Revealed: Tanzanian Thieves have Sh315bn in Swiss Banks!

Watanzania kwa ndoto za mchana! Nani huyo anatakiwa ampe DCI Manumba amri ya kufungua police inquiry(PI)... hao hao wanufaika wa hizo account? Unapomtaja Ngeleja kama Ngeleja, unakosea sana kwani unasahau jambo moja muhimu...mfumo unaobariki/unaoruhusu mambo kama haya kutendeka. Je vijisenti vya Chenge vilirudishwa? Juzi hukushuhudia mfumo ukimwongezea majukumu na sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha bungeni na bado! Unacheza na CCM!

Sasa naona kuna haja ya kuwa mpambanaji active zaidi!,

Hospitali hazina maji wala umeme, shuka hazifuliwi na magodoro ni yale tuliyoyakuta mwaka 1961. Madakitari na waalimu wameamua kuwa walevi wa gongo kwasababu ya maisha magumu. Mbaya zaidi wanywa gongo wanafungwa wakati wale wa madawa ya kulevya wanashangiliwa! Mkulima ndio usiseme make huyu ndio ngazi ya kupandia, anakanyagwa kichwani. Analima kwa tabu sana halafu anazuwiwa kuuza!

Hivi hatujachoka hii hali?
 
Kwa mtindo huu vita ya ufisadi kweli ni ngumu mno! Mashaka yangu ni kama kweli PCCB wanaweza kuwakamata wahusika kama anavyosema mh. Hosea.

Ndugu yangu wee, ukiona wanavyotoa povu na kujiapiza utafikiri wanamaanisha......yaani nawachukia mno PCCB na kaka yao Beleshi..
 
At the same time, global pressure on Switzerland has been mounting, with demands that the country orders its banks to share information about clients with foreign governments.

Tanzania’s anti-corruption boss said Tanzania would need to establish from Switzerland who owns the money and if it happens it were money that has been illegally earned, he would consult the BoT on the immediate steps to take.

“After we have established where the money originated, we will follow due procedure and make sure it is returned home,” Dr Hoseah said, adding: “We shall use the relevant international law to sort this thing out.”

Recently, the Bank of Tanzania received over Sh72 billion as compensation for a dubitable military radar transaction under a settlement agreement between the government of Tanzania and British Aerospace Defence System Limited.

Over expenditure in the construction of the BoT twin towers is among scandals that have cost Tanzania billions in taxpayers’ money.

Dr. Hosea inabidi atueleze alikuwa wapi hadi nchi ikaporwa kiasi hicho na huyo gavana wa BOt ambaye kaweka vikwazo vya uhamishaji wa hela humu ndani kupitia mabenki yetu ilikuwaje hadi ikawa hivyo?

jibu ni kuwa fedha hizo zinapatikana kwa misamaha ya kodi..............na kupitishwa kama mali ghafi khalafu zikifika kule nje ndipo hubadilishwa na kuwa dola.......................lakini Mwenyezi Mungu aliweka wazi mwizi zake ni arobaini na sasa imefika.................
 
NADHANI mpaka sasa pesa hizo zitakuwa zimesha hamishwa kama serikali haitakuwa imefunga acc zao
 
Kama sio hii shida ya UDHAIFU, hizi zikichanganywa na zile za shimbo, tatizo la foleni Dar na Mgao wa umeme Tanzania kwishney! Tunahitaji kuweka kwenye mitaala yetu somo maalum la jinsi ya kuondokana na UDHAIFU na kufanya maamuzi magumu.
 
Mbunge-wa-Kigoma-Kaskazini-Kabwe-Zitto.jpg
Tuesday, 26 June 2012 21:38


Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni,Zitto Kabwe

ZITTO AMTAKA PINDA ATAJE WAHUSIKA, WANANCHI WATAKA FEDHA ZIREJESHWE, MABILIONI ZAIDI YAIBWA MTANDAONI
KUBAINIKA kwa Sh303.7 bilioni zilizofichwa katika akaunti za vigogo wa Serikali na wanasiasa nchini Uswisi, kumetikisa nchi huku shinikizo likitolewa kwa vyombo vya dola kuchunguza haraka na kuchukua hatua za kisheria, ikiwamo kurejesha fedha hizo.

Jana kutwa nzima, gazeti hili lilipokea simu kadhaa kutoka kwa wasomaji wake wakiwamo wabunge na mawaziri, huku baadhi wakichangia maoni kwenye tovuti na mtandao mbalimbali ya kijamii, wakitaka kujua majina ya wamiliki wa akaunti hizo.

Bungeni mjini Dodoma, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliitaka Serikali kuchunguza tuhuma hizo kisha kuwachukulia hatua watu sita wanaotajwa kwamba wanamiliki akaunti zenye mabilioni hayo ya shilingi chini Uswisi.

Fedha hizo zimebainishwa na ripoti ya Benki ya Taifa ya Uswisi (SNB), iliyotolewa hivi karibuni, ikitaja nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania, na kiwango cha fedha zilizohifadhiwa huko.

Tayari Kitengo cha Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kimeeleza kuwapo kwa fedha hizo katika benki mbalimbali nchini Uswisi, zilizoingizwa na kampuni za uchimbaji mafuta na madini.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nayo imeweka bayana kuwa inafuatilia suala hilo kwa mamlaka za Uswisi, ili kujua fedha hizo ziliko na nani anazimiliki.

Mbali ya Tanzania, nchi nyingine ambazo zina fedha nyingi katika benki za Uswisi ni Kenya (dola 857 milioni), Uganda (dola 159 milioni), Rwanda (dola 29.7 milioni) na Burundi dola 16.7 milioni.

Chanzo cha habari hizo, kilieleza kuwa tangu akaunti hizo zifunguliwe, wamiliki wake halali hawajawahi kuingiza hata shilingi moja.

Kauli ya Zitto

Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, aliliambia Bunge jana kuwa haiwezekani nchi ikaendelea ilhali watu wanakusanya fedha kutokana na utafiti wa gesi na mafuta, ambao bado haujaanza kulinufaisha Taifa.

Akichangia Bajeti ya Waziri Mkuu, Zitto alisema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) ielekezwe ili ifanye uchunguzi utakaowezesha wamiliki wa akaunti hizo kufahamika, ili wachukuliwe hatua mara moja bila kujali nafasi wanazozishikilia ndani ya Serikali.

“Viongozi wanaohamisha na kupeleka fedha za Watanzania nje ya nchi wanatakiwa wachukuliwe hatua mara moja. Hili litatusadia katika siku zijazo, kwani kama wapo wengine wanaodhani wanaweza kuficha fedha zao nje basi wajue kwamba popote watakapozipeleka tutazifuata na kuzirejesha,” alisema Zitto na kuongeza;

“Namuomba Waziri Mkuu aagize uchunguzi ufanyike, fedha hizi zirejeshwe na wahusika wachukuliwe hatua,” alisema Zitto.
Zitto alitoa kauli hiyo akiyanukuu magazeti ya Mwananchi, The Citizen na The East African ambayo kwa nyakati tofauti yameandika kuhusu kuwapo kwa kiasi kikubwa cha fedha zinazotokana na rushwa, ambazo zimehifadhiwa kwenye akaunti kadhaa nchini Uswisi.

Alisema kuachia suala hilo kuendelea ni hatari, kwani uchumi wa nchi utahujumiwa hata kabla ya miradi husika haijaanza kutekelezwa.

“Haiwezekani sisi tupo tunahangaika kutafuta gesi na mafuta huko baharini Lindi na Mtwara, halafu watu wengine tayari wameishawekewa hela kwenye akaunti, kwa hakika lazima uchunguzi ufanyike na watu hawa wajue kwamba Serikali ina uwezo wa kuwafahamu na kurejesha hizo fedha hizo nchini,” alisema Zitto.

Alitoa mfano wa Serikali ya India ambayo iliwahi kupata taarifa za baadhi ya watumishi wake kuficha fedha nchini Uswisi na kuchukua hatua za kiuchunguzi zilizowezesha wahusika kutajwa hadharani, kisha fedha zilizoibwa serikalini kurejeshwa.

