Regia Mtema is No More!

Status
Not open for further replies.
Nachukua nafasi hii kwa masikitiko makubwa kutoa rambirambi zangu kwa wazazi, ndugu, jamaa, viongozi wa CDM, wanachadema wote na wanaJF wote kwa ujumla. She was lovely, she was unavoidable.
 
Wema hawana maisha na mbuzi wa masikini hazai. Bwana alitoa na Bwana ametwa, jina la Bwana libarikiwe.
 
Poleni familia kwa ujumla,poleni wapendamaendeleo wote. Tumempoteza dada yetu mpendwa Regia Mtema mpigania haki wa kweli,tumepata pengo kubwa sana. Lakini Mungu ni mkuu, hivyo tunamwomba atusaidie ktk haya majonzi.
 
[h=6]TANZIA!

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepatwa na majonzi makubwa na kinasikitika sana kwa kifo cha Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Taifa, Mheshimiwa Regia Mtema ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira. Mheshimiwa Regia Mtema amefariki leo tarehe 14 Januari 2011 kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu darajani.

Katika uhai wake marehemu Regia Mtema amefanya kazi mbalimbali za kisiasa na kijamii katika taifa. Marehemu Regia Mtema amezaliwa tarehe 21 mwezi Aprili mwaka 1980 na kusoma shule za sekondari kidato cha kwanza mpaka cha sita katika shule ya sekondari ya Forodhani na Shule ya Wasichana ya Sekondari ya Machame. Marehemu Regia Mtema alipata shahada yake ya kwanza (Bsc Home Economics and Human Nutrition) katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

Mara baada ya kuhitimu masomo yake marehemu Regia Mtema alifanya kazi katika taasisi mbalimbali kabla ya kujiunga na CHADEMA na kuteuliwa kuwa Afisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Vijana ya CHADEMA na baadaye kuteuliwa kuwa Afisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Mafunzo ya CHADEMA nafasi ambayo aliishikilia hadi mwaka 2010 alipoteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum.

Viongozi wakuu wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Katibu Mkuu Dr. Wilbroad Slaa, wajumbe wa kamati kuu, wakurugenzi wa chama makao makuu na wabunge wamejumuika hivi sasa na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu.

CHADEMA inatoa pole kwa familia ya marehemu Regia Mtema, wanachama wote na wananchi wa Mkoa wa Morogoro hususani wa Jimbo la Kilombero kutokana na msiba huu wa ghafla katika wakati ambapo mchango wake ukihitajika kwa chama na kwa taifa.

Taarifa zaidi kuhusu taratibu za maziko, itatolewa mara baada ya kukamilisha majadiliano baina ya familia ya marehemu, chama na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mipango ya mazishi ya marehemu inapangwa nyumbani kwa Baba wa Marehemu Regia Mtema, Ndugu Estelatus Mtema, Tabata Chang'ombe. Ratiba ya maziko itatolewa baada ya kukamilika kwa taratibu zinazopangwa na familia ya marehemu, Ofisi ya Bunge na chama.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Regia Mtema, mahali pema peponi. Amina.

Imetolewa na:

John Mnyika(Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
[/h]
 
Poleni CHADEMA, Poleni wana familia na pole kwa vijana wote wa Tanzania ambao Regia alikuwa msitari wa mbele kuwatetea. Nasikitika kuwa kifo hiki kimetokea akiwa barabarani akiendela na shughuli za mapambano ya kupigania haki za watanzania.

May god rest her soul in peace ............. AMEN!
 
Eeeh Regia ..nenda..enenda!!! Hapa Duniani si mahala salama,chuki,fitna ,nyodo, vita, vitisho nk vimetanda kila sehemu ya dunia hii, wote ni wasafiri, tuwekee makao huko uliko kwani umependwa zaidi ya mwanadamu yeyote!! Ni ngumu kumeza lakini kwa Jina lla Bwana tumeamini na tutazidi kukupenda na kukumbuka!! Ulale Salama!!
 
Wakuu poleni kwa msiba nina swali kwa wanaomfahamu Dada Regia magazeti ya leo yametoa picha ya Kamanda Regia ana mguu mmoja tena anatembea kwa msaada wa fimbo hii picha ilipigwa baada ya ajali alikuwa na mguu mmoja kabla ya ajali ?.Kama alikuwa na mguu mmoja aliwezaje kuendesha gari au gari lake ni maalumu.
 
Hakika ni muswiba mkubwa sana sio kwa familia yake bali pia kwa Tz na w Tz wote, Chadema na wanachadema wote, Bunge na wabunge wote lakini pia wana JF wote na wananchi wote kwa kumpoteza mwenzetu kipenzi chetu.

Hakika Mola ametoa kisha ametwaa, jina lake lihimidiwe,

Kazi ya Mola haina makosa.
 
Wakuu poleni kwa msiba nina swali kwa wanaomfahamu Dada Regia magazeti ya leo yametoa picha ya Kamanda Regia ana mguu mmoja tena anatembea kwa msaada wa fimbo hii picha ilipigwa baada ya ajali alikuwa na mguu mmoja kabla ya ajali ?.Kama alikuwa na mguu mmoja aliwezaje kuendesha gari au gari lake ni maalumu.
Mh.Mtema alikua mlemavu na gari ilikua ya kawaida sio maalumu kwa walemavu.Kifo cha Huyu dada kimenishtua na kunisikitisha sana,she was so lovely.Mwenyezi Mungu awe pamoja nasi katika msiba huu,poleni ndugu , na marafiki.
 
RIP Regia..........Umetangulia.....sisi..........tunakuja.........na wana JF wote tutakuja.......Mungu akurehemu
 
pole sana familia mungu awape moyo wa amani na uvumilivu na mungu aiweke mahala pema peponi roho yake kwa jina la Yesu Ameen.
 
Utaratibu mzima wa michango ya wana JF uwekwe mwanzoni mwa thread kuliko watu kuuulizauliza maswali. Baada ya maelezo weka Directives ya jinsi ya kuchangia rambirambi..kushiriki msibani........na kupata T shirt. Sasa mpaka mtu apekue page karibia 45 kupata utaratibu ndo nini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom