Real Estate Developer

bigjeff

Senior Member
Oct 25, 2009
111
22
Wandugu ambao mpo kwenye Sector hii naombeni msaada wakujua jinsi ya kupata mkopo wa kujenga ,changamoto zake, gharama, na vinaitajika nini ili upate mkopo?(Business Proposal).Tuna sehemu nzuri sana Dar(kijitonyama) viwanja viwili vitatu ambavyo nataka kuviendeleza kwa kujenga small apartments kwa ajili ya waajiriwa (mabachelors)......myelife na olesaidimu nimesoma Threads mbili tatu mnaonekana mnauzoefu kidogo nitaomba msaada wenu.Asanteni.
 
Simply mkopo wa kujenga unategemea na conditions ambazo zinakuwa attached na taasis husika, ambayo ndio itakayokupa hiyo huduma. Either ni bank or micro finance institutions kama WAT SACCOS etc. So cha muhimu hivyo viwanja viwe na hati miliki ambayo itakuwa ndo collateral/security/dhamana ya mkopo husika.
Changamoto za mkopo sana sana ni jinsi taasisi husika itakavyokutathimin na kuridhia kukupa huo mkopo, pia masharti ya mkopo yatimizwe kama kulipa mkopo kwa wakat husika... Na mpaka sasa mabenk mengi hapa nchini yanatoa mortgage loan kwa interest ya 18-20%.
Nakushauri kabla ya kuamua kufyatua hzo appartments hapo fanya feasibility study kwanza kujua kama biashara yako itakulipa na pia kiwezesha kulipa mkopo wako utakaouchukua.
KARIBU
 
Asante sana 4G kwa kuchukua mda wako kuandika haya machache ya muhimu
 
Wadau mchango jamani naona hii sector inakuwa ngumu sana kupata details zake nimesoma threads zilizopita but naomba mawazo zaidi ningependa sana mchango wanaoelewa hii kitu mfano kutayarisha business proposal (,kupata michoro,costs,attorney,schedule,) na mengineyo.
 
Uwekezaji kwenye sekta ya Real Estate ni mkubwa na una market risk kubwa zaidi. Kabla ya kuwekeza ni vema kuzingatia hali ya soko na kufanya tafiti za uwezekano wa mradi kufanikiwa (appraisals).

Kimsingi unapoamua kuwekeza kwenye real estate kuna bidhaa za aina mbalimbali kama vile nyumba za kuishi, ofisi, maduka makubwa, kwa miji mikubwa hata parking space au mchanganyiko wa bidhaa zote hizo kwa pamoja.

Bidhaa hizi huwekwa sokoni kwa njia mbalimbali pia. Unaweza kuuza au kupangisha kadili ya malengo yako. (Sheria imerahisisha mambo si lazima uuze jengo lote unaweza kuuza hata nusu floor au apartment moja katika jengo zima)

Mambo ya msingi ya kufanya;

1. Kabla hujaamua kuwekeza kwenye bidhaa yeyote kati ya nilizotaja au na ambazo zijataja fanya utafiti bidhaa gani inalipa na ina risks zipi. ( Market and Financial feasibility studies) Hii kuna wataalamu wanafanya kama valuers, real estate analysts, finance and economic analysts etc

2. Chagua bidhaa yako. Unataka apartments, office au retail property? Unaweza kuchagua baada ya kuwa umefanya utafiti wa kina.

3. Andaa michoro kutokana na uchaguzi uliofanya hapo juu. Hapa utaenda kwa Architects na Engineers. Then tafuta QS wakuandalie gharama za ujenzi wa bidhaa yako hadi inakamilika.

4. Kama hauna ardhi, huu ndio muda wa kuinunua ila hakikisha pale unapoinunua panakidhi matazamio na malengo yako kwa bidhaa uliyoamua kuwekeza. Mfano usijekwenda Kwa mtogole unaweka Mall utapoteza pesa bure. Ni vema wanaokufanyia feasibility studies wakueleze pia mahala sahihi pa kuweka mradi wako.

5. Tafuta mkopo wa kukuwezesha kujenga bidhaa yako. Feasibility reports ndio Proposal yako na michoro yako pia ni part. Sambamba na hilo unatakiwa uwe na business plan inayoonesha utafikia vipi kile ambacho kipo kwenye feasibility.

