Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Kwa nini hao Wabunge wa CCM wanataka kukutana wenyewe? Hivi wanachi wataendelea kusalitiwa mpaka lini? Kweli watajadili hiyo ripoti kwa moyo wa kizalendo au ndio watajifanya kubweka tu, wakiwa wameelekezwa cha kusema? Yetu macho na masikio..halafu mauvimivu makali..ila hatujazoe..ipo siku..nayo ni leo....MTANZANIA AMKAAAAAAAAAAAAA

..wanakutana kuwekana sawa.

..kule kuzomea hakukuwa kwa kawaida.

..i hope "watawekana sawa".
 
Hapa issue sio kukutana na kuwekana sawa,jamaa washajua mzee kajamba,waliogopa kumwambia kajamba,mzee keshaona jamaa wameshtukia kuwa ni yeye mjambaji,lakini kama ilivyo kawaida mkubwa hakosei,anatafutwa mtu ataebebeshwa hilo shuzi,na hali ilivyo yaelekea ni ngumu,hivi tunavyo zungumza kuna vidagaa vidogo vinatafutwa,vikamatwe fasta,vipelekwe mahakamani fasta,ikishafika huko pm,atakua amesalimika,maana bunge halitakua na mamlaka ya kujadili kilichoko mahakamani.mwaonaje.
 
Nasikia dakika za mwisho mwisho za uchunguzi waliweza kuona mpini wa ile bunduki ifukayo moshi... na kuna uwezekano alama za vidole zilibakia. Hilo linawatisha.
 
halitakua na mamlaka ya kujadili kilichoko mahakamani.mwaonaje.

Hili changa la macho wazeee.....lakini siku zao zinahesabika time will be a good judgemet mi nasubiri tu wacha waruke ruke wataingia tu kwenye urimbo.

...watacheza na mahakama iliwatuzuge tusahau kama tunavyoelekea issue za, Zombe,IPTL, Ditopile, Mahalu and soon BOT, Rich Monduli, na Buzwagi....

Lakini ......itafikia wakati wananchi watajua nini cha kufanya zaidi ya kwenye vyumba vya kupigia kura, maana yalitokea Kenya hayatafutika vichwani mwa watanzania. Mungu ibariki Tanzania laani na wape mikosi Mafisadi ....amen
 
Nasikia dakika za mwisho mwisho za uchunguzi waliweza kuona mpini wa ile bunduki ifukayo moshi... na kuna uwezekano alama za vidole zilibakia. Hilo linawatisha.

Mpaka sasa natafuta mahakama yenye jurisdiction over this one ila siioni! Yaliyofanyika hapa ni makubwa na sidhani kama vitisho peke yake tu vitatosha. Tatizo ni kwamba aliyejaribu kuificha hii bunduki alisahau kuvaa gloves kwa hiyo alama zake za vidole nazo zilibakia, akafanya makosa pia akaificha bunduki kwenye scanning room ambayo iliscan bunduki yote na kutuma hizo alama za vidole kwenye remote and secure storage room......

Nadhani ifike wakati wananchi waambiwe kuchukua sheria mkononi kama vile wanavyofanya kila siku kwenye vituo vya mabasi mikoani dhidi ya wezi wa mfukoni.
 
Jamani,hapa ninawasiwasi saana,na uwezo wa wabunge wetu kuhimili vitisho vya mtu kama pm,nina wasiwasi saana na kile wakiitacho nidhamu ya chama,ambayo kwayo inazidi ile ya wananchi ambao wamewapeleka kule,kumbuka pia,wakiikubali hii,haswa ya bot,ambayo inasemekana walipata pasu walilotumia kwenye kampeni zao za ubunge japo kidogo,itakua ni mwisho wa chama na mwisho wao pia kihali ,kimali na kisiasa.mwaonaje
 
..mama kilango-malecela anaweza,lakini sidhani kama atafanya hivyo.

Kwa nini huamini kwamba Mama Kilango Malecela hawezi kumkoma nyani mchana kweupe? Huyu ana ghadhabu na mtandao kwa sababu walimbania nafasi ya kuwa na EOTF yake, baada ya mumewe kumwagwa kule Chimwaga.
Watamjua kwamba yeye ni nani.
 
Kwa nini huamini kwamba Mama Kilango Malecela hawezi kumkoma nyani mchana kweupe?

..issue sio kuamini. na ndio maana nikasema anaweza! ashafanya mambo hayo mara kadhaa!
Huyu ana ghadhabu na mtandao kwa sababu walimbania nafasi ya kuwa na EOTF yake, baada ya mumewe kumwagwa kule Chimwaga.
Watamjua kwamba yeye ni nani.

..na hii ndio huwa inampa charge! ila,sidhani kama atasimama uwanjani mwenyewe na kutangaza vita dhidi ya EL.
 
Sasa KIKAO CHA WABUNGE WA CCM, kesho USIKU.... na mambo yote yatawekwa hadharani hiyo kesho kabla ya watu kuanza "kutema cheche" Alhamisi
 
Nasikia dakika za mwisho mwisho za uchunguzi waliweza kuona mpini wa ile bunduki ifukayo moshi... na kuna uwezekano alama za vidole zilibakia. Hilo linawatisha.

Mheshimiwa Mzee Mwanakijiji,

Haunitendei haki kabisa unapoondelea hiyo bunduki.....halafu jamaa wanasema thank you...duh, ina maana niko peke yangu nisiyeona nini??

Ukiweza nipe dondoo basi.....aksante
 
EL IS SICK OF AL FASADI DISEASE,tangu lini waziri mkuu akaitisha kikao cha baraza la mawaziri?tena cha ghafla..huu ndio ubia ambao muungwana hataki kuukubali,HAO wanaotaka kumfufua THE LATE AMINA,naomba wamfufue na marehemu mwalimu JULIUS JK nyerere,aje aone ccm aliyoitabiri!
 
EL IS SICK OF AL FASADI DISEASE,tangu lini waziri mkuu akaitisha kikao cha baraza la mawaziri?tena cha ghafla..huu ndio ubia ambao muungwana hataki kuukubali,HAO wanaotaka kumfufua THE LATE AMINA,naomba wamfufue na marehemu mwalimu JULIUS JK nyerere,aje aone ccm aliyoitabiri!

Kwamba anaugua ni SAHIHI na kwamba wamfufue Nyerere aone ni sahihi lakini PM ana madaraka ya kuitisha kikao cha utendaji cha mawaziri na manaibu wote si Baraza la MAwaziri japo linaweza kuwa baraza dogo
 
ina maana the comedy wanafanya maonyesho yao kesho,kwa hiyo na tiketi ni hapo hapo mlangoni au itakuwaje? mimi nashauri wauze hizo tikeki online ilikupunguza vurugu pale mlangoni.
 
Hivi ni nani huwa anaitisha na kuongoza kikao cha balaza la mawaziri TZ?? Miye nilidhani ni Rais!!
 
sidhani kama hiki ni kikao cha Baraza la Mawaziri lakini Kikatiba (ibara ya 54:2) inampa uwezo Waziri Mkuu kuongoza kikao cha Baraza Mawaziri endapo Rais au Makamu wake hawapo.
 
sidhani kama hiki ni kikao cha Baraza la Mawaziri lakini Kikatiba (ibara ya 54:2) inampa uwezo Waziri Mkuu kuongoza kikao cha Baraza Mawaziri endapo Rais au Makamu wake hawapo.

Asante Mkuu kwa kunielewesha. Naona katiba umeikariri mwenzetu (joke)!!!
 
Back
Top Bottom