Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

kama haya ni ya kweli basi chadema ni chama dhaifu mno.rufaa moja toka mwaka 2005 mpaka leo bado haijapatiwa ufumbuzi...mkipewa nchi iliojaa rufaa za mahakamani,mabaraza ya ardhi,polisi,wajumbe wa nyumba kumikumi mtaziweza kweli..Maji Moto pia ni mtu wa kumpima kama ana akili sawasawa kwa kuwa huwezi kumfukuza katibu wako wa wilaya,bali unapeleka malalamiko ndazi ya juu yake na pia huwezi kusema kuwa ata mkoani wanamlinda,hapo tayari ni mpasukomkubwa ktk chama...ili chadema kweli iwe ni chama imara ni lazima ikubali ukweli kuwa kuna migogolo mikubwa ndani yake na hakina njia bado ya kuitatua.migogolo hio itakuwa mikubwa zaidi kama mtaweza kupewa uongoza nchi.imagine hapo ni chama kidogo tu na kina mtandao mdogo tu unaoishia katika wilaya kwa sehemu kubwa.
 
Kufikiri kwamba wasomaji wa gazeti ni "timu" ya gazeti hilo si sahihi, unaweza kuwa supporter na mwanaharakati wa gazeti fulani lakini ultimately kama kuna litigation atakayekuwa responsible ni mhariri labda na wandishi wake.

Unachoweza kufanya ni kuwaelewa, ku protest kwa njia nyingi ikiwa pamoja na barua za wasomaji au barua personal kwa mhariri/muandishi au kuonyesha kutoridhika publicly kama unavyofanya hapa.Kama yote unaona hayafai unaweza kuacha kununua hilo gazeti au hata kuanzisha lako.

Walioandika habari hiyo ni waandishi/ timu ya gazeti na wenye wajibu wa kuomba au kutoomba radhi ni wao wenyewe, sisi wengine ni waangaliaji na kama tutawajudge itakuwa ni kwa wallets zetu.

Tatizo la sheria, kwa mtu anayeelewa sio kweli kwamba mara zote inasimamia ukweli.Unaweza kusema ukweli kwamba fulani ni mwizi lakini kama huna ushahidi wa kuthibitisha hivyo anaweza kukupiga libel charges ikabidi uombe msamaha.Wenye kuelewa wataelewa nini kinachoendelea.

Tanzania ingawa tunahitaji "exposee journalisms" pia tunahitaji a balanced approach na responsible journalism ili tusiwape hawa mafisadi ushindi unaotokana na legal technicalities.Kitu kikiandikwa watu wawe tayari kwenda mahakamani kukitetea, ama sivyo hata kama tuna habari za nguvu hapa, na tunajua ni za kweli, lakini kama tunakosa ushahidi unaoweza kusimama mahakamani hatuchapishi ng'o!

...you couldnt have said it better. Haya hasa ndio maelezo ya nini kilichowafanya RAIA MWEMA kumuomba jamaa msamaha. the point is, iwavyo vyovyote message ilifika!
 
Habari ikishakuwa na "inasemekana" tu inakuwa yale yale....

Kama una ushahidi unaweka "ThisDay can reveal"

Halafu wabishe unawatolea document mahakamani, habari za kusemekana hata huko Scotland inasemekana kuna "Loch Ness Monster" inasemekana pia kuna parallel universes with different laws of physics and particles such as tachyons with the speed of light as lowest speed barrier.

Key world ni "inasemekana"

...Naam, kama lilivyo na tatizo pia neno la "nasikia eti' huko kwenye vijiwe vyetu.....!
 
Na hii pia iangaliwe katika mjadala huu

Baada ya kumshtaki kubenea.. Wahariri sasa kumvaa Rostam

29.04.2008 0532 EAT

Na Said Mwishehe

WAKATI Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz amefungua kesi Mahakama Kuu ya akidai fidia ya sh.bilioni 3 kutoka gazeti la Mwanahalisi akidai limempaka matope kuhusiana na kashfa ya Richmond, sasa Jukwaa la wahariri linaangalia namna ya kumsaidia apambane katika kesi hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Sakina Datuu, alisema taarifa za kushitakiwa kwa gazeti hilo linalomilikiwa na Saed Kubenea wamezipata na tayari wameanza kuzungumza ili kuona wanaweza kushirikiana vipi na uongozi wa gazeti hilo kuhusu kesi hiyo.

