida kabisa katika ulimwengu wa ushindani wa kibiashara ambapo kila kampuni inatafuta kandarasi kutoka kwa mwenzake.

Mheshimiwa Spika, kama ilivyoeleza kampuni yangu ya Caspian ni kampuni ya kandarasi ambayo huwa inatafuta kazi kwa kampuni nyingine zenye shughuli hizo. Caspian iliwasilisha zabuni ya kufanya kazi ya kandarasi ya ujenzi kwa ajili ya uwekaji wa mtambo wa General Electric 40MW LM6000 Gas Lurbine kwa Dowans ambayo hatukufanikiwa kuipata. Hata hivyo, tuliomba kazi nyingine ndogo ya kandarasi ya ujenzi wa ukuta wa uzio ambayo tulifanikiwa kuipata.

Nawasilisha mbele ya Bunge lako nakala za barua mbili kutoka Dowans kwenda kwa Caspian kuthibitisha haya, moja ya tarehe 10 Machi, 2007 ikitueleza kutofanikiwa kupata kazi tuliyoomba awali, na ya pili ya tarehe 25 Oktoba, 2007 ikitufahamisha kuwa zabuni yetu imefaulu.

Mheshimiwa Spika, aina ya kazi za ujenzi ambazo kutoka kwa Dowans tuna ujuzi nazo na tumejijengea jina zuri kwa jinsi tunavyozifanya. Tumewahi kufanya kazi kama hizo kwa ufanisi wa hali ya juu kwa kampuni ya WARTSILA ya Finland baada ya kushinda zabuni ya kimataifa. Nawasilisha kwako Mheshimiwa Spika, nakala za barua mbili (ya kwanza ya tarehe 31 Machi, 2008) kutoka kwa WARTSILA kwenda kwa Caspian kuthibitisha ukweli huu.

Mheshimiwa Spika, kwa taarifa ya Bunge lako tukufu, WARTSILA ni kampuni iliyosifiwa na Kamati Teule kwamba mradi wake ni wa kuigwa katika uzalishaji wa umeme hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, hayo ndiyo mahusiano ya kikazi kati ya Dowans na Caspian ambayo ni ya kawaida kabisa, yaliyofuata taratibu zote na yaliyofanyika kwa uwazi. Ni mahusiano ambayo kama Kamati Teule ingetaka kuyajua ingeweza kufanya hivyo. Hata hivyo, Kamati Teule iliamua kukwepa wajibu wa kuujua ukweli huu na badala yake ikaamua kuibua maswali yaliyoandaliwa kwa usanii mkubwa ili yatimize lengo lililokusudiwa la kutuchafulia majina baadhi yetu na pengine hata kuhujumu sifa njema za biashara tunazofanya.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuweka kumbukumbu sawa kuhusiana na hoja hizo zilizoibuliwa na Mheshimiwa Mwakyembe, sasa nijielekeze katika hoja ya msingi ambayo ndiyo hasa niliyotakiwa niithibitishe. Hii ni ile inayohusu hoja yangu kwamba Kamati Teule iliyochunguza mkataba wa Richmond iliendelea na kazi zake hata baada ya muda wa siku 45, yaani baada ya tarehe 31 Desemba, 2007, na mpaka wiki moja kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge na hivyo kama ilikuwa na nia thabiti ya kuupata ukweli kutoka kwangu ingeweza kufanya hivyo.

Mheshimiwa Spika, nimesikitishwa ingawa sikushangazwa na kitendo cha Mhe. Mwakyembe kujikakamua katika ukumbi mtukufu wa Bunge lako kwamba eti madai hayo ni uongo.

Mheshimiwa Spika, nina ushahidi wa hoja hiyo kwamba kamati iliendelea na kazi zake hadi baada ya muda iliyopangiwa kumalizika. Ushahidi huo nauwakilisha hapa mbele ya Bunge lako ili lione ni nani kati yangu na Mhe. Mwakyembe anayesema kweli.

