Rais Robert Mugabe alitimiza miaka 85 Jumamosi iliyopita na jitihada zimekamilika za kumwandalia hafla nzito Jumamosi hii ambayo itahudhuriwa pia na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai. Takriban dola za Marekani elfu 250 zimekusanywa na wafuasi wa Rais Mugabe kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Maadhimisho yatafanyiwa katika mji wa Chinhoyi, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Huku maankuli yakiandaliwa uchumi wa Zimbabwe umeporomoka na njia pekee yakuunusuru ni kuomba dola za Marekani bilioni mbili kutoka kwa nchi jirani.
Hadi sasa hakuna nchi yoyote ya kusini mwa Afrika ambayo imeitikia ombi hilo kwa kutoa ahadi ya kihakika.
Wakati huo huo visa vya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu inaongezeka. Zaidi ya watu elfu tatu unusu wakufa kutokana na kipindupindu.
Wenye shibe
Ili kupamba sherehe za 'Birthday' ya Rais Mugabe, mfanyibiashara mmoja ambaye pia ni afisa wa chama cha ZanuPF, Philip Chiyangwa alitoa mchango wa zaidi ya dola laki moja.
Serikali ya muungano inakumbwa na hali ya kutoaminiana
Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai ambaye amekuwa mpinzani mkali wa Rais Mugabe, naye pia hajawachwa nyuma. Atakuwepo.
Ni mwaka jana tu ambapo Bwana Tsvangirai alikejeli sherehe hizo na kuzitaja kuwa mkusanyiko wa wachache wenye shibe.
Muungano wa Rais Mugabe na Tsvangirai ungali unayumbayumba kutokana na hali ya kutoaminiana na kutokuwepo usawa katika ugawaji wa nyadhifa za uongozi.
Source: BBC