6. Ukishapata pesa kinachofuata ni ujenzi, engineer wako anaweza kukupatia schedule ya ujenzi ambayo utaitumia kupata mkopo kwa awamu iwapo hutopata mkopo in a lump sum.

Ntarudi baadae kuendelea
 
Nashukuru sana chief kwa kuchukua muda wako na kuandika haya muhimu nitayafanyia kazi, haya niliojifunza na sita sita kukusumbua pale nitakapokwama nipate ushauri zaidi hii ni ndoto yangu .
Kwa sehemu ipo ni maeneo ya kijitonyama nimefanya utafiti nikaona mji unakuwa sana ukianzia victoria kuja makumbusho new offices ni nyingi ,kwahiyo vijana wengi professionals wataitaji kuishi karibu ndio target market yangu napia unaona NHC wanajenga apartments zao but bei zao kidogo nikubwa kwa vijana wanaonza kazi sidhani kama they can afford .
Na nataka nijue ninapoenda bank watataka kuona business proposal kwanza au watatuma valuers wao waone eneo nakuamua wao watatoa how much?
Na suala la michoro ninaweza kuwatumia hawa vijana fresh from chuo nadhani gharama zao sio mbaya kama hawa wengine ambao wazoefu na bei zao ni zoefu pia?Na pia hao Qs?
Engineers inabidi wenye uzoefu maanna isiletekizaazaa kwenye ujengaji
 
KOTU CHA KUFANYA KWANZA THAMINISHA HILO ENEO LAKO,UKISHAPATA NA KUJUA THAMANI YA ENEO LAKO..NDIYO UNAWEZA FIKIRIA KUHUSU KUCHUKUA MKOPO WA KIASI KIKATACHO KUFAA

OVA
Wandugu ambao mpo kwenye Sector hii naombeni msaada wakujua jinsi ya kupata mkopo wa kujenga ,changamoto zake, gharama, na vinaitajika nini ili upate mkopo?(Business Proposal).Tuna sehemu nzuri sana Dar(kijitonyama) viwanja viwili vitatu ambavyo nataka kuviendeleza kwa kujenga small apartments kwa ajili ya waajiriwa (mabachelors)......myelife na olesaidimu nimesoma Threads mbili tatu mnaonekana mnauzoefu kidogo nitaomba msaada wenu.Asanteni.
 
KOTU CHA KUFANYA KWANZA THAMINISHA HILO ENEO LAKO,UKISHAPATA NA KUJUA THAMANI YA ENEO LAKO..NDIYO UNAWEZA FIKIRIA KUHUSU KUCHUKUA MKOPO WA KIASI KIKATACHO KUFAA

OVA
Thanks Chief nitafanya hivyo kaka
 
Tha
KOTU CHA KUFANYA KWANZA THAMINISHA HILO ENEO LAKO,UKISHAPATA NA KUJUA THAMANI YA ENEO LAKO..NDIYO UNAWEZA FIKIRIA KUHUSU KUCHUKUA MKOPO WA KIASI KIKATACHO KUFAA

OVA
Thanks Chief will do that.
 
Nashukuru sana chief kwa kuchukua muda wako na kuandika haya muhimu nitayafanyia kazi, haya niliojifunza na sita sita kukusumbua pale nitakapokwama nipate ushauri zaidi hii ni ndoto yangu .
Kwa sehemu ipo ni maeneo ya kijitonyama nimefanya utafiti nikaona mji unakuwa sana ukianzia victoria kuja makumbusho new offices ni nyingi ,kwahiyo vijana wengi professionals wataitaji kuishi karibu ndio target market yangu napia unaona NHC wanajenga apartments zao but bei zao kidogo nikubwa kwa vijana wanaonza kazi sidhani kama they can afford .
Na nataka nijue ninapoenda bank watataka kuona business proposal kwanza au watatuma valuers wao waone eneo nakuamua wao watatoa how much?
Na suala la michoro ninaweza kuwatumia hawa vijana fresh from chuo nadhani gharama zao sio mbaya kama hawa wengine ambao wazoefu na bei zao ni zoefu pia?Na pia hao Qs?
Engineers inabidi wenye uzoefu maanna isiletekