Reli hii itakuwa mkombozi kiuchumi wa nchi hizo tatu za Afrika Mashariki

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Reli hii hakika itakuwa mkombozi wetu kiuchumi Thursday, 17 March 2011 20:18
kikweteutabiri.jpg

Jakaya Kikwete

RAIS Jakaya Kikwete jana alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Wawekezaji wa Reli inayotazamiwa kujengwa kutoka Dar es Salaam kwenda Kigali, nchini Rwanda na Keza hadi Musongati, nchini Burundi. Mradi huo utagharimu kati ya Sh5.2 trilioni na Sh7.6 trilioni.

Kongamano hilo lililohudhuriwa na mabalozi wa nchi wahisani, mawaziri wanaosimamia masuala ya usafiri wa reli nchini Tanzania, Rwanda na Burundi na wawakilishi wa benki za biashara za ndani na nchi za nje, lilijadili jinsi ya kupata fedha za ujenzi wa reli hiyo inayotegemewa kusafirisha tani milioni 35 ifikapo mwaka 2030. Inatia moyo kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), tayari imetoa Sh18 bilioni kwa ajili ya upembuzi yakinifu wa mradi huo.

Hapana shaka kuwa reli hiyo ikikamilika itakuwa chachu kubwa ya maendeleo na mkombozi kiuchumi wa nchi hizo tatu za Afrika Mashariki. Pengine wakati tukifurahia ujio wa mradi huo wa reli na kuzungumzia maendeleo ambayo nchi zetu hizo zitapata kutokana na kusafirisha mizigo na abiria kwa kutumia reli hiyo, ingekuwa vyema tujiulize kwa nini imechukua muda mrefu kiasi hicho kabla ya viongozi wetu kubuni mradi huo.
Hii ni kutokana na ukweli kuwa nchi wahisani zilikuwa tayari kuufadhili siku nyingi tu na nchi zetu zilikuwa na uwezo wa kuunganisha nguvu na kupata fedha za mradi.

Imetolewa hoja na baadhi ya watu kwamba mradi kama huo usingewezekana siku za nyuma kwa sababu Rwanda na Burundi zilikuwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Lakini tunadhani kuwa tatizo hasa halikutokana na vita, bali lilitokana na viongozi wetu kukosa ubunifu pamoja na kushindwa kuvua mbeleko za ukoloni mamboleo, Tanzania ikiwa imetawaliwa na Uingereza na Rwanda na Burundi zikiwa na uchovu uliotokana na utawala wa Ubelgiji.

Siyo siri kwamba, ingawa Rwanda ilipata uhuru mwaka 1960 ikifuatiwa na Burundi mwaka 1962, nchi mbili hizo zilikuwa hazina vita katika miongo mitatu ya kwanza baada ya kupata uhuru kutoka Ubelgiji.
Rwanda ilikumbwa na vita mwaka 1990 hadi 1994 yalipotokea mauaji ya kimbali na Burundi ilikumbwa na vita mwaka 1992. Tanzania imekuwa na amani wakati wote tangu ipate uhuru 1961.

Tunachojaribu kusema hapa ni kwamba viongozi wengi katika Bara la Afrika wamechelewa sana kutambua umuhimu wa usafiri wa reli katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo. Tuangalie jinsi viongozi wa Tanzania na Zambia walivyoitelekeza Reli ya Tazara (mashuhuri kama Reli ya Uhuru), hadi ikafikia katika hali ya kusikitisha iliyomo hivi sasa.

Viongozi wenye dira na mwelekeo wangehakikisha reli hiyo inapasua kupitia Zambia na kutokezea Bahari ya Atlantic kupitia Angola. Leo hii bidhaa za Afrika Mashariki zingekuwa zinafika Bara la Amerika kwa gharama ndogo mno.

Tunataka viongozi wetu watambue kuwa usafiri wa reli katika nchi yetu ndilo jibu pekee kwa changamoto nyingi za usafiri zinazotukabili. Licha ya usafiri huo kuwa wa gharama ndogo sana, husafirisha abiria wengi na mizigo mingi mizito kwa mara moja. Nchi nyingi duniani hutumia reli, badala ya barabara kusafirisha mizigo mizito kwani, kama tunavyoshuhudia uharibifu wa barabara zetu kwa kiasi kikubwa unatokana na sababu hiyo.

Tunapendekeza kuwa Serikali isifanye mzaha kwa ujenzi wa reli hii. Inawezekana kabisa kuwa inaweza kuua ndege wawili kwa jiwe moja, kwa maana ya kuhakikisha kuwa reli hii ikifika Isaka, Shinyanga, Serikali inaunganisha reli ili ifike mjini Mwanza.

Kwa kufanya hivyo, hata bei za bidhaa kama sementi, sukari, vifaa vya ujenzi na kadhalika zitapungua kwa kiasi kikubwa. Serikali itafute wawekezaji ili zijengwe reli nyingine kwenda katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha na pia iangalie uwezekano wa kuijenga katika mikoa mingine, hasa ya kusini.
 
Mama yangu, ina maana malori yangu yatakosa biashara, nafwa!!!!!! watoto wangu hawataenda shule. I cant imagine kabisa, no no no no way, haiwezekani kabisa????
 
wameshindwa kuboresha reli ya kati c inafika mpk kigoma au inaruka ikifika tabora na kigoma imepakana na wapi kama c unafik na wahudhuriaji na hawana mambo ya kufanya, na et itakua mkoboz wa uchumi mbona tunayo ya TAZARA na tupo pale pale kikubwa reli inazid kufa tu wakati imeunganishwa mpk south kwa upande wa zambia
 
Huyo Mheshimiwa ni mnafiki, alipo ingia madarakani reli ya Moshi Arusha likuwa inafanya kazi, lakini sasa nenda kaangalie imeota nyasi an kutu. Nadhani hata ya Dar -Kologwe- Tanga -Moshi sidhani kama ziko salama. Atengeneze kwanza hizi za ndani aweze kurukia nje!!!!!!!!
 
Tatizo la tanzania ni NATO maana yake NO ACTION TALK ONLY, maneno mengi vitendo hakuna. Wakati reli yetu tumewapa rites miaka mitano hakuna kilichofanyika railway stations zimekuwa magofu, staff houses wameuza sijui atakayeendesha hiyo reli atakaa kwenye hema? Mizigo ipo mingi ukiliza kwa nini inasafirishwa kwa barabara huwezi jibiwa.

Leo watu eti wanafanya semina kudiscus hicho kitu.

Tunachekesha kweli
 
In time limit au ndo itatake forever? hii reli tangu enzi za mwalimu imekuwa ikizungumzwa pamoja na umeme kutoka maporomokoya ya maji Rusumo lakini utekelezaji wake hola! Mwanzoni walisema itaanzia Isaka leo hii twaambiwa itaanzia Dar, which is which jamani?
 
JK ni ahadi tupu. Hiyo ni ahadi ya 69! Rwanda na Burundi wanaweza lakini Tz labda chini ya uongozi wa Rais mwingine siyo JK.
 
baada kupata KIKOMBE toka kwa babu naona mkwere kapata nguvu sasa ahadi kemkem zinaendelea hatuoni chochote cha maana.
 
Huyo Mheshimiwa ni mnafiki, alipo ingia madarakani reli ya Moshi Arusha likuwa inafanya kazi, lakini sasa nenda kaangalie imeota nyasi an kutu. Nadhani hata ya Dar -Kologwe- Tanga -Moshi sidhani kama ziko salama. Atengeneze kwanza hizi za ndani aweze kurukia nje!!!!!!!!

kweli aisee. Angeanza na zilizopo.
 
Reli hiyo haitakuwa na maana yeyote iwapo bandari ya Dsm haitaboreshwa na kufanya kazi bila ya ukiritimba.
 
Back
Top Bottom