Road Safety: Stika za Nenda kwa Usalama ni wizi, tuungane kuupinga

Mie huja dereva wangu na kukusanya pesa za wafanyakazi woote wanaotaka stika 5000 na hurudi nayo kila mtu na ya kwake,
Ila mkuu hadi mfike mahakaman gari linatakiwa liwe limesimama/kulala polisi ambapo kila siku moja ni sh 30,000 na kama itatumia wiki basi ni 210,000 sawa na motor vehicle,we wape tu kama ni kupinga tuwatume wabunge wetu wawajibike.
Nipo Tayari ku-invest katika hili
 
Hii ya sticker ya kwenda kwa usalama ni kuwaibia wananchi bure kama gari halijakaguliwa, na hapo Tanzania sijaona kituo chochote rasmi cha kugagua magari. Kwa kawaida gari linatakiwa likaguliwe mara moja kwa mwaka na kuingizwa kwenye databse ya magari kama limekaguliwa na limepitishwa. Kama gari baada ya kukaguliwa limekutwa na ubovu, linabidi litengenezwe ili lipate kibali cha kuingia barabarani tena. Hata hivyo naona kwa Tanzania mtindo huo bado sana. Watu wataendelea kutajirika kwa kuwaibia wananchi.

Tuwagomee tu nashangaa watu wamekuwa wanaogopa
 
Mimi kila mwaka naenda pale Polisi ya Buguruni. Mwaka huu nikaenda. Nikamwambia afande natak &nbsp;sTIKA. Akaniuliza gari iko wapi, nikamletea karibu. Alivyoona inaanza na nmba C kwenye registration yake akasema kumbe ni mpya. Akanipa stika na &nbsp;nikalipia buku tano. Wala hakukagua gari.<br><br>Tunafanya hivi si kwamba tuna pesa nyingi bali ni kuepuka usumbufu wa hawa paka weupe
 
nchi hii ukiwa na gari shida

Utalipishwa stika ya usalama

Utalipishwa fire

Bado trafiki hawajakuwinda kuomba chai utafikiri wewe ni baba yao au ndo umewaleta mjini

Bado mtaani kuba wahunj wanaojifanya kutengenezA barabara wakuombe 200-500 (hawa ukiwanyima sana huchelewi kukuta huna power window)

Hapo hujakutana na waosha vioo wakung'ang'anie

Huu ni unyonyaji unaoongozwa na viongozi wetu

Yaani serikali ikukamue
Trafiki wakukamue
Hata mtaani wakukamue!!
 
Ndugu yangu nchi hii ina shida nyingi uwezi kuhamini... kila eneo shida

1. Chakula shida
2. Maeneo tunayoishi shida hakuna huduma yoyote ya Jamii.. maji ya kununua kwa matenki... Umeme kuupata shida kuutumia shida....
3. Mitaa tunayoishi haieleweki
..... barabara na viwanja kupimwa ni ndoto ... kila kitu ovyo..
4. Baa kila mahali kelele ... vumbi...

.. unaweza jaza JF Saver ukiendelea kuelezea .... kifupi tu ni kwamba...

Bado hatujapata uhuru.. Mpaka tutakapopata uhuru mambo yatabadilika .. kwa sasa nchj inaenda kwa remote...

nchi hii ukiwa na gari shida

Utalipishwa stika ya usalama

Utalipishwa fire

Bado trafiki hawajakuwinda kuomba chai utafikiri wewe ni baba yao au ndo umewaleta mjini

Bado mtaani kuba wahunj wanaojifanya kutengenezA barabara wakuombe 200-500 (hawa ukiwanyima sana huchelewi kukuta huna power window)

Hapo hujakutana na waosha vioo wakung'ang'anie

Huu ni unyonyaji unaoongozwa na viongozi wetu

Yaani serikali ikukamue
Trafiki wakukamue
Hata mtaani wakukamue!!
 
Watu wanakufa kila siku, kwa nini usalama wa barabarani uwe suala la kuzingatiwa na kutiliwa mkazo wiki moja tu?
 
Kamtaji ka washkaji hako na wanavyozigombania zikija utasikia mi Sina nenda kwa fulan unaenda unaambiwa anauzia stand.wanaficha wiki iishe wauze bei kubwa wizi mtupu.
 
wadau sijui kama kuna mwenzangu ambaye amekutana na kadhia ya hawa jamaa( TRAFFIC POLICE), wanadai stika ya wiki ya kwenda kwa usalama, hali ya kuwa stika hapa polisi trafic hakuna. wanakusumbua hadi uwape hela ndo wanakuachia.
 
Mi kuna mmoja alinikamata tena kanionea tu kwa hasira nikaenda nae kitu kimya kama bubu kufika nikapiga simu nikampa aongee akabakia "samahani akuniambia" pumbavu sana hao
 
Nimekutana na mtu mmoja katika kituo cha kujaza mafuta pale round about ya stand ya daladala Morogoro mjini anauza sticker za wiki ya nenda kwa usalama kwa Tshs 5,000 huku zikiwa zimeandikwa kiasi cha Tshs 3,000, nilipomwuliza kwanini unaziuza wewe raia wakati zilitakiwa zitolewe na kikosi cha usalama barabarani baada ya kufanya ukaguzi wa gari, akanambia hao usalama barabarani ndiyo wameniuzia zote nilizonazo mkononi.

Nimejiuliza swali huu utaratibu wa raia kuuza sticker umelipeleka jeshi la polisi hususani kikosi cha usalama barabarani likizo?

Kuna sababu gani kuuza stucker kama ukaguzi wa magari haufanyiki kama sheria inavyotaka?

Huyo kiongozi wa kikosi cha usalama barabarani aliyempa raia burungutu la sticker aziuze anatambua madhara yake?

Huyo kiongozi anayepaswa kuzitoa sticker hizo kwa magari yaliyo kaguliwa anafanya kazi gani kama kazi yake imekabidhiwa kwa raia?
 
Gosh, leo nimesimamishwa na trafiki hapa mwanza kaniuzia tsh 10, 000/. Huo ni mradi wa askari wa usalama barabarani
 
Dah huyu jamaa hapa round about (Lake Oil) nami kaniambia nikienda kituoni na kupata hizo stika atanirudishia buku 5 na elfu 2 za usumbufu. Huu ni mradi wa wakubwa.
 
Tuzikatae kwani tayari tunalipa road license, bima, parking fees, mafuta levy etc. Huu ni uonevu tu, kisha tukishazichanga wanapeana na watoto zao
 
Ubinafsishaji ndo sera, huo ni mwendelezo tu mkuu. Kesho subiri gereza binafsi you pay before. Ila huduma utapata tv gazeti vitabu vyakula customer service ya juu and no virungu.
 
Back
Top Bottom