Mheshimiwa Spika, sisi wengine hatuna kawaida ya kuja na mbwembwe nyingi za kujisifu hata kama ni kwa gharama ya kulipotosha Taifa na kuwapotosha wananchi. Tuna asili na rekodi ya kusema kweli, tena kweli tupu. Tunaamini katika kutenda na kutendewa uadilifu. Kwa hivyo, kila tunachokisema na kukitenda kina misingi yake. Leo hii, nimeona niwasaidie watanzania kupitia Bunge lako tukufu kuujua ukweli kamili ambao umejaribiwa kufichwa sana kwa malengo wanayoyajua wajumbe wa Kamati Teule.
 
....... Lakini kwa kusubiri siku 7 tu kabla ya kumalizika kwa muda ambao walipaswa wawe wamekamilisha kazi yao, tena ikiwa ni kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka ambapo familia nyingi zisizo na kazi za serikali huchukua likizo, kunaonyesha wazi kuwa kulikuwa na malengo ya kutaka kuchafuana tu kwa kujua kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kutopatikana yule anayehitajika kutoa ushahidi. ......

Hivi huyu mbumbumbu anafikiri kuwa ubunge ni GENGE lake binafsi?? Hajui kuwa nayo ni kazi ya serikali?? Tena ni kati ya MIHIMILI ya nchi?? Kazi kweli kweli!!!!
 
Mheshimiwa Spika, nimesikitishwa ingawa sikushangazwa na kitendo cha Mhe. Mwakyembe kujikakamua katika ukumbi mtukufu wa Bunge lako kwamba eti madai hayo ni uongo.

Mheshimiwa Spika, nina ushahidi wa hoja hiyo kwamba kamati iliendelea na kazi zake hadi baada ya muda iliyopangiwa kumalizika. Ushahidi huo nauwakilisha hapa mbele ya Bunge lako ili lione ni nani kati yangu na Mhe. Mwakyembe anayesema kweli


Jamani! Mbona inaonekan wazi taarifa hii imekatwa? Fuatilieni acheni kukurupuka kwa kualaumu tu. Ukweli ni kwamba chini ndio kulikuwa na mamba ya jinsi ripoti ilivyobadilishwa. Na ukweli huo ndio uliomwogofya Sita!!!!!!!
 
Mheshimiwa Spika, nimesikitishwa ingawa sikushangazwa na kitendo cha Mhe. Mwakyembe kujikakamua katika ukumbi mtukufu wa Bunge lako kwamba eti madai hayo ni uongo.

Mheshimiwa Spika, nina ushahidi wa hoja hiyo kwamba kamati iliendelea na kazi zake hadi baada ya muda iliyopangiwa kumalizika. Ushahidi huo nauwakilisha hapa mbele ya Bunge lako ili lione ni nani kati yangu na Mhe. Mwakyembe anayesema kweli


Jamani! Mbona inaonekan wazi taarifa hii imekatwa? Fuatilieni acheni kukurupuka kwa kualaumu tu. Ukweli ni kwamba chini ndio kulikuwa na mamba ya jinsi ripoti ilivyobadilishwa. Na ukweli huo ndio uliomwogofya Sita!!!!!!!

Ni kweli kabisa angalieni vizuri, hii taharifa imekatwa kuna vitu muhimu havijawekwa, perhaps tunaweza kujisifia hapa kumbe mafisadi wanatuchezea. Lets check well

Mimi nafikiri that man has something to offer to us, naomba apewe nafasi aseme kile ambacho report ya Mwakyembe imekificha kwani ile report aisemi RDC ni ya nani wakati mojawapo ya hadidu za rejea za kamati ilikuwa ni hiyo, hivi nani anaweza kusema tunavyoelewa mpaka sasa RDC ni ya nani.

Je Dr. Ringo Tenga anasema alimwakilisha nani wakati anasaini mkataba, nani aliipa kampuni yake kazi ya kuiwakilisha RDC hapa Tanzania, perhaps tumuulize huyo atuambie tunaweza kupata fununu, maana mpaka sasa RDC haina mwenyewe.

Ni kweli ile kamati imemsaidia JK kuondoa vingozi hasiowahitaji serikalini, na hii inadhibitishwa na hatua ambazo serikali inachukua kwa kuwaacha watu ambao wanalipwa mamilioni kila siku kuendelea kulipwa wakati mkataba haukuwepo, kwani upande wa pili haukuwepo kisheria.

Mafisadi wataumbuka wengi maana ninachokiona sasa kuna wanasheria wengi ambao wataingia kwenye huu mkumbo bila kujua maana walikuwa wanasaini documents bila kujua kinachoendelea, professionally ni kosa kubwa sana.

