Invisible
Robot
- Feb 11, 2006
- 9,075
- 7,878
- Thread starter
- #41
Umenena vema mkuu FM,Lakini kama kuna major structural au technical failure, inayofanya jengo lisiweze kutumika ipasavyo, kinyume cha maagizo ya mshitiri hii sifahamu lakini naamini inadumu kwa uhai wa jengo. Kwa mfano, kama kuna conference room ghorofani iliyotakiwa kuchukuwa watu mia lakini haijawahi kuchukuwa watu hao hadi miaka kumi kupita. Ikiwa baada ya miaka kumi, mshitiri akapata mkutano wa watu mia na jengo kuanguka kutokana na uzito wao, basi wataalam wote watakuwa liable (kuanzia msanifu majengo hadi mhandisi wa structures). Hasa ikiwa walikagua na kupitisha kazi ya mkandarasi kuwa ilifanyika kama walivyomuagiza.
Hivyo ndivyo ninavyoelewa. Labda nimekosea.
Lakini bado pia Structural Designer anaweza kuwa hana hatia endapo Design span ilishapitiliza.
Wasiwasi wangu ni huu, jengo hili ukiliangalia vema utaona kuwa watoto wote walianza kutegemea sehemu moja ya kutolea hewa kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini, siamini kama professional designer yeyote anaweza ku-recommend upupu huu: