Elections 2010 Richard Ndassa Atumia Lugha ya Kisukuma Kufanya Kampeni

tartoo

Senior Member
Jul 2, 2010
129
2
Kwa waliokuwa wanatizama taarifa ya habari ya saa mbili usiku leo TBC1 bila shaka mmeyaona.

Ndugu yangu Richard Ndassa alikikoroga, na mie sijapata kitu kabisa.

Kanuni na sheria zasemaje kuhusu hilo.

Wanasheria mtujuze
 
Kama sikosei maadili ya uchaguzi mkuu yanavitaka vyama vya siasa kutumia lugha ya kiswahili katika kampeni na
kutumia wakalimani kutafsiri pale jamii husika inapokuwa haiielewi lugha ya kiswahili. Adhabu kwa kukiuka
yaweza kuwa faini au kubatilishwa kwa mgombea pale anapoendelea kukaidi.
 
Kwa waliokuwa wanatizama taarifa ya habari ya saa mbili usiku leo TBC1 bila shaka mmeyaona.

Ndugu yangu Richard Ndassa alikikoroga, na mie sijapata kitu kabisa.

Kanuni na sheria zasemaje kuhusu hilo.

Wanasheria mtujuze
Mod;
Mwanzisha thread alitaka ku-draw an unnecessary attention kwa wana jukwaa kwa sababu anajua kuwa ni udaku, hivyo alidhani watu wata-ignore kuisoma.

Kwako totoz;
Mzee una bifu naye nini? Huko usukumani hata wachagga wapo kibao lakini wanaongea kisukuma utadhani ni wasukuma. Unless mtu anabisha, lakini the fact ni kwamba mgeni yeyote akishafika usukumani baada ya wiki moja anaongea kisukuma angalau to 60% accuracy. Hivyo, usukumani hakuna mtu mwenye haki ya kupiga kura huko, lakini hajui kisukuma. Huyo siyo mgombea uraisi kwamba ameongea kisukuma akiwa tarime, au kyela. Waacheni watu watambe kwenye maeneo yao ya kujidai, na pia siasa zetu zilenge zaidi katika kuwaangalia watu na siyo chama chao. Zitto hata akihamia UDP leo, Kigoma Kaskazini lazima wampe kura, wanamwangalia yeye sana, na si chama alichonancho! Usiwe unachukia watu halafu unatoa hoja ambayo haina upeo!
 
Back
Top Bottom