Mtu kama Dr. Tenga nafikiri anaweza kusaidia kujua mmiliki wa RDC ni nani hata kama aliyefanya negotiations alikuwa partner wake lakini si kuna mkataba wao na RDC utaonyesha RDC ni ya nani.

Kinachotakiwa ni utashi wa viongozi wetu kulifuatilia suala hili kwa undani zaidi kwani mwanga upo. Je RDC ni ya JK au EL jibu tutalipa mahakamani maana huko kila mtu yuko huru kusema bila kufungwa na ibara ya 15:1
 
Kuna some few interesting things emerging from the content of Rostam's speech. Ni vigumu kuona haya ukiwa biased kwa kumwangilia Rostam badala ya kile alichowasilisha. Kwa mfano:

i) Rostam, pamoja na mambo mengine, anadai kwamba ripoti ya Mwakyembe "imepotosha na kupindisha mno hoja zinazohusu masuala ya fedha, uchumi na biashara". Sasa binafsi naona this is a very serious assertion na ninashangaa inawezekanaje spika hakutaka ufafanuzi kwa jinsi ambavyo kamati ilipotosha. Nafikiri kwamba Rostam alitakiwa atoe maelezo zaidi kuthibitisha jinsi ambavyo kamati ilipotosha mambo ya accounts.

ii) Even more glaring: je, ni kweli kwamba Kamati ya Mwakyembe iliendelea na muda baada ya deadline bila kibali cha spika? Na kama ni kweli iliendelea na muda, kwa au bila kibali cha spika, kwa nini Mwakyembe alikanusha bungeni? Kuna ubaya gani kujua ukweli kuhusu nani mwongo kati ya Mwakyembe na Rostam katika hili?

Bila kuyapatia majibu maswali kama haya, hili la Rostam litaendelea kubaki kuwa ni doa sio tu katika ripoti ya kamati hii bali pia katika utendaji wa bunge.

Kuna kitu cha kuchota kutoka kwenye haya maelezo kama mtu utaamua ku-focus kwenye content ya kile alichokisema kuliko personality ya aliyeyasema!
KITILA KWA MACHO YAKO MWENYEWE PITIA WALICHOANDIKA WENZAKO KTK THREAD HII,JAMAA WAKO SUBJECTIVE NA WANAHITAJI MAREKEBISHO MAKUBWA KAMA HUKU NDIKO KUJENGA HOJA YA KUMPINNGA RA,WALAU WEWE NDIO UMETOA MWANGA.....ISSUE MPAKA RAA ANAKWENDA BUNGENI KUJIBU HOJA NA AZIMIO LA BUNGE KUWA RA ATHIBITISHE KUWA KAMATI YA MWAKI ILIPITILIZA.MAMBO MENGINE YOTE NI MBWEMBWE ZAKE MWENYEWE,TENA MWAKI MWAENYEWE NDIE ALIEPINGA KWA NGUVU ZOTE KUWA WALIPITISHA SIKU...RA AMETOA UTHIBITISHO KTK KIAMBATISHO AMBACHO HATUJAKIONA HAPA..KIAMBATISHO CHA UTHIBITISHO WA HOJA YAKE ALIOTAKIWA NA BUNGE KUJIBI.NA SIYO KUTHIBITISHA JAMBO JINGINE LOLOTE.KWA KUWA MAKALA HIO HAINA SOURCE,TUNAJUAJE KAMA HAIJAKUWA EDITED HASA UKIZINGATIA KUWA IMELEAK KIPITIA S6.MAANA RA NA MWANAHALISI HAWANA UHUSIANO TOKA PROPOSAL KUOMBA FEDHA YA YA KUBENEA YA KUANZISHA GAZETI LA MWANAHALISI ILIPOPIGWA CHINI NA RA.
 
Haya sasa RAIA MWEMA WAMERUDI TENA KWA ROSTAM, mambo mdundo

Mh. Rostam, mtu mzima hatishiwi nyau'

Lula wa Ndali-Mwananzela
Mei 7, 2008



KUNA watu wanaitwa mashujaa na majasiri; kuna watu wanaojidhania kuwa ni mashujaa na majasiri; na kuna watu ambao ni mashujaa na majasiri.

