Red Brigade: Kikundi cha mauaji, watekaji, wamwagia sumu na "nchi kutotawalika"

Status
Not open for further replies.
Mh Mwigulu. Nimekukubali wewe ni mzushi wa historia. Unakariri kuwa shilingi ya Tanzania ni sawa na ya Kenya, kwamba Dollar ya USA ni sawa na ile ya Zimbabwe. Kikundi siyo jina lake, bali ni matendo yake. Hivi nikikwambia kuwa kuliwahi kuwa na kichaa anaitwa Mwigulu utasema ndo maana uliitwa jina lake? Ok tuache porojo sana, hebu nipe michapo na historia kuhusu GREEN GUARD.
1044947_10201565346164177_1796414905_n.jpg
 
CHADEMA walifanya makosa sana kuita kikosi chao cha ulinzi Redbrigades wakati wanafahamu tuko kwenye ulimwengu wa political correctness.

Ni rahisi sana kusema hili ni jina tu lakini katika ulimwengu huu, jina ni zaidi ya jina tu ikichukuliwa pia jina ni utambulisho.

Huwezi kumuita mwanao Hitler au jina lolote linalohusika na matendo ya kishetani hata kama matendo yake yatakuwa siyo ya kishetani na ndiyo maana ni nadra sana kusikia mtu anaitwa Hitler.

Ndiyo maana hata waumini wa dini wanapewa majina ya maraika, mitume na wafuasi wa Mungu au watu ambao matendo yao yalikuwa siyo ya kishetani. Hii haitokei by coincedence bali kuna sababu zake ambazo mojawapo ni hii (political correctness).

Hili jina litawasumbua sana kisiasa huko mbele ya safari.
umri wangu ni miaka 54 nimeona mengi duniani,kwa jinsi ccm inavyofanya nipo tayari kujiunga na red brigade hata leo huu uonevu hauvumiliki,CDM ni haki kujilinda,
 
umri wangu ni miaka 54 nimeona mengi duniani,kwa jinsi ccm inavyofanya nipo tayari kujiunga na red brigade hata leo huu uonevu hauvumiliki,CDM ni haki kujilinda,
Ni kweli CHADEMA wana haki kujilinda kama ilivyo kwa kila raia mpenda amani.

Hoja yangu ni kwenye jina la kikundi hiki cha ulinzi na siyo kwenye malengo na madhumuni ya kuwepo kwake nchini.
 
Najiandaa kuwapa CDM plan ya ku execute mafunzo...bila kificho na bila Jeshi wala Usalama kujua...tena hadharani.Na hakuna wa kumshika bila kuchokoza raia.
 
I cant believe umeamua chuku abendera yako ya china ukaamua wabambika CDM..yaani mwigulu hii habari ni ya kitoto sana km visa ya Sheikh yahaya na ilm yake ya nyota.Stori ya kitoto.

Naona umeamua ongea your mind..Aisee.
 
Paw, Invisible, naomba mwongozo.

Katika thread yenu Topic gani hufungwa au kufutwa kabisa JF?


Vifungu vifuatavyo

3. Kuleta makala au kuendeleza mijadala yenye kuleta ugomvi, uchochezi na yenye muelekeo wa kutengenishana badala ya kuungana miongoni mwa wajumbe wa JAMII FORUMS na Watanzania wote kwa ujumla.

6. Kutoa maelezo au shutuma dhidi ya mwanachama mwenzako, kiongozi wa au watu wenye hadhi kijamii bila kuwa na ushahidi wa kutosha kwa lengo la kuchafua rekodi safi ya mhusika kijamii.


17 - Questionable Content:

Since we can't have a rule to cover everything, this is the rule to, well, cover everything. These are public boards, so act like you would if you were in a public place. These issues are left to the discretion of the individual moderators, but may include any material that is knowingly false and or defamatory, misleading, inaccurate, abusive, vulgar, hateful, harassing, obscene, profane, sexually oriented, threatening, invasive of a person's privacy, that otherwise violates any law, or that encourages conduct constituting a criminal offense.

Na tukizingatia uhalisia wa majibu aliyopewa Mwigulu na wachangiaji mbalimbali yakionesha kabisa kwamba ameanzisha uzi huu kwa propaganda, kwa ajili ya kumchafua Dr. Slaa na Chadema.


  • [*=1]Kuhusisha masomo ya Dr. Slaa Roma na Red Brigade, wakati hata Chadema wala mfumo wa vyama vingi haujaanzishwa (Late 1970s to Early 1980s).


