Risasi Zaruka Pemba: Ni Katika Zoezi La Uandikishaji Wapiga Kura

Inachukiza, yaani CCM inalazimisha kubaki madarakani kwa mtutu wa bunduki?
Inachukliza zaidi kuona CUF wanataka kuingia madarakani huko Zenj kwa njia za ubabe , za kijahilia, za kiharamia zisizo za kistaarabu na zenye kuhatarisha maisha ya wanajamii.
 
Kusema kweli WaPemba wanastahili hongera jamani ,ni watu ambao hadi sasa wameonekana kustand na vyombo vya dola ,na wanasimama kidete ,ikiwa vituo vilifikia kufungwa basi mjue kuwa walikuwa ngangari kinoma sio mchezo .

Mfano ambao wanauonyesha ni mfano hai ambao unafaa kuigwa na sehemu yeyote hapa Tanzania ili kuikataa dhulma.

Ila naona Mkapa amepewa salaamu na watu wa Pemba open kabisa mchana kweupe kuwa ajiandae any time kutokea sasa ataitwa kujibu tuhuma za mauaji ya halaiki ya watu katika kipindi cha utawala wake ,asidhani kasahaulika au haliwezekanai ,mambo yapo katika hatua za mwisho ,aombe huko Tanganyika wamfunge na mapema kwa tuhuma za ufisadi vinginevyo ,WaPemba wamekusudia kutoa onyo.

"Tunachohitaji ni daftari tofauti kwa Zanzibar na Muungano ili watu wapige kura kwa haki kinyume cha hapo watamuunganisha Kikwete na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ambaye anaandaliwa mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya The Hague."
 
kama anatishia amani na maisha ya wengine walio wengi afanywe nini? atizamwe tu - tungojee ushahidi wa kinyamwezi- hapo atakapokuwa ameshawaangamiza wenziwe pengine wapatao kumi?
Hii hadithi ya mwanambuzi na chui, nani anachufua maji ya mto, ni chui aliyeko juu yanakotokea au mwanambuzi aliyeko chini yanakotiririkia?
Kife Chama cha Kafu, na uharamia wao Lo!
Nani haramia tokea mwaka 1977 hadi leo wangapi wameuliwa, wamedhulumiwa, wamfungwa jela, wameteswa, wamebabikiwa kesi, wamenyan'ganywa na kuharibiwa mali zao na kulazimishwa kuwa wakimbizi na hayo kayafanya nani?
Inachukliza zaidi kuona CUF wanataka kuingia madarakani huko Zenj kwa njia za ubabe , za kijahilia, za kiharamia zisizo za kistaarabu na zenye kuhatarisha maisha ya wanajamii.
Bado una mawzo ya Ki-Omari Mapuri kuwa eti CUF wanataka madaraka ili wamrejeshe Sultani, what for? Kama njia za ubabe nani ana dola, nani ana mahakama na nani anatunga sheria kandamizi kati ya chama tawala na wapinzani. CCM imeshamwaga damu kwa kulazimisha kubaki madarakani huu si ujahilia, uharamia na ubabe. Au kuweka makambi ya vijana kule Tunguu, Hanyegwamchana na Kama (Janjaweeds camps) ndo ustaarabu wa unaouzungumzia, au kuweweka watu magerezani kwa kesi zisizo mbele wala nyuma huo ndo ustaarabu wa kidemokarasia, kweli watu si mapapai kama wataoza jela kama "komandoo" wenu alivyosema lakini je ni uungwana na utu kuwa jahili kama vile? CCM wasiseme kitu kuhusu utu na ubinaadamu wao ni madhalimu wa rangi zote za kipigi.
 
Tunajua sote kuwa Pemba ndio kitovu cha upinzani Zanzibar.Wanachofanya Serikali ya Mapinduzi na CCM ni kuhakikiksha wanawadhibiti wananchi wa Pemba ikewemo kuwapiga kuwanyanyasa na ikibidi kuua.Lakini iko siku itafika yote haya yatakwisha !
 
Uchaguzi safari hii utakuwa mgumu kwani hakuna ajenda mpya. Mengi yalizungumzwa 1995, 2000, na 2005 na kwa huu unaokuja itakuwa vigumu kupata la kufanyia kampeni.

Haya tunayoyaona ni katika kutafuta agenda ya kampeni na wanasiasa wetu wapo tayari hata kuyaweka rehani maisha ya wafuasi wao ili mradi lipatikane la kuongelea.

Kila upande wanajaribu-jaribu jambo fulani kuona linavutia kwa kiasi gani: tumesikia ya mafuta ambayo hakika wala hayapo, na yale ya mpira FAT-ZFA; na yote hayaonyeshi kusaidia kampeni ya 2010.
 
hivi busara ya kawaida tu , nchi za wenzetu siku hizi hata ukiwa nje waweza kupiga kura, sasa hii ya wenzetu ya mtu ukitoka kidogo ukirudi, haki ya kupiga kura inakuwa na utata, kama huja kaa sehemu hii kwa miaka au miezi kadha, je hii ni haki? ndio kukuza demokrasia yenyewe? je watawala wana hofia nini? na hata idadi yenyewe haiwezi kuwa zaidi ya 10% ya wapiga kura kwa kisiwa kama pemba lakini , hii kitu ni mgogoro huko visiwani kulikoni?
 
Back
Top Bottom