Wale wa kundi la kwanza huitwa hivyo na watu wengine kwa sababu mbalimbali za ukweli na za uongo, zenye msingi na zile za kutunga. Wale walio kundi la pili ni wale ambao wanajivisha ushujaa na ujasiri na kujitungia sifa za ukuu huo ili kuwavutia watu au kutisha watu.

Wale wa kundi la tatu ushujaa na ujasiri unathibitishwa na vitendo vyao ambavyo havihitaji kupigiwa panda na mtu yoyote kwani ni dhahiri kuviona.

Mwandishi wa makala ya "Tusimbeze Rostam, hatikisi kiberiti" kwenye toleo lililopita la gazeti hili amejaribu kutupatia Watanzania shujaa wa kundi la kwanza. Joseph Wambura akijibu makala yangu ya wiki mbili zilizopita iliyokuwa na kichwa cha habari "Sipendi Rostam Aziz atikise kiberiti bungeni" amejaribu kwa jitihada kubwa kuonyesha kuwa nilichokisema kwenye makala yangu ya awali hakina msingi, ni cha kutunga na hakina msingi katika ukweli.



ROSTAM Aziz

Jaribio hilo la kujibu hoja zangu japo dhaifu, halina budi kupongezwa kwani bila ya shaka baada ya kuacha magazeti yote aliyokuwa anayasoma na kuvutiwa na makala yangu kiasi cha kuamua kuijibu kunaonyesha ni jinsi gani makala hiyo ilimgusa Wambura (kwa uzuri na kwa ubaya).

Hivyo najihisi ni heshima ya pekee kwangu kuchaguliwa kati ya makala nyingi zilizoandikwa habari za Rostam wiki ile kujibiwa kwa kina na kiufundi namna ile. Pia nimefurahishwa sana na jitihada zake za kujenga hoja zenye nguvu badala ya kulazimisha hoja kwa kutumia nguvu kama alivyosema yeye mwenyewe "Sina sababu ya kutumia nguvu kuonyesha ukweli umelala wapi katika kueleza Rostam alipata kuchangia nini akiwa bungeni."

Na mimi, basi, kwa heshima kubwa na taadhima naomba nisitumie nguvu niweze kujibu hoja zake kama vile nimefumbwa macho na mkono mmoja ukiwa umefungwa nyuma yangu niweze kuonyesha ni jinsi gani hoja za Wambura hazina mantiki, ni dhaifu, na ukiziangalia kwa ukaribu hazina msingi kwani ni jaribio dhaifu la kumjenga Rostam kama shujaa na mbunge jasiri ambaye anaweza kutikisa nchi.

Kwanza kabisa niseme kile nilichosema kwenye makala yangu ya awali; sipendi tena sitaki (nimeongeza hilo) Rostam atikise kiberiti bungeni. Nasema hivyo kwa sababu naamini kama nilivyoandika kwenye makala hiyo kuwa "Hofu ambayo Spika ameijenga kuwa Rostam akisema basi kutazuka "vurugu bungeni" au kwa namna fulani kutafanya taifa liyumbe ni hofu isiyo na msingi na ni hofu ambayo inaongeza nguvu za kimungu za Rostam. Rostam ni mwanadamu mwenzetu na hana nguvu zozote zile ambazo zinaweza kusababisha mvua inyeshe au jua lichomoze!"

Kitu pekee ambacho Wambura amejaribu kujibu ni swali langu ambalo niliuliza "Hivi ni lini mara ya mwisho kwa Rostam kutoa mchango bungeni na alichangia nini? Ni kitu gani ambacho watu wanakumbuka ambacho Rostam Aziz alisema bungeni katika mijadala ya bajeti au mingineyo ambayo inaweza kukumbukwa? Kama huko kote hajasema jambo lolote la kukumbukwa iweje leo tugwaye kama Taifa ati Rostam anataka kusema?"

Katika kujibu hoja zangu Wambura anatoa mifano ya kuonyesha jinsi gani Rostam ni shujaa na jasiri akiwa bungeni. Anasema kuhusu hilo kuwa "matukio haya aliyotenda kwa ufasaha wa hali ya juu na kutikisa nchi akiwa bungeni." Hebu tuangalie mifano hiyo na tuone kama kweli ni ya "ufasaha wa hali ya juu" na ya kuwa Rostam aliweza "kuitikisa nchi akiwa bungeni".