Katika hatua nyingine, Zitto alitaka mvutano baina ya Tanzania Bara na Visiwani kuhusu masuala ya gesi umalizwe ili kuwezesha utafiti kuendelea kufanywa katika maeneo ya bahari ya Hindi.

Alisema utafiti katika baadhi ya maeneo hasa eneo la Bahari karibu na kisiwa cha Pemba umesimama kutokana na mvutano wa iwapo suala la mafuta ni la Muungano au la.

“Kama visiwani watavumbua gesi ni sawa, wavumbue kivyao, na sisi Tanzania bara tumeshavumbua matrilioni ya gesi, basi tuendelee kivyetu lakini tusisimamishe tafiti kutokana na mvutano usio na maslahi kwa nchi,” alisema.

Lowassa atoa kauli

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge Edward Lowassa, alisema jana kuwa kamati yake imesikia suala hilo kwenye vyombo vya habari na inajipanga kuzifanyia kazi taarifa hizo mara moja.

"Tumesikia kupitia vyombo vya habari na kama kamati tutahakikisha tunazifanyia kazi," alisema Lowassa alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano aliouitisha kuzungumzia safari ya kamati yake nje ya nchi.

Chadema yatoa tamko
Kwa upande wake, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeonya kuwa tatizo la ufisadi halitaisha nchini hadi pale Serikali itakapochukua hatua za dhati za kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu wote ambao wamehusika na ufisadi wa raslimali za nchi.

Chama hicho kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kutumia mamlaka yake ya kikatiba kuagiza kukamatwa kwa watuhumiwa wote wa ufisadi wa ununuzi wa rada na wale ambao wanatuhumiwa kuhifadhi Sh 303.7 bilioni nchini Uswisi.

“Chadema kinatambua kwamba kuachwa kwa mafisadi bila kuchukuliwa hatua kamili za kisheria na mali zao kufilisiwa, kunafanya taifa kuendelea na ufisadi ikiwemo ule wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Richmond na sasa tuhuma mpya za ufisadi wa shilingi bilioni 303 kwenye akaunti Uswisi,” ilisema Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, kupitia taarifa kwa
vyombo vya habari jana.
Wizi mwingie kupitia mtandao

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Pereira Ame Silima alilieleza Bunge jana kuwa hadi sasa kiasi kilichoripotiwa Polisi kuhusina na wizi kwa njia ya mtandao nchini ni Sh2.2 bilioni.
Fedha hizo ni zimegawanywa katika makundi matatu, Sh1.3 bilioni, Euro 8,897 (Sh17,660, 545) na dola 551,777 (Sh882,843,200).

Kauli hiyo ilitolewa wakati Waziri Silima akijibu swali la Hussein Mussa Mzee (Jang’ombe-CCM) aliyetaka kujua ni kiasi gani cha fedha kimeripotiwa Polisi kutokana na wizi kwa njia ya mtandao.
Mzee alihoji Serikali imejipanga vipi kudhibiti wizi wa mtandao, idadi ya waharifu wa wizi huo ambao wamekamatwa huku akitaka itungwe sheria maalumu kushughulikia wizi huo.
Silima alisema kuwa Serikali imetunga sheria inayoshughulikia uhalifu unaofanywa kwa njia ya mtandao, Electronic and Posta Communication Act, 2010 na sheria ya kudhibiti fedha haramu (The Anti – Money Laundering Act – 2006.

Aliongeza kuwa Serikali kupitia vyombo mbalimbali vya dola kama vile Polisi, taasisi za fedha, vyombo vya habari, TRA na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imejiwekea mikakati ya kuelimisha wananchi kuhusu aina ya uharifu wa kimtandao na jinsi ya kupambana nao.
Waziri alibainisha kuwa jeshi la Polisi limeanzisha Kitengo cha Makosa ya Kimtandao (Cyber Crime Unit) ambacho kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kinafanya kazi kubwa ya kupambana na majanga hayo.
Kilio cha wabunge

Wakati huohuo wabunge wameendelea kumbana Pinda huku baadhi yao wakikataa kuunga mkono hotuba yake hadi pale atakapojibu hoja walizotoa.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy akichangia hotuba ya hiyo jana, alisema vita dhidi ya ufisadi haiwezi kufanikiwa kwani vyombo vya husika wakiwamo Takukuru wanashindwa kuchukua hatua kwa makosa ambayo yako wazi.