  • [*=1]Kupotosha makusudi, kuonesha Chuo Kikuu cha Trento ni jirani na Roma wakati viko umbali wa km. 360.


  • [*=1]Kuhusisha mauaji yanayofanywa na polisi na chama cha Chadema, wakati uchunguzi huru haujafanyika, na Rais wetu ambaye pia ni kiongozi mkuu wa CCM amekataa kuunda uchunguzi huru.


  • [*=1]Kupotosha makusudi kuwa kufanya maandamano ni fujo, huku akijua kuwa katiba yetu ya Tanzania imeruhusu
​Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania toleleo la 1977


  • [*=1]Kwamba haya aliyoandika ni madai na shutuma nzito ambazo zinapaswa kupelekwa kisheria na kujadiliwa kwa weledi, na si kipropaganda kama afanyavyo hapa, na kwamba matokeo yake ni mabaya sana kwa jamii yetu? Iwapo kuna ukweli katika hayo anayoandika hoja yenye mashiko ni kufuta chama, na si kukipa chama nafasi ya kupigiwa kura na wananchi na kuwatisha wananchi eti cha kihalifu.

Moderators wetu wapendwa Paw, Invisible, ninyi wenyewe mmetuandikia

Naomba mwongozo wenu moderators
Mkuu kuwa na moyo wa kutafiti mambo umeanza kuomba huruma ya mwamuzi kwa kutaka upewe penati mapema hivi,

Hili ni dalili ya kukosa hoja na kuanza kutapatapa kama mfa maji,

binafsi sikutegemea kama watu wazima mnaweza kuishiwa hoja kiasi hicho mpaka kuomba penati kwa waamuzi,

kwa mtindo huu chadema mtapata shida sana make mda ni mwingi na mmeanza kutapatatapa mnono lazima mtafutane.
 
Wewe HAMY-D huwa unafikili kwa kutumia nini? jina linauhusiano gani na maneno unayo ongea? RED BRIGADE haijaanza kazi hizo sifa unazoipa zinatoka wapi?, unatabili au we ni mganga wa kienyeji? si lazima uandike humu kilasiku au tatizo ujira wa buku 7
 
Wewe HAMY-D huwa unafikili kwa kutumia nini? jina linauhusiano gani na maneno unayo ongea? RED BRIGADE haijaanza kazi hizo sifa unazoipa zinatoka wapi?, unatabili au we ni mganga wa kienyeji? si lazima uandike humu kilasiku au tatizo ujira wa buku 7

ID yako ina akisi maneno yako!

Naona umeporomosha maneno yasiyo na tija kabisa, labda nikusaidie tu, Mbowe kasema wana kiimarisha kikosi cha Red Brigade kwa kuwa hawaoni tija ya uwepo wa polisi kwenye kulinda usalama.

Lakini Dr Slaa anajua fika kuwa kikundi cha Red Brigade ni kikundi cha waasi, na mbaya zaidi bado vikundi vya waasi hawa vipo. Sasa kwa akili yako unadhani haileti shaka kwa serikali na raia juu ya mafunzo yanayo tarajiwa kufanywa?
 
Chadema imetikisa Tanzania kwa kauli yake ya kuimarisha ukakamavu wa vijana wa chama ili kuwa na uwezo wa kutoa ulinzi makini, wakisayansi na wa dhati kwa mali, viongozi, wanachama na wapenzi wa Chadema. Watanzania wanalipa kodi ili ziweze kuendesha serikali kwa kulipa mishahara wafanyakazi wa umma kulinda na kuhakikisha jamii nzima inapata haki ya msingi ya kuishi. Ni wajibu na kazi ya msingi ya jeshi la polisi, usalama wataifa na majeshi yetu kuhakikisha raia wote wanapata haki ya ulinzi, kuishi, kuheshimiwa na kupewa hifadi stahiki.

Vile vile ni wajibu wao kukomesha uhalifu kwa kukamata, na kufikisha kwenye vyombo vya kisheria wote wanaovunja sharia bila kujali sura cheo, fedha au ubaguzi wa aina yeyote. Ni ajabu leo serikali chini ya utwala wa JK Raisi wa nchi kushangaa kwanini wananchi hawaamini tena jeshi la polisi na serikali yake. Haingii akilini kwanini serikali ya JK inapata kigugumizi kuunda tume ya kimahakama kuchunguza vifo vyote vilivyotokea kwenye mikutano ya chadema ambayo chadema wameomba serikali ifanye hivyo ili kila atakayebainika ni chanzo cha mauaji yale ashitakiwa na aende jela.