Mfano wa kwanza ni ule anaosema "Mwaka 1994 Taifa lilikumbwa na mfumuko wa bidhaa kutoka Zanzibar. Bidhaa hizo zilikuwa zikipita kwa njia ya panya, maarufu kama ‘Zanzibar Route.' Zilikuwa zikiingia nchini bila kulipa kodi na kufurika madukani. Rostam alisimama bungeni, akajenga hoja na Serikali ikachukua hatua za haraka kudhibiti hali hiyo…Hapo alionyesha ujasiri wa kwanza akiwa mbunge kijana kuliko wote wakati huo."

Ningefurahi kama Wambura angetuwekea alichosema Rostam bungeni na ambacho hakikusemwa na mbunge mwingine yoyote kabla yake kuhusu suala hilo. Wambura anasema Rostam alijenga hoja lakini hatuambii hiyo hoja ilisemaje na Rostam alisema nini. Angeweza kutuambia ni kwenye hansadi gani ili na sisi wengine tuende kuangalia.

Katika hoja yangu ya awali niliuliza ni kitu gani ambacho Rostam alisema bungeni ambacho kinaweza "kukumbukwa"? Hivi msomaji unakumbuka alichosema Rostam kuhusu "njia za panya"? Mimi ni mfuatiliaji wa masuala ya kisiasa na kumbukumbu yangu ni nzuri. Alichokisema Rostam hakikumbukwi na kwa hakika hakikuitikisa nchi.

Mfano wa pili ni ule anaosema "Mwaka 1997 kwani ndio wakati sheria ya madini ya 1998 ilikuwa imeanza kujadiliwa) Rostam alikuwa mbunge pekee aliyekataa kuunga mkono muswada wa Sheria ya Madini. Alisema muswada huo ulikuwa na upungufu mkubwa wa msingi na akaonya kuwa iwapo ungepitishwa, vizazi vijavyo vingewahukumu wabunge kwa uamuzi huo. Leo, kamati ya Madini ya Rais, chini ya Jaji Mark Bomani, imeipitia sheria hii. Si ajabu matokeo yatakuwa sawa na alivyokuwa amependekeza Rostam."

Ingawa hili linawezekana kuwa ni kweli, lakini Rostam hakumbukwi kwa alichosema (ndiyo hoja yangu). Hivi ubaya na mapungufu ya sheria ya madini tulisikia toka kwa Rostam au kwa Zitto Kabwe? Kwa nini, wakati ule hatukumuona Rostam mtu jasiri akisimama na kutetea msimamo wake hata kutengwa na chama chake au kupewa adhabu na Bunge? Hata kama alipinga muswada huo, je, ulipoletwa wakati wa kupiga kura ya Bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba au ule wa madini, Rostam alipinga na kuondoa Shilingi au aliunga mkono hoja?

Kwa hakika, huko kupinga kwake sheria ya madini si kitendo cha kishujaa kwani ni wajibu wake na kwa hakika sidhani kama kuna Mtanzania anakumbuka, na zaidi ya yote haikutikisa nchi kama kina Zitto walivyotikisa nchi mwaka jana!

Mfano wa tatu Wambura anasema "Mwaka 1999 Rostam huyu huyu ambaye mwandishi hakumbuki iwapo aliwahi kusema lolote bungeni, aliweka historia katika chama tawala. Akiwa mbunge wa chama tawala, aliongoza kundi la wabunge 50 kupinga iliyoitwa kesi ya uhaini dhidi ya wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF).

Kumbuka CUF ni chama cha upinzani. Kesi hii ilikuwa imepandikizwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, akidai wabunge hao walikuwa na njama za kumpindua. Baada ya hoja ya Rostam, muda mfupi baadaye watuhumiwa wote waliachiwa."

Hapa nianzie na hili la mwisho. Wambura anadai kuwa kesi ya Uhaini ilikuwa "imepandikizwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya nne wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour".

