Revealed!! CHADEMA ilitumia mitambo maalum ya DVR kurekodi mkutano wa tarehe 15/06/2013

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Wana JF,

Imethibitika kwamba technology ya mawasiliano hivi sasa imekua kwa kasi ya ajabu sana, kiasi chakufikia kuwa kumbe siyo lazima tutegemee camera za waandishi wa habari kuchukua matukio.

Ni kwamba Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kwenye mkutano wake wa mwisho licha ya kutumia setlite kurekodi mikutano yake, imethibitika kuwa chama hicho kilitumia mtambo maalum wa mawasiliano kurekodi mkutano wake wa mwisho katika uwanja wa soweto Arusha. Mtambo huo ambao unauwezo wa kurekodi matukio kwa masaa 72 mfululizo bila kuhitaji chaji, ulifungwa sehemu maalum ili kuweza kunasa matukio yaliyokuwa yanaendelea kwenye mkutano.

Mtambo huo ulisaidia kunasa tukio la mlipuko wa bomu na matumizi ya risasi kwenye mkutano kuwapiga raia, ambapo ulionyesha askari polisi aliyesimama pembeni ya nguzo ya umeme karibu na mfereji ulio mkabala na round about iliyo karibu na soweto garden akiwapiga risasi watu waliokuwa wanamkimbiza mtu aliyevaa suruali ya jeans aliyekimbia nakuingia kwenye gari ya polisi na kuondoka kwa kasi kwenye eneo la tukio. Mtambo pia uliweza kuonyesha gari ya blue landcruiser iliyoweza kui escort gari ambayo amepanda tule mtu aliyekuwa anakimbizwa.

Ule mtambo ambao una uwezo wa kurekodi matukio kwa around 360 degree angle uliweza kuonyesha tukio la watu wanaosadikiwa kuwa maaskari kufika kwenye eneo la tukio hasa kwenye gari la matangazo la chadema majira ya usiku, na kuweza kuzurura pale bila kuonyesha kwa kina walichokuwa wanakifanya pale.

video inaonyesha ule mtambo ulizima wenyewe saa moja na madakika asubuhi ya siku ya pili.

Kwa ujumla mtambo una taarifa nyeti za kuweza kusaidia kwa ushahidi wa tukio hili ambalo limegharimu maisha wa watu wasiokuwa na hatia. Muda utakapofika nadhani kwa idhini ya mwenyekiti wa chama kila kitu kitawekwa wazi.
Mungi kuna taarifa nilizopata leo, yule kijana askari polisi mwenyeji wa Songea aliyekuwa amepangiwa kikazi Morogoro aliyerusha bomu kwenye mkutano, ameshauawa na waliomtuma kwa vile alionekana kwenye tukio lile! Wanafuta ushahidi! Bado nafuatilia.
 
Ukweli upo na utafahamika bila chembe ya ujanja.

Ukweli huchelewa tu, lakini hutokea baadaye kama bibi harusi anayesubiriwa.

Nikimwangalia machoni Mbowe, hasa kwa matukio haya ya Arusha naona hazina kuu ya ukweli, upendo, ushujaa, uzalendo na utu!
 
You can fool some people sometimes but you can't fool all the people all the time. Siilaumu ccm, Polisi wala mwigulu nawalaumu watanzania kwa ubinafsi, kila mtu Ana u Mimi woga na mabingwa wa kulalamika Mpaka wa Mwisho kuuliwa na nyie viongozi wa chadema Kama hampendi rife Mbona hamsimamii matamko yenu? Yale maandamano ya nchi nzima yaliishia wapi? Mna boa sana saa nyingine kwa woga wenu.

CC DR. W. Slas
Bcc Mbowe
 
Back
Top Bottom