Ni CDM wanaoishinikiza serikali ifanye hivyo ila ni serikali inayokataa na kumwaelekeza Mwigulu kupanda majukwaani na kushambulia CDM kwa maneno ya kejeli na matusi. Ni serikali hii hii ya JK kwa kutumia jeshi la polisi, inashutumiwa kurusha bomu kufyatua risasi na kuuuwa raia mjini arusha. Ni polisi hawa hawa chini ya maelekezo ya serikali ya JK walimshambulia mwangosi kwa bomu la machozi na kumwua. Ni askari hawa hawa chini ya uraisi wa JK waliuwa watu wawili Arusha kwa risasi bila kuulizwa. Matukio haya pamoja na yale ya Igunga, morogoro, Mwanza, Karatu, Tarime, Mbeya, Mtwara,ndago na sehemu nyingi za ambapo mauaji yenye sura za kisiasa yametokea Chadema wameomba tume ya kimahaka iundwe ila serikali imekataa kata kata.

Ni nini maana ya tume ya kimahakama , ni tume ambayo wote wale watakaobainika na hatia lazima wafikishwe kwenye vyombo vya sharia na hakuna anayeweza kuzuia. CCM na serikali yake wanaogopa kwani ndio wahusika wakuu. Wananchi wengi leo wanagharama kubwa sana za kuishi kwa amani kwa kuajiri walinzi wa milangoni, makampuni ya ulinzi ya kujitegema nk kwani polisi wameonekana hawana msaada wowote kwa ulinzi wa jamii. Tamko la CDM chini ya mwenyekiti wa Taifa ni kwamba baada ya jitihada zote za kuripoti matukio yote ya kihalifu pamoja na yale yenye ushahidi wa wazi kuripotiwa polisi bado polisi wamegoma kutoa ulinzi, kuchunguza na kukamata wahalifu, kinachotokea ni wafuasi na viongozi wa CDM kendelea kuuwawa na kukamatwa bila hatia. Muda umefika wa kujilinda dhidi ya wauaji ambao kwa ushahidi wa mazingira ni ma-agent wa serikali ya chama cha mapinduzi kwa woga wa kushindwa chaguzi mbali mbali hasa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Ujumbe muhimu JK anatakiwa aupate ni huu hakuna serikali yeyote ile duniani imeweza kuendela kukaa madarakani kwa kuuwa wananchi, kuwatesa, kuwatoa kucha, kuwateka na kuwashambulia kwa mabomu. Serikali ya ajabu tu ndio itafanya hivyo. Leo hakuna mkoa wa TZ ambapo polisi na JWTZ hawajauwa wananchi, kubaka, kupiga, kuiba, kudhuru mali, miili ya akina mama, watoto, na wazee.

Hasira hii ipo nchi nzima sio Mwanza, Mbeya, Mtwara, Bumbuli, Iringa, Kyela, Mwandinga, NK kila mahali kuna vilio vya mateso ya polisi chini ya maelekezo ya serikali ya CCM bila onyo wala karipio. Kuonyesha serikali inahusika moja kwa moja waziri mkuu alibariki mauaji na mateso ya polisi dhidi ya Raia. Sasa Raia wanataka kujilinda dhidi ya serikali iliyoamuru raia wauwawe. Hakuna atakayekubali kuona kizazi chake kinateswa na kunyanyaswa daima. Stop has been made.

Umetoa tuhuma nyingi kwa serikali ambazo hazina mashiko kwani ni uzushi mtupu.

Pia umesema suala la kauli za Mwigulu, hivi ulishawahi kusikia kauli hii "nchi haitatawalika?" hii je, "Ikulu tutaenda hata kwa kumwaga damu", vipi hii "hata tukiuwawa hakuna kurudi nyuma" lakini kuna hii "Kikwete ni muasisi wa udini by Lema".

Nimekupa kauli hizo ili tufakari upya ni nani anae vuruga amani na utulivu katika hii nchi. Kwanini kila kitu kiovu ni CHADEMA?

Halafu hao hao CHADEMA wanataka kuunda jeshi ambalo wamelipa jina la kikosi cha uasi cha Red Brigade (Italia)? hii inaleta picha gani kwako kama una akili timamu?
 
ccm hovyooooooooo hovyooooo! Kusanyeni nyenu kabisaaaa 2015, kuanzia saiv nahakikisha kila watu ninaokaa nao nikuwahubiri ubaya wa ccm, ikifika sept 2015 niwe na vichwa vyangu mia 7, jamani wanamapinduz wenzangu tufanyeni hvyo

jumlisha na vyangu 700
 
Hawezi kuacha kumuogopa wakati anajua alimwibia kura zake 2010...alizidiwa kwenye kampeni mpaka akawa anakaa chini kuomba kura kama hivi
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1373674013.469846.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1373674013.469846.jpg
    61.2 KB · Views: 168
Hilo jina ndio zuri kupita yoteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.wow.Sasa tuendelee.Nyie magamba sio mnajifanya wajanja,kwa kutengeneza movie za kihindi.enough is enough sasa.msitetemeke ,wala nini sasa hivi.
 
