RITA yapiga marufuku uvaaji wa mavazi yasiyofaa

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Kwenye ofisi za RITA kuna hili tangazo.

TANGAZO

Ndugu wapendwa wateja wetu, mnakumbushwa kwamba hii ni taasisi ya Serikali ambayo inaendeshwa kimaadili hivyo basi hatutapendelea baadhi ya mavazi yasiyofaa na yasiyo na heshima kuvaliwa ofisi kama yafuatayo:-
  1. Mavazi yanayofunika uso wote - Kininja "Nikab".
  2. Singet (fulana zisizo na mikono)
  3. Kaptula
  4. Suruali zinazolegea "Mlegezo"
  5. Kofia kubwa "Parma"
  6. Vitop vya kike vinavyoonyesha vitovu
Wateja wetu mnakumbushwa kwamba atakayekiuka maagizo hayo hapo juu hataruhusiwa kuingia ndani kupata huduma zinazotolewa na Wakala.

UTAWALA
08 Februari 2011


rita.jpg
 
Hiyo namba 1 sio sahihi kabisa. Ku-list nikab kama mavazi yasiyofaa ni uonevu.
Sasa hata wateja wanakuwa monitored, kama natoka kukaanga samaki ferry napitia vyeti vyangu inabidi nibebe suti kwenye kirambo? Badala ya kukazania ufanisi wanaangalia mavazi, bongo bwana!
 
Hilo tangazo mushkeli:
  • Halina nembo ya RITA
  • Halina sahihi ya mtoa tangazo
Hivo huu ni uchonganishi tu.......tuupuuzilie mbali.....vaa NIKABU,SINGLENDI,KAPTURA etc yako nenda kadai cheti cha kuzaliwa
 
Mtu akienda kitovu nje hawatampa huduma? Kwa sheria gani ya nchi mtu hahudumiwi na serikali kisa maadili?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hii thread tayari ipo!...LAKINI IMEKUWA CLOSED KUTOKANA NA UCHANGIAJI HASI!


https://www.jamiiforums.com/habari-...rita-yapiga-marufuku-nikab-2.html#post3335595

Nimeona. Nafikiri tatizo ni huyo aliyeanzisha ile thread. Alibase kwenye vazi moja tuu tena la kidini wakati suala ni pana zaidi. Nafikiri hiyo ndio iliyosababisha michango hasi. Hope hawatafunga hii pia na naomba wachangiaji wajadili kwa mapana zaidi badala ya ku-stick kwenye vazi moja la kidini. Usikute hili lina uhusiano na vazi la taifa.
 
Mtu akienda kitovu nje hawatampa huduma? Kwa sheria gani ya nchi mtu hahudumiwi na serikali kisa maadili?

Je, hizi ni dalili kuwa vazi la taifa lipo njiani linakuja?
 
Hilo tangazo mushkeli:
  • Halina nembo ya RITA
  • Halina sahihi ya mtoa tangazo
Hivo huu ni uchonganishi tu.......tuupuuzilie mbali.....vaa NIKABU,SINGLENDI,KAPTURA etc yako nenda kadai cheti cha kuzaliwa

nakubaliana na wewe kabisaa.

Mtoa mada hakuliona hilo.

Lakin vile vile lazima ajue kuwa Tz kuna dressing code za kuingia kwenye taasisi zake zote.
Kwani RITA siku hizi ni private ompany?

 
nakubaliana na wewe kabisaa.

Mtoa mada hakuliona hilo.

Lakin vile vile lazima ajue kuwa Tz kuna dressing code za kuingia kwenye taasisi zake zote.
Kwani RITA siku hizi ni private ompany?


Naomba ushuhuda wa aliyekosa huduma RITA kwa ajili tu ya uvaaji wake?
 
Hilo tangazo mushkeli:
  • Halina nembo ya RITA
  • Halina sahihi ya mtoa tangazo
Hivo huu ni uchonganishi tu.......tuupuuzilie mbali.....vaa NIKABU,SINGLENDI,KAPTURA etc yako nenda kadai cheti cha kuzaliwa

Mkuu lakini kuna mwananchi anadai ameenda pale kupata huduma akakataliwa kwa sababu alikuwa amevaa kaptula. Hatuwezi kulipuuzia kama kweli watu wanakataliwa huduma kutokana na mavazi yao. Soma hapa: MICHUZI: yale yaleeeee....
 
Back
Top Bottom