"Ni kweli tumepata taariza za gazeti hilo kushitakiwa na Rostam hivyo kwa kuwa hivi sasa ni mapema mno kujua nini tunafanya, tumeanza kuzungumzia suala hilo. Jukwaa la wahariri tunatarajia kukutana haraka iwezekenavyo ili tuone tutashirikiana vipi na Saed Kubenea," alisema.

Sakina alikuwa akijibu swali aliloulizwa baada ya kuwasilisha mada katika mkutano wa kujadili wajibu wa vyama vya siasa, vyombo vya habari na asasi za kiraia katika kuendeleza demokrasia ya vyama vingi nchini.

Alisema binafsi anaamini wahariri watakapokutana wataweza kutoa mwelekeo mzuri zaidi wa kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri kwani wahariri wamekuwa wakishirikiana katika kushughulikia masuala mbalimbali yanayowabili wahariri na waandishi wao.

Alitoa kauli hiyo baada ya mmoja wa wajumbe waliokuwa katika mkutano huo kuuliza Jukwaa la Wahariri lina mkakati gani wa kumsaidia Saed Kubenea baada ya kushitakiwa mahakamani na Rostam Aziz.

"Tunataka kujua wahariri mmejipanga vipi katika suala la kumsaidia Kubenea ambaye amefunguliwa kesi na Rostam akidai kuwa gazeti la Mwanahalisi limemchafulia jina lake kwa sababu ya kumuandika kwa kumuhusisha na kashfa ya ufisadi.Tunaomba mtupe msimamo wenu kwa sasa,"aliuliza mjumbe huyo.

Katika kesi hiyo, Rostam anamshataki Mhariri Kubenea, na Pritench Company Limited wachapishaji wa gazeti hilo.

Kwa mujibu wa hati ya mashataka iliyosainiwa na Wakili wa Rostam, K.M Fungamtama, katika toleo namba 084, Februari 13 mwaka huu gazeti hilo katika ukurasa wa wake wa kwanza lilichapisha habari ikiambatana na picha ya Rostam yenye kichwa cha habari kisemacho"Richmondi ya Rostam Aziz-Ikulu",'Ndiye aliyeileta nchini', 'Lowassa alimuagiza'

Kubenea katika siku za karibuni amekumbwa na masahibu mengi ikiwa ni pamoja na kumwagiwa tindikali akiwa ofisini kwake pamoja na mhariri mshauri wa gazeti hilo, Ndimara Tegambwage ambaye alipigwa mapanga.

Baada ya mkasa huo, alipelekwa hospitali ya Muhimbili na kisha India ambako alitibiwa na kupewa miwani ya macho. Watuhumiwa walikamatwa na kesi bado inaendelea.
 
hatimaye, Bwana Mkubwa Rostam Aziz ameamua kukamilisha ile ahadi yake ya kukutana na waandishiw a habari. Atafanya mkutano wake na wahariri kesho Jumapili katika ukumbi wa Kibo 1, uliopo katika Hoteli ya Kilimanjaro kempisk. tafadhali sana kwa mliokuwa na hamu ya kutaka kwenda msiende kwa sababu imetolewa mialiko exclusive ambayo is non transfferable. Hi vyo ni uhakika kuwa watakaozamia watapigwa chini na msije mkawalaumu waandaaji kwa hilo.
Kwa mujibu wa mwaliko ambao mimi nimeuona, kati ya mambo atakayoyazungumzia ni ziara yake ya hivi karibuni katika kanisa la KKT ,agomeni na mchango alioutoa kwa kanisa (kwaya ya kanisa) hilo.
 
it is their move now... ! na jumatatu au jumanne wengine... the noose seems to be tightening around Sitta's neck... NImeanza kuwa na hofu ya nani kiongozi atakayefuatia kuwa hayati. Mungu aipushie mbali. Somebody need to take this act under control.
 
Just as i said here, this guy is a thug and he will choose the few waandishi he likes. So do it as waandishi wa ulaya, flock at the hotel, akishuka tu garini kabla hata ya kwenda ndani mbaneni maswali na mhakikishe kama hajibu basi mnaingia naye. Kama atalala hotelini basi mkae mlangoni wa chumbani kwake au mwa hilo chumba cha press!

Yale maswali niliyoyatoa hapa muulizeni huyo fisadi.

Asha
 
... So do it as waandishi wa ulaya, flock at the hotel, akishuka tu garini kabla hata ya kwenda ndani mbaneni maswali na mhakikishe kama hajibu basi mnaingia naye. Kama atalala hotelini basi mkae mlangoni wa chumbani kwake au mwa hilo chumba cha press!