Keissy alisema mafisadi na walarushwa nchini wanalindwa na Takukuru, kwani licha ya kuwapo kwa ushahidi na viashiria vya wazi, chombo hicho hakichukui hatua zozote.

Alisema, kama wapo watu wanaodiriki kuuza dawa ambazo zilipaswa kupelekwa katika hospitali na matokeo yake wagonjwa wanakufa, mtu huyo hana budi kunyongwa.

“Sheria za nchi hii zinawalinda wezi, ndiyo maana ufisadi hauwezi kuisha, mtu ana majengo makubwa leo, wakati ni jana tu amepata ubunge, amepata wapi utajiri huo wa haraka, aulizwe na akishindwa kutoa maelezo achukuliwe hatua,” alisema Keissy na kuongeza:

“Sasa la ajabu ni kwamba eti wanakwambia kwamba kama unamjua mla rushwa basi uwapelekee taarifa, kwani wao hawawaoni watu wanaotajirika haraka haraka?” alihoji.

Keissy ambaye aliipinga Bajeti ya Waziri Mkuu hadi pale atakapopewa majibu ya kuridhisha, alisema sheria za nchi hii ni dhaifu, ndiyo maana mafisadi wanaoiba mamilioni wanaendelea kudunda barabarani wakati mwizi anayeiba simu hupigwa na kuchomwa moto hadi kufa.

Mbunge huyo alisisitiza ujumbe wake, akisema kuwa, “hata ikitokea mafisadi hao wakafariki basi pingu ziwekwe juu ya makaburini yao.”

Naye Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Riziki Lulida alisema kuna njama zinazofanyika za kudhoofisha maendeleo mkoani Lindi kwa kuwapeleka viongozi wala rushwa katika mkoa huo.

Alisema, uduni wa mkoa huo unasababisha wapinzani kuufanya kuwa kichaka cha wapinzani, kuwadhalilisha na kuwasema kwamba wao ni maskini.

“Viongozi wengi wa halmashauri wanaofanya ubadhirifu wa fedha kutoka mikoa mingine hutupwa Lindi,” alisema Lulida kabla ya kuanza kuwataja kwa majina wafanyakazi hao wa halmashauri:

“Joachim Materu ameiba 577 milioni, akapelekwa Lindi, Eunice Maro ameiba 262 milioni na akapelekwa Lindi, baada ya kufanya wizi huo, Maro aliziweka katika akaunti inayoshukiwa kuwa ni ya rafiki yake, yenye akaunti namba 206660017 NMB ambaye alihamishiwa Ofisi ya Kilimo Lindi,” alisema.

Aliwataja wengine kuwa ni Macha anayetuhumiwa kuiba Sh6 bilioni ambaye amehamishiwa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na kwamba kuhamishwa kwao ni kusambaza ufisadi katika maeneo mengine.

Lulida aliongeza kuwa, kama Waziri Mkuu anataka aiunge mkono bajeti yake, basi aje na majibu sahihi kuhusu maendeleo mkoani Lindi pamoja na kurudisha programu ya kilimo ya Kanda ya Kusini, (SAGCOT)

Habari hii imeandaliwa na Neville Meena, Florence Majani na Habel Chidawali, Dodoma na Leone Bahati Dar

 
pesa za uswiss ni za JK!kila siku wanasema utafiti wa mafuta unaendelea kumbe wameshaanza kuyauza nje
 
TAKUKURU inangoja nini katika kuyaanika majina ya mafisadi hawa hadharani!?
 
Mikataba ya gesi, mafuta ipitiwe upya




Na Nyaronyo Kicheere - Imechapwa 25 July 2012

Waraka wa Wiki
Mwanahalisi




IMEZUKA staili moja siku hizi nchini ya kufikiri kwa kutumia kiungo fulani cha mwili badala ya kichwa. Aliyegundua kuwepo staili hii ingawa hajatangazwa kupewa Tuzo ya Nobeli ni meya wa jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi.
Kwa wasiomfahamu Masaburi, ni yule bwana mnene, mzito, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Dar es Salaam na mmiliki wa chuo cha manunuzi, mauzo na upangaji bei kilichopo Chanika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Kwa hiyo, mtu mwenye sifa kubwa na nyingi kama Masaburi ni muhimu na anayeijua sana serikali na chama tawala kwa vile yeye mwenyewe ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na katika serikali, hivyo anaposema staili ya kufikiri imebadilika lazima tukubali.