Wambura anataka kuacha taswira kwa msomaji kuwa bila Rostam kuongoza kundi la wabunge 50 wa Bara, basi, kesi ya uhaini ingeendelea kuwapo na wale wabunge wa CUF wangeendelea kusota. Huku ni kujipa ujiko usio na msingi. Kuachiliwa kwa wabunge wale hakukutokana na juhudi za Rostam pekee na wala hastahili hata kidogo kubeba sifa za juhudi za mamia ya watu, vikundi na asasi mbalimbali.

Kushikiliwa kwa wabunge wale wa CUF lilikuwa ni doa kubwa kwa Tanzania na Zanzibar, na hasa watu wengi walipinga kushikiliwa kwao. Sekretariati ya Jumuiya ya Madola na viongozi wastaafu na wenye kuheshimika Afrika walishikiri katika kuishawishi Serikali ya Zanzibar kuwaachilia wabunge hao.

Kwa kumkumbusha tu Wambura ni kuwa Januari 2000 Rais Benjamin Mkapa alifanya mazungumzo na Rais Salmin kuhusu sakata la wabunge hao wa CUF. Na hilo lilitokana na shinikizo toka ndani na kutoka nje hasa baada ya kesi ya uhaini kuanza.

Ni siku hiyo hiyo ndiyo wabunge hao walipoandika barua yao ambao hawakuungwa mkono na Waziri Mkuu wa wakati huo, Fredrick Sumaye ambaye aliwaambia kuwa hawakuwa na baraka ya Chama.

Walichofanya wabunge hao ni kudandia treni ambalo wengine walishalianzisha akiwamo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ali Mohammed Ali Omar ambaye alisema kuwa kesi hiyo ilikuwa ya "kisiasa" kitu ambacho kiliashiria kuwa haishindiki mahakamani. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wenyewe kabla ya G50 walisema hilo hilo na asasi nyingine zisizo za kiserikali.

Hivyo kumpa ujiko Rostam kwa kazi ya watu wengi zaidi ya kundi hilo la G50 na kumfanya kuwa ndiye shujaa aliyesababisha wabunge wale kuachiliwa si haki na si kweli. Na zaidi ya yote kutoa madai bila ushahidi kuwa "Baada ya hoja ya Rostam, muda mfupi baadaye watuhumiwa wote waliachiwa" ni kutulaghai kwa kutudhania kuwa hatujui historia ya miaka michache tu iliyopita.

Watanzania wangapi wanakumbuka jina la Rostam juu ya hoja hii? Je, Rostam aliitikisa nchi kwa hilo? Msomaji hukumu mwenyewe.

Lakini kwa ujanja wa kujaribu kuchomea hoja Wambura ameongeza: "Mwaka huo huo, kwa ujasiri mkubwa, Rostam aliongoza mapambano dhidi ya Dk. Salmin aliyetaka kubadili Katiba ya Zanzibar na kuongeza muda wake wa kuwa madarakani."

Yaani, aliyesimama kati ya Dk. Salmin na kubadilisha Katiba ni Rostam! Sasa hapa naamini Wambura alikuwa anafanya mzaha. Yaani Rostam ndiye aliyeongoza mapambano dhidi ya Dk. Salmin? Hili nitawaachia wachambuzi wengine kwani itabidi michango ya Mwalimu Julius Nyerere, na Watanzania wengine itupwe katika kiza cha historia na tuanze kuimba nyimbo za kumtukuza Rostam kwa kuiokoa Zanzibar kutoka utawala wa Komandoo! Nani anakumbuka jinsi Rostam aliongoza "mapambano" dhidi ya Dk. Salmin? Je aliweza kuitikisa nchi?

Mfano wake mwingine anasema kuwa "Yapo mengi, ila nikumbushe hata hili. Rostam huyo huyo anayebezwa, mwaka 2001, alisimama kidete kupinga mabadiliko ya Katiba yaliyokuwa yakimpa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mamlaka makubwa zaidi, ikiwa ni pamoja na kuteua wabunge 10."

Kwa mara nyingine Wambura ameshindwa kutuonyesha alichosema Rostam na ambacho hakikusemwa na watu wengine. Kimsingi Wambura ametoa maelezo ambayo hayana msingi katika ukweli na yanaendeleza jaribio lake la kumpamba shujaa wake ambaye anaamini kuwa anaweza kuitikisa nchi.

Hakuna mahali ambapo amenukuu alichosema Rostam na hakuna mahali ambapo ameonyesha ni wapi na sisi wengine tunaweza kuangalia.