Yale maswali niliyoyatoa hapa muulizeni huyo fisadi. Asha

Hakuna Press Tanzania ya kumbana Rostam Aziz. He is too much for them!
 
it is their move now... ! na jumatatu au jumanne wengine... the noose seems to be tightening around Sitta's neck... NImeanza kuwa na hofu ya nani kiongozi atakayefuatia kuwa hayati. Mungu aipushie mbali. Somebody need to take this act under control.

MMKJJ,

vidole hivyo! ... wenyewe wamesema wana mkono mrefu
 
hatimaye, Bwana Mkubwa Rostam Aziz ameamua kukamilisha ile ahadi yake ya kukutana na waandishiw a habari. Atafanya mkutano wake na wahariri kesho Jumapili katika ukumbi wa Kibo 1, uliopo katika Hoteli ya Kilimanjaro kempisk. tafadhali sana kwa mliokuwa na hamu ya kutaka kwenda msiende kwa sababu imetolewa mialiko exclusive ambayo is non transfferable. Hi vyo ni uhakika kuwa watakaozamia watapigwa chini na msije mkawalaumu waandaaji kwa hilo.
Kwa mujibu wa mwaliko ambao mimi nimeuona, kati ya mambo atakayoyazungumzia ni ziara yake ya hivi karibuni katika kanisa la KKT ,agomeni na mchango alioutoa kwa kanisa (kwaya ya kanisa) hilo.

Itakuwa vizuri kama akiwapa nafasi wamuulize maswali mbali mbali na ayajibu bila woga wala kificho ikiwemo ya Richmond/Dowans na yale aliyotaka kuzungumza Bungeni na kuzuiliwa kufanya hivyo na Sitta na kamati ya CCM bungeni, vinginevyo hakutakuwa na lolote la maana.
 
Damu ikimwagika hapa nchini ni Juu ya JK na si mtu mwingine yeyote yule!
Hawezi kukaa kimya tu na Upuuzi huu unaendelea!
Nani alimwambia agombee urais kama hawezi kuongoza?
 
Huyu Mh. wa Igunga Fisadi Rostam hajalikashifu Bunge aliposema pale kanisani (KKKT) kuwa kanisa halikufuata maneno ya kijiweni ambayo ni tuhuma za ufisadi juu yake... Tukumbuke kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliunda Kamati maalumu kwa ajili ya kuchunguza hilo sakata na kutoa taarifa mbele ya wabunge na yeye akiwemo. Sasa tangu lini Bunge letu likawa KIJIWE? Huyu fisadi kweli alishadharau watanzania na kuita chombo chao cha kutunga sheria kijiwe.
 
Pamoja na kuliita Bunge "kijiwe", Rostam aliishatamka kuwa Bunge ni sawa na "Ze Comedy". Tatizo la huyu jamaa ni kuwa hakai Bungeni, yuko busy kutoa statements kwenye vyombo vya habari anavyomiliki kama vile RAI (kifupi cha Rostam Aziz wa Iran). It is disgusting kuwa Wasukuma wa Igunga wamempa hata "uchifu"! Ama kweli pesa inatesa!
 
Wanasema TOA HELA!
 
"Mtikila hastahili heshima ya kujibiwa na mimi" na anasema "kama ingekuwa ni mimi tu anayemshambulia nisingemjibu, lakini kwa kuwashambulia KKKT Kinondoni, amevuka mpaka". Anasema Watanzania wasiwe na wasiwasi na dhamira yake njema.

anasema:

Alienda kwa mwaliko hakujipeleka
Justin Mkandala ndiye mzee wa Kanisa aliyeenda kumchukua nyumbani.
Alipokelewa na viongozi wa Kanisa na kwenda kutia sahihi kitabu cha wageni...
na baadaye kwenda kwenye hafla.

anasema hakwenda kujisafisha anadai na kusema "mimi ni msafi, najivunia rekodi yangu, naishi na mke na watoto wangu ninaowapenda, ni mfanyabiashara na nafanya biashara zangu kihalali kama wengine... hapa nchini na nje ya nchi, na ninawawakilisha kwa dhati wananchi wa Igunga"..

anasema "mimi si miongoni mwa wale walioshindwa kuishi na wake zao na kuchangamkia watoto wadogo wanaolingana na mabinti zao au wajukuu zao"
 
Back
Top Bottom