Akizungumzia matatizo ya utapeli, ufisadi na hujuma miongoni mwa watu fulani fulani kuingilia utaratibu wa ubinafsishaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Masaburi alisema tatizo la watu wengine ni kwamba wanatumia "nanihii" kufikiri!

Baada ya kutafakari sana hoja, mantiki na uzito wa maneno ya "poti" wangu Masaburi, nimekubali kuwa Watanzania wengi na hasa waliopo mjengoni wanafikiri kwa staili hii mpya ya "kimasaburisaburi".

Hebu fikiria kwa mfano, fedha nyingi zilizogunduliwa kufichwa Ughaibuni huko Uswisi; nimesikia kwamba fedha hizo zimefichwa kwenye mabenki ya mji mkuu Berne, mji mashuhuri kibiashara wa Zurick na mji wa utalii na starehe wa Geneva !

Taarifa ya kugundulika fedha hizo kufichwa nje ya nchi, tena wahusika wa kuficha pesa hizo wakitajwa kuwa maofisa sita, waliohusika kwa namna moja au nyingine na utoaji vibali vya kutafuta mafuta na gesi katika pwani ya Tanganyika , ziliibuliwa na Wakenya.

Magazeti ya Kenya – Daily Nation na The East African – ndiyo yaliyotoa taarifa za awali kabisa kuwa mabilioni ya dola yalikuwa yamefichwa katika mabenki ya Uswisi.
Japokuwa hata fedha za Kenya , Uganda , Rwanda na Burundi zimefichwa nchini Uswisi, hizi za Tanganyika ndizo zinatia uchungu zaidi kwa sababu matatizo yetu ni mengi kuliko ya wengine.

Magazeti ya Kenya yalieleza kuwa akaunti hizo sita zilifunguliwa na maofisa waliopo kwenye sekta ya gesi na mafuta na kwamba tangu walipofungua akaunti hizo mabwana hao hawakurudi tena kuongeza au kuweka senti yoyote.

Kilichowashangaza wachunguzi wa mambo ni kwamba akaunti hizo baada ya kufunguliwa na maofisa wa sekta ya nishati na madini wanaosimamia utafutaji gesi na mafuta nchini, ziliongezewa pesa na wageni tu hadi zikanenepa ‘kishenzi'.

Taarifa zilizopo zinasema waliokwenda kuzinenepesha akaunti hizo za maofisa wa Tanzania wa sekta ya gesi na mafuta ni maofisa wa kampuni za kigeni za mafuta na gesi!

Swali la kujiuliza ni kwa nini kampuni za mafuta na gesi ziliona haja ya kuwawekea wakubwa hawa mapesa kwenye akaunti zao? Wote tunajua hakuna cha bure duniani, sasa hawa wakubwa wa gesi na mafuta walifanya kazi gani kustahili pesa hizo?

Pia inaeleweka kwamba maofisa wa kampuni za mafuta wasingeweza kujua akaunti za wakubwa wetu hawa wa mafuta na gesi bila kukutana nao na kupeana akaunti hizo! Hii inaashiria yalikuwepo makubaliano kuwa "nyie kafungueni akaunti halafu tuwawekee…"

Ukifika hapo ndipo unakumbuka mchango wa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zito Kabwe alipolalamikia mikataba ya mgawanyo wa mapato baada ya mafuta au gesi kupatikana (Profit Sharing Agreement) inayoingiwa na maofisa wa Tanzania .

Zito alilalamika kwamba kampuni moja ya ya utafutaji mafuta na gesi imeingia mikataba na nchi mbili – Tanzania na Msumbiji, kwamba upande wa Msumbiji mkataba unataka nchi hiyo ipate asilimia 40 ya faida.

Lakini cha ajabu Zito anasema upande wa Tanzania mkataba unataka nchi kupata asilimia 10 tu ya faida! Kwamba kampuni hiyo hiyo moja, upande wa Tanzania tupate asilimia 10 lakini upande wa Msumbiji wao wapate asilimia 40!

Baada ya siri hii ya maofisa wa mafuta kuwekewa pesa kwenye akaunti zao za Ughaibuni ndipo tumeelewa kwa nini Tanzania ina mkataba mbovu wa kupata asilimia 10 tu wakati nchi nyingine zinapata asilimia 40 – rushwa, hongo, posho, zawadi walizopewa hawa.

Sasa hapa hatuna ujanja tena, dawa pekee ni kuvunjwa mikataba hii ya kitapeli na wakubwa hawa warejeshewe pesa yao waliyowawekea maofisa wetu wanaohusika na usimamizi wa sekta ya mafuta na gesi.

Yaani wao wawekewe mabilioni halafu kampuni za mafuta zichote hazina yote ya mafuta na gesi kwa miaka dahari hadi yatakapokauka? Mimi nasema mtu pekee anayetaka turejeshewe fedha hizi ni yule anayefikiri kimasaburi tu.

Yaani turejeshewe pesa hizo bilioni sijui ngapi halafu watoaji rushwa (kampuni za mafuta na gesi) ziendelee kuchota mafuta na gesi asilimia 90 na kutuachia kiduchu cha asilimia 10! Hapana, siyo wote tunaofikiri kimasaburi nasi wengine tuna vichwa na tunavitumia.

Mkataba haukufikiwa in good faith tunayo haki kuuvunja. Ushahidi wa bad faith upo. Ni hiyo rushwa iliyowekezwa Uswisi, tunaogopa nini? Kama kweli kampuni hizi zilijadili mikataba kwa nia njema, rushwa ya Uswisi ya nini?

Vijisenti vilivyokutwa Ughaibuni havikurudishwa na mhusika hakuchukuliwa hatua yoyote badala yake alipandishwa cheo kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu huko CCM makao makuu.

Safari hii hatutaki wala hatuombi CCM wachukue hatua. Tunachokiomba seriously ni kwamba mikataba ya gesi na mafuta irejewe kujadiliwa ili tupate haki kama inavyofanyika katika nchi nyingine kama vile Nigeria , Gabon , Cameroon , Congo ya Brazaville, Angola na hata Msumbiji.

Kwa nini sisi tu ndio tupate asilimia 10 wakati nchi nyingine zote nilizozitaja zinapata asilimia 40? Kwa hili naomba wote tuungane, tunaofikiri kikawaida na wale wanaofikiri kimasaburi, tuungane kudai haki yetu ya kupata asilimia 40 na siyo kudai eti kurudishwa pesa zilizofichwa nje ya nchi!
 
Kila jambo lina mwisho wake, walkiozea ubabe kwamba wanaongea tu maneno magumu mtaani, hiki ndicho kiamba. Tunaomba hiyo swiss judge summon's itumike fasta hayo manyang'au yarudishe hela zetu
 
Halafu waziri Mkuu anasema mchana kweupe kuwa maDC na maRC waendelee kupiga kampeni za ccm ili CCM iendelee kushinda!!!!!ishinde nini sasa? Inshashinda several times matokeo ndo haya!!!!kila siku wanalia sungura ni mdogo tugawane kidogokidogo kumbe wao wameficha mabillion huko uswiss....shame! Very shame!!!hata mtu mwenye akili timamu kushabikia ccm ni kitu cha ajabu sana ati!!!!walimu wanadai billion 54 tu ila huko uswiss mtu mmoja anamiliki zaidi ya hizo peke yake!!!!!kwenye mitandao ya kijamii wamejaa watu kuitetea ccm mwisho wa siku wanaliopwa makombo ya madolali yaliyoibwa....mlaaniwe wote mnaoishabikia ccm na viongozi wake wezi.....
Sometime you feel like crying but it does not make sense to them....very soon I will stop crying and something will follow...this can not go on forever....our time will come,yeah very soon!!
 
Na hawa wezi lini watapandishwa kizimbani!?au na wao walitoa mgao pale Ikulu?
 
Back
Top Bottom