Lakini bado nasimamia maneno yangu ya awali. Rostam hana cha kuitisha nchi hii; na yeye kama raia mwingine yeyote yule hana nguvu yoyote ya kuifanya Tanzania itetemeke mbele yake ati kwa sababu anataka kusema kitu fulani. Aendelee kuwatetemesha anaowatetemesha na wale wenye kugwaya mbele zake wagwaye. Wale ambao wanaamini kuwa yeye ndiyo shujaa wake basi na wambebe juu juu ili nasisi tujue wamempata shujaa wao.

Vinginevyo, Rostam anayo haki ya kusikilizwa na chochote anachotaka kusema anaweza kusema bila kupigwa mkwara na mtu yeyote. Si Spika, si CCM na wala si waandishi wa habari.

Kama madai ya Wambura kuwa "Rostam alikuwa akidai kutotendewa haki na kwamba kamati ilifanya kazi nje ya muda wake, hivyo aliamini kuwa ilifanya kazi kisiasa. Kama kweli wangekuwa na nia ya kumhoji wangeweza kumhoji, ila kumhoji kwao kungeweza kuvuruga mchezo wa kisiasa ulionuiwa" yana ukweli basi Rostam aandike makala au amtumie mwandishi kuandika makala na aweke hoja zake hadharani badala ya kulalamikia pembeni.

Hofu ya kuwa ati akisema nchi itatikisika ni hofu ya nchi ya wenye hofu. Kama mada yangu inavyosema leo kuwa mtu mzima hatishiwi nyau na ncha ya mkuki haipigwi konzi. Lolote alilonalo Rostam litamtikisa yeye na chama chake na watu wake wa karibu. Linaweza kumtikisa Spika, Rais, wabunge, mawaziri na waandishi wa habari! Lakini kwa hakika haliwezi kuitikisa Tanzania!

Majuzi Waziri Mkuu wa nchi hii alijiuzulu na kesho yake watu waliamka na kwenda zao sokoni! Waziri wa Miundombinu ameanguka kama lumbesa na saa chache waliokuwa na harusi zao waliendelea. Sasa huyu Rostam hiyo nguvu ya kuweza kuitikisa nchi ataitoa wapi.

Tunaweza kushtushwa, tunaweza kupigwa na mshangao, na tunaweza kusikitishwa lakini nawahakikishia Watanzania wamekomaa kiasi cha kuweza kuhimili jambo lolote kama Taifa. Anayedhania kuwa Rostam anaweza kuitikisa nchi basi huyo aende kupiga magoti na kumbembeleza asiseme.

Kwa upande wangu narudia nililosema kama analo lake la kusema na anafikiri ameonewa asimame ajitetee; wenye kutikisika watatikisika na Tanzania haitotishika. Wale walio mabua ya mitete ambao wanatetemeka akikohoa na kukosa pumzi akipita waende kupanga foleni na kumlilia asiseme.

Mimi nasema Rostam anatikisia kiberiti ambacho akikiwasha vitakavyoungua ni yeye na nguo zake na za marafiki zake. Sisi wengine tutakaa pembeni kuwachora wanavyoumana na kutafunana kama mchwa. Kama haamini na asubiri.

Mashujaa wetu bungeni wapo na tunawajua, Rostam si mmoja wao.

Niandikie: lulawanzela@yahoo.co.uk

http://www.raiamwema.co.tz/08/05/07/lula.php
 
Nadhani huyo jamaa aliyejaribu kumpamba Rostam huko aliko hana raha tena...

Huyo, kama si Rostam, basi alifanya "dectation" jamaa akaandika na kujipa pen name.... Sasa hapo si jamaa ni Rostam...!!!! Aluta Continua
 
Mashujaa wetu bungeni wapo na tunawajua, Rostam si mmoja wao.
Mwandishi wa habri hii ndio wale ambao tulikuwa tunawatka siku zote ,na hawa ndio wale wanoitukuza kanuni ya tano ya TANU. "Nitasema Ukweli Daima, Uongo kwangu Mwiko"

Yes I sadi first and am saying again Rostam siyo mmoja wao ,siyo mmoja wa mashujaa wetu Bungeni!
 
Back
Top Bottom