Reli ya Bendera Tatu Bandari Street BP Puma Ing'olewe

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Kwa wakazi na washaija watumiao Bandari Street, ile barabara ya kutokea Gerezani Ilala mpaka mzunguruko wa barabara ya Bandari na ya Kilwa, aghalabu pana foleni ndefu inayosababishwa na reli zinazokatiza barabara pale usawa wa matangi ya BP / Puma.

Vipande hivyo vya reli ving'olewe kwa vile vinazorotesha uchumi wa taifa kwa kupotezesha muda mwingi kwa magari makubwa yasafirishayo mafuta, na kwa yale yaendayo bandarini na barabara ya Kilwa (Kilwa Road), na hata kwa magari madogo.

Inavyoonekana, treni zilishaacha kupita hapo siku mingi, na sasa reli imebaki kama historia.

Ni wazi pana ujenzi wa barabara ya mwendokasi unaendelea, ila hili likifanyika kabla ya yote, itapendeza.


(picha zote zimetoholewa kutoka kwenye ramani za Google na washirika wake.)
ReliBandariStreetImage.png ReliBandariStreet.png

Kama nyongeza, barabara ya Mafuta (Mafuta Road) nayo ikiwekewa lami itapendeza.
 
NYONGEZA: Sehemu hii korofi imerekebishwa kwa kujazwa kifusi. Japo reli hazijatolewa, ujazaji kifusi umekuwa wa mafanikio kwa kupunguza foleni kwa kiwango kikubwa. Kongole kwa wahusika wote.
 
Back
Top Bottom