Ronaldo de Lima abatizwa na kuwa Mkristo!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,643
33,439
Mshambuliaji mashuhuri duniani Ronaldo de Lima amebatizwa katika Kanisa la Sao Jose do Jardim Europa Parish huko Sao Paulo.

Ronaldo de Lima ame post picha kwenye Instagram page yake na kusema "Imani ya Kikristo imekuwa msingi muhimu wa maisha yangu toka utoto ingawa nilikuwa sijabatizwa. Kwa sakramenti hii najisikia kuzaliwa upya kama mtoto wa Mungu kwa namna mpya, kihisia na kwa undani kabisa."

Hongera kwake kuamua kujikabidhi kwa Kristo.

Screenshot_20230914_124143.jpg
 
View attachment 2749085
Mshambuliaji bora wa mda wote nnae mjua mimi
 
Kubatizwa ni kuoga?
Usijali...huo ni mwili tuu...na mwili hauna manufaa yoyote mbinguni..

Ile roho ndio dhahabu ya mbinguni...au ww unahisi viwete wataenda mbinguni wakiwa viwete...acha hizo mkuu...

Maji mengi au kidogo haijalishi, mbinguni kwa Baba yake kuna makao mengi...ukiweza kufafanua hapo basi swala la yeye kunawa kichwa litafutika akilin mwako
 
Hapo habatizwi bali anaoshwa kichwa!
Wewe unataka battle za dini, kwenye ubatizo maji ni ishara tu na sio yanayotakasa. Hakuna andiko lolote linaloelekeza ubatizo uwe wa maji kiasi gani zaidi wengi mnakimbilia ku refer Yesu kubatizwa mtoni na maana ya ubatizo yaani kuzamishwa!

Kiasi cha maji hakijawahi kuwa issue toka enzi za mitume. Mkitoka kusema lazima yawe maji mengi itabidi tuulizane kiasi gani? Kwa maelekezo ya mapokeo au maandiko gani? Mkitoka hapo wengine watasema Yesu alibatizwa mtoni hivyo lazima ukabatizwe kwenye mto tu! Wengine watasema lazima uende mto jordan penyewe! n.k

Christianity sio imani ya juzi, tumepokezana miaka 2000 sasa kuanzia utaratibu wa ibada hadi masakramenti, you can't teach the church my friend! Hili sio Kanisa liloanzishwa na mtu tu.
 
Wewe unataka battle za dini, kwenye ubatizo maji ni ishara tu na sio yanayotakasa. Hakuna andiko lolote linaloelekeza ubatizo uwe wa maji kiasi gani zaidi wengi mnakimbilia ku refer Yesu kubatizwa mtoni na maana ya ubatizo yaani kuzamishwa!

Kiasi cha maji hakijawahi kuwa issue toka enzi za mitume. Mkitoka kusema lazima yawe maji mengi itabidi tuulizane kiasi gani? Kwa maelekezo ya mapokeo au maandiko gani? Mkitoka hapo wengine watasema Yesu alibatizwa mtoni hivyo lazima ukabatizwe kwenye mto tu! Wengine watasema lazima uende mto jordan penyewe! n.k

Christianity sio imani ya juzi, tumepokezana miaka 2000 sasa kuanzia utaratibu wa ibada hadi masakramenti.
Hayo mambo ya dini umeyaanzisha wewe!

Mimi nimekuulza unaelewa maana ya UBATIZO?
 
Back
Top Bottom