CHADEMA wanataka kuanzisha Boko Haram Tanzania, ni kitu ambacho hakiwezekani. Walikuwa wanapima akili za viongozi wa serikali waone.
 
Nchemba nakushukuru sana kwa kazi yako.wazazi wangu walikuwa wagumu kweli kuhama ccm.Kwa kazi yako nzuri unayofanya nakushukuru sana.week iliyopita wazazi wangu wote wameama ccm na sasa ni chadema na wapo kijijini kabisaaaa.big up endelea tutawaokoa watu wangi na watajua ukweli.Hongera sana Gamba.
 
Ukiangalia huyu funguo malaya juliana na mwenzake hawana tofauti na wachezaji wa kulipwa kama ngasa,leo timu hii kesho ile,ili mradi maslahi yakae vizuri,afadhari ya ngasa alieshindwa kuzuia mapenzi yake kwa yanga,lakini haya malaya wa siasa ni vigumu kuwaelewa wana mapenzi wapi?,huwezi niambia siku chache baada ya kufukuzwa CHADEMA,husahau mapenzi yako kwa CHADEMA,na kuponda as if hukuwahi kukifanyia kazi,hakuna mapenzi yanayopotea ghafla kiasi hicho,ata wale wanaokutumia kuandika utumbo wanajua unafanya hivyo si kwa mapenzi bali ni kama mchezaji wa kulipwa anapotoka timu moja kwenda nyingine,mbaya zaidi tunasikia juliana kaanzisha mapenzi na kocha wa timu aliyoamia,sasa sijui kwa kumpenda kocha ndio style ileile ya mapenzi bila pesa hayaendi,watu kama hawa hawajui watapewa talaka lini,na siku wanapokabidhiwa huwa wanaiahia kujinyonga au kurudi kwa bwana wa zamani kwa kizingizio cha shetani alinipitia.
 
Acha kuleta ujinga humu JF kwa nini mnapenda kujivua akili zenu za kawaida na kuingiza akili za kushikiwa? naomba unifafanulie yafuatayo1. Wale Green Guard waliomkata kwa shoka yule kijana wa CDM wakati wa kampeni kule Arusha walipitia Chipukizi?2. Kama CCM inachagua vijana wa Green Guard kwa kufuata maadili je yule kijana anayesemwa sana kule Arusha kwa ujambazi na huku akiwa Green Guard je huoni kwamba ni wengi wa aina hiyo ndo waliopo Green Guard na ndo maana kila kukicha mnafanyia wenzenu wa CDM uhalifu?3. Katika makambi ambayo CCM ilikusanya vijana mbali mbali kutoka vijijini kule Uyole na wengine kule Singida na kupatiwa mafunzo ya kijeshi na matumizi ya siraha hayo ndo mafunzo ya Chipukizi?4. Kuna thread inayomuonyesha yule Green Guard aliyehasi na kuelezea mambo yote yanayofanywa na Green Guard likiwemo la kumwagia Tindikali yule kijana mnayemfanya katuni kwenye mikutano yenu mbona mmeamua kuipotezea ebu nieleze kidogo tu ni kweli yule kijana alikuwa Green Guard?

Mkuu, ni propaganda za CHADEMA tu ambazo kimsingi hazina mashiko, hakuna kijana wa Green Guard aliempiga mtu na shoka, yule kijana ambae ni mshabiki wa CHADEMA ni mkorofi na inasemekana ni mwizi, hivyo alinusurika kuuwawa kutokana na kitendo chake cha wizi. Kama unavyojua Lema na vijana wake walivyo, hapo hapo wakazusha kuwa Green Guard ndio wamehusika na kumpiga na shoka,jambo ambalo kulithibitisha hawawezi.

Kuhusu kijana anaedai kuwa amesaliti UVCCM, kwanza nianze kwa kusema UVCCM hawapewi bunduki, hivi kwa akili ya kawaida, bunduki inatumika wakati gani kwenye uchaguzi? mkuu propaganda zingine ni za ajabu kweli.Umeona wapi mtu akatishiwa bunduki kwenye uchaguzi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom