Ripoti ya CAG, je jeshi la Polisi, TAKUKURU wanatimiza wajibu wao?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Mdhibiti na mkaguzi wa fedha za umma amekuwa anatoa ripoti za ukaguzi wa matumizi na mapato ya serikali na matumizi ya serikali.

Kila ripoti imejaa ushahidi tena wa kitaalam namna ambavyo fedha ya umma imetumika ama kuchezewa kupitia vote mbalimbali zilizopitishwa na Bunge.

Jambo la kushangza kuhusu ripoti ya CAG ni kwamba sheria inalitaka Bunge kujadili na kushauri hatua za kuchukuliwa wale wote wanaoonekana kufanya madudu au kusababisha hati chafu kwenye mamlaka walizopo.

Ajabu zaidi ni kwamba, ripoti za CAG zimesheheni ushahidi pasi shaka kuhusu matumizi ya fedha za umma. Lakini sheria ambayo inapaswa kutafsiriwa kupitia mahakama imepindishwa na kuelekeza Bunge na Rais ndo wenye maamuzi nini kifanyike.

Sheria isiyotambua umuhimu wa proccess kuelekea kwenye HAKI ni sheria inayolenga kukwepesha uwajibikaji na utakatifu wa matumizi ya fedha za umma. Jeshi la polisi ambalo kimsingi linawajibika kwenye ulinzi wa umma limekuwa kama haliguswi na huu uhalifu mbaya kabisa wa matumizi mabaya ya fedha za umma. TAKUKURU ambao wamewezeshwa kisheria kuchunguza na kushughulikia kesi za ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi. Lakini kwenye hili sakata la ripoti za CAG mamlaka hizi za kutekeleza sheria zimekuwa na kigugumizi kikubwa kuchukua hatua. Upo uwezekano mkubwa kwamba sheria zetu zina meno ya kutosha dhidi ya mwenendo wa kisiasa unaotishia maslahi ya CCM kuliko ulinzi wa umma yaani, maliasili, fedha za umma na uwajibikaji wenye tija.

Jeshi la Polisi na TAKUKURU wanapaswa kujitafakari ni nani wanayemtumikia kati ya sheria/Katiba/umma au wanatumikia maagizo kutoka juu.

Ni aibu kwa nchi kuwa na taasisi dhaifu ambazo zinatumia nguvu kubwa kupambana na raia wanyonge huku zikilinda maslahi ya wezi, mafisadii na wabadhirifu wa mali ya umma.

SWALI
Nini kinawapa kigugumizi Polisi na TAKUKURU kushughulikia makandokando yaliyoainishwa kwenye ripoti ya CAG?
 
Chama cha majizi ndio kizuizi cha madudu yote serikalini watu wasiwajibishwe..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakumbuka lakini agizo la nambari wani alilosema?
Ndio maana wanatuona manyani tuuu
8112630c564f73deab9ae715b6405c4f.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdhibiti na mkaguzi wa fedha za umma amekuwa anatoa ripoti za ukaguzi wa matumizi na mapato ya serikali na matumizi ya serikali.

Kila ripoti imejaa ushahidi tena wa kitaalam namna ambavyo fedha ya umma imetumika ama kuchezewa kupitia vote mbalimbali zilizopitishwa na Bunge.

Jambo la kushangza kuhusu ripoti ya CAG ni kwamba sheria inalitaka Bunge kujadili na kushauri hatua za kuchukuliwa wale wote wanaoonekana kufanya madudu au kusababisha hati chafu kwenye mamlaka walizopo.

Ajabu zaidi ni kwamba, ripoti za CAG zimesheheni ushahidi pasi shaka kuhusu matumizi ya fedha za umma. Lakini sheria ambayo inapaswa kutafsiriwa kupitia mahakama imepindishwa na kuelekeza Bunge na Rais ndo wenye maamuzi nini kifanyike.

Sheria isiyotambua umuhimu wa proccess kuelekea kwenye HAKI ni sheria inayolenga kukwepesha uwajibikaji na utakatifu wa matumizi ya fedha za umma. Jeshi la polisi ambalo kimsingi linawajibika kwenye ulinzi wa umma limekuwa kama haliguswi na huu uhalifu mbaya kabisa wa matumizi mabaya ya fedha za umma. TAKUKURU ambao wamewezeshwa kisheria kuchunguza na kushughulikia kesi za ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi. Lakini kwenye hili sakata la ripoti za CAG mamlaka hizi za kutekeleza sheria zimekuwa na kigugumizi kikubwa kuchukua hatua. Upo uwezekano mkubwa kwamba sheria zetu zina meno ya kutosha dhidi ya mwenendo wa kisiasa unaotishia maslahi ya CCM kuliko ulinzi wa umma yaani, maliasili, fedha za umma na uwajibikaji wenye tija.

Jeshi la Polisi na TAKUKURU wanapaswa kujitafakari ni nani wanayemtumikia kati ya sheria/Katiba/umma au wanatumikia maagizo kutoka juu.

Ni aibu kwa nchi kuwa na taasisi dhaifu ambazo zinatumia nguvu kubwa kupambana na raia wanyonge huku zikilinda maslahi ya wezi, mafisadii na wabadhirifu wa mali ya umma.

SWALI
Nini kinawapa kigugumizi Polisi na TAKUKURU kushughulikia makandokando yaliyoainishwa kwenye ripoti ya CAG?
WAPIGAJI WOTE NI MAKADA WA CCM USITARAJIE MAAJABU KTK HILI HAKUNA HATUA ZOZOTE ZITAKAZOCHUKULIWA MPAKA REPORT NYINGINE IJE IFUNIKE REPORT HII
 
Back
Top Bottom