Safi sana. Hili ni jambo la kupongeza ingawa maamuzi haya yamechelewa sana. Uganda waliliona hili siku nyingi na wanalo jengo lao New York tena pembeni ya Jengo la Ubalozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa opposite na UN. Nigeria pia wanalo na wengine wengi. Itafaa sana kama Serikali itanunua pia majengo katika miji ya Paris na Geneva ili kupunguza mzigo mkubwa wa gharama za kupanga. Maamuzi haya na utekelezaji ungefanyika miaka 20 iliyopita Serikali ingekuwa imeokoa mamilioni ya shilingi.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanunua jenglo la East Side, New York, kwa dola milioni 24.5 za kimarekani

Oktoba 13, 2011 04:30PM

Na Katherine Clarke
The Real Deal (The Real Deal | New York Real Estate News)

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imenunua jengo maarufu linalojulikana kama The Timekeeper Building, ambalo lina urefu wa ghorofa sita, linalotumika kwa upangishaji wa ofisi, lenye anuani ya 307 East 53rd Street, ambalo lipo jirani na makao makuu ya Umoja wa Mataifa (United Nations), kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 24.5, sawa na Shilingi 44,100,000,000 za Kitanzania, kwa mujibu wa kumbukumbu za umma zilizosajiliwa kwenye nyaraka za Jiji hapa New York, Oktoba 13, 2011.

Jengo hilo lenye ujazo wa mraba wa futi 40,000, lenye ghorofa sita, lililopo kati ya Mtaa wa Kwanza na Mtaa wa Pili, lilitangazwa kuuzwa na kuwekwa sokoni na kampuni ya uwekezaji wa majengo iliyopo Philadelphia, Pennsylvania, Amerimar Enterprises mnamo Septemba 2010. Robert Garrish, Paul Gillen na Darcy Stacom wamiliki wa kampuni ya udalali wa majengo na nyumba ya CB Richard Ellis ya New York ilipewa zabuni ya kulitafutia soko jengo hilo.

Mnamo mwaka 2005 Amerimar ilinunua jengo hilo kutoka kwa kampuni ijulikanayo kwa jina la Mittman Associates kwa gharama za dola za Kimarekani milioni 15.45.

Wakati jengo lilipowekwa sokoni na kutangazwa kuuzwa, wapangaji wake walikuwa Amerimar pamoja na Bombo Sports and Entertainment, kampuni ya kusambaza mvinyo ya Frederick Wildman & Sons pamoja na Caudalie Vinotherapy Spa.

Mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuweza kupatikana ili kuweza kutoa tamko kuhusu ununuzi huo, hata hivyo, mtu aliyepokea simu iliyopigwa kwenye ubalozi wa Tanzania jijini Washington, D.C., alithibitisha kwamba ubalozi wa nchi hiyo uliopo New York huenda ukahama kutoka mahali ulipo hivi sasa, yaani anuani ya 201 East 42nd Street.
Mwakilishi wa Amerimar hakuweza kujibu simu iliyopigwa ofisini kwake wakati tukienda mtamboni. Garrish, Gillen na Stacom walikataa kuzungumzia kazi waliyoifanya kuhusu ununuzi huo.

Ununuzi huu unaweka kumbukumbu ya ununuzi wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miezi chache iliyopita. Kama ilivyoripotiwa hapo awali, ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo New York, ulinunua nyumba iliyopo mjini Great Neck, Long Island, maarufu kama colonial house kwa bei ya dola za Kimarekani 1.26 milioni, sawa na Shilingi 2,268,000,000 za Kitanzania. Orly Hollander wa kampuni ya Laffey Fine Homes, ambaye alikuwa wakala wa nyumba hiyo wakati ilipokuwa sokoni, amekaririwa akisema kwamba kwa wakati huu, nyumba hiyo inatumika kwa makazi ya ofisa wa kibalozi wa Tanzania pamoja na watoto wake.

Maelezo ya picha (Kutoka kushoto, Darcy Stacom, Makamu wa Rais wa CB Richard Ellis, kampuni ya udalali wa nyumba iliyopewa kazi ya kutafuta wateja kwa jengo hilo lililopo 307 East 53rd Street, New York, na bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa imesimamishwa nje ya jengo lililonunuliwa.)

Republic of Tanzania purchases East Side building for $24.5M | The Real Deal | New York Real Estate News