JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Akizungumza baada ya timu yake kufungwa magoli 5-1 katika mchezo dhidi ya Yanga, Kocha wa Simba, Roberto Oliveira “Robertinho” amesema kipindi cha pili wachezaji wake walipoteza umakini.
Amesema “Magoli mawili tuliyofungwa kipindi cha pili wachezaji wetu (Simba) walizubaa na kupoteza umakini, walifikiri kuna faulo wenzetu wakaendelea kucheza na wakafunga, nawapongeza wapinzani wetu (Yanga) kwa kushinda ‘Dabi’ na sisi tumepoteza mchezo muhimu.”
Kipigo hicho ni cha kwanza kwa Simba msimu huu katika Ligi Kuu Bara, pia ni cha kwanza kwa Robertinho dhidi ya Yanga tangu akutane na wapinzani hao katika mechi 4 ikiwemo pamoja na zile alizokuwa Vipers.