Ripoti ya CAG kwa mwaka ulioishia 30 Juni, 2017 imejaa madudu

Sijasoma ripoti ya CAG lakini niliwahi kusema humu JF,kutokana na Bunge kutokuwa na nguvu pamoja na zile kamati zake zinazoibuaga madudu ya serikali kuongozwa na makada na bunge lenyewe kutokuwa live,viongozi kuona kwamba kuikosoa serikali hii ni kukosa uzalendo na uzalendo ni kumuunga mkono mkuu katika kila jambo,vyombo vya habari kusifia na kupongeza tu na kuficha habari za kukosoa/uoga. Watu watapiga sana fedha zetu.
 
hawana uwezo wa kujibu wanasubiri teuz tanzania bado sana tuna viongozi wachache sana wenye kupigania uhalisia wa nchi ila wengi wao n pesa kwanza
 
Wenzetu nyie ni miongoni mwa wanasiasa waliohama vyama vya upinzani na kujiunga na CCM kwa madai ya kuridhishwa na utendaji wa serikaki ya Rais Magufuli huku baadhi yenu mkilaumu wapinzani kwa kupinga kila kitu.

Baada ya ripoti ya CAG kutoka ya mwaka wa fedha wa 2016/2017, ningependa kusikia maoni yenu nyinyi pamoja na wale wengine wote waliohama upinzani na kuhamia CCM ili kumuunga mkono mheshimiwa.

Je,kwa upotevu huu mkubwa wa fedha za umma,mtahama tena CCM?

Kwa tuhuma hizi za upotevu huu mkubwa wa fedha za umma na matumizi haya makubwa ya fedha za umma nje ya bajeti, tuambieni CCM ya Kikwete na hii ya Magufuli ipo bora?

Je,sasa mmeamini maneno ya viongozi wa dini kuwa "kiongozi mzalendo si mbadala wa Katiba mpya"?

Tuambieni mnajifunza nini?

Katambi na Kitila Mkumbo sijawasahau.

Naombeni majibu.

Yaani mumpe hela KINENEKO halafu mnatafuta maoni kwa Kafulila na Machali? Mnaumwa?
 
Mhhh!! Nimesikitishwa sana na hili la Sheria Mpya ya madini kumbe Wabunge wa CCM wakishirikiana na Spika Bungeni huwa wanafanya fujo za kuwatoa wabunge wa Upinzani hususani wale wa UKAWA ili wapitishe madudu kama haya? Hivi inakuwaje Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG asiruhusiwe kukaguwa maeneo ya migodi? je ni kweli tuna nia ya dhati kulinda lasilimali zetu hususani madini?
 
Hivi kama umemtengea mkandarasi bilioni 10...na so far amefanya kazi ya bilioni 2 na amepata certificate ya bilioni 2 ...matumizi ya fedha yataonekana ni bilioni ngapi?

kwa lugha nyingine...umezicommit bilioni 10 kujenga barabara but uwezo wa mkandarasi kwenda na kasi ni bilioni 2 so far ...utampatia ili uonekane umetekeleza?

wewe ni mchumi hebu nijibu!

Kwa swala la wakandarsi lipo wazi na unaeleweka, ila narudia utekelezaji w abajeti kwasasa ni alomost 50% kwanini na wakati maksuanyo ni 90%, huku halmashhuri hela aziendi mawizarani hivyo hivyo au husikii ndugu? na hizo hela sio za wakandarasi tu, hata hela za maendleo ya kawiada hakuna.

By the way kama tunajua mkandarasi amalizi kazi mwaka huu kwanini tutenge hela yote, na nijuavyo mimi JPM akiw awaziri alisharekjebishaga hilo, hela huw ainatengwa kwa makadiro ya kazi ya mkandarasi mwaka huo tu na sio hela yote.
 
Mhhh!! Nimesikitishwa sana na hili la Sheria Mpya ya madini kumbe Wabunge wa CCM wakishirikiana na Spika Bungeni huwa wanafanya fujo za kuwatoa wabunge wa Upinzani hususani wale wa UKAWA ili wapitishe madudu kama haya? Hivi inakuwaje Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG asiruhusiwe kukaguwa maeneo ya migodi? je ni kweli tuna nia ya dhati kulinda lasilimali zetu hususani madini?
Ipo taasisi maalum ya umma inayofanya ukaguzi wa migodi na madini nchini (Tanzania Mineral Audit Agency).
 
Ipo taasisi maalum ya umma inayofanya ukaguzi wa migodi na madini nchini (Tanzania Mineral Audit Agency).
Una uhakika mbona hii TMAA ilifutwa baada ya kuonekana imehusika kuihujumu nchi katika lile suala la makinikia?
 
Tuliaminishwa na CAG kuwa ripoti yake ni siri na itabaki kuwa siri hadi pale itakapowasilishwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa. Tuliaminishwa pia na Prof Assad kuwa alichotoa kwa public wakati ule ni Muhtasari wa muhtasari na siyo ripoti kamilifu. Cha ajabu hadi kufikia leo mawaziri kadhaa wameshaifanyia kazi ripoti hiyo na kuwasimamisha kazi watendaji kadhaa, waziri mwingine kaunda na tume ya uchunguzi kabisa. Kama hiyo haitoshi Kiongozi wa ACT naye katoka na ripoti kamili hadharani na kuanza kuichambua hali iliyopelekea mume wa mbunge wa Chadema naye kuibuka hadharani na ripoti nzima ya CAG na kuanza kujibizana na Zitto. Ndio najiuliza baada ya kujadiliwa bungeni mapendekezo watayapeleka wapi kwani serikali kwa maana ya mawaziri watakuwa wameshaifanyia kazi. Nawasilisha!
 
kuna jamaa humu wanaquote hadi vipengele.
hivi inapatikana wapi ili nasisi wakulima tusome na tuchambue kwa akili yetu timamu.
 
Hivi seriously kuna watu bado mnapromote usirisiri? Zimeanda wapi zama alizoanzisha Mkapa za uwazi na ukweli? By the way, kujadiliwa mtaani si ndo kunalipa bunge nyenzo na dhana za kujadili kwa upana zaidi na ku-address concerns za wananchi?
 
Tanzania ni taifa la wafukunyuku, ndio maana report nyingi zinatuonyesha tuko mbeke kwenye haya mambo ya siasa, huwa tunajidharau tu lakini tuko mbele, jiulizeni katika nchi za EAC huwezi sikia mambo kama haya ya CAG anatoa report na nchi nzima inaanza kujadili kwa uwazi, ni hatua nzuri pia. Kwa sasa report iko out, hata ukienda cyber unaipata tu, hii ndio bongo.
 
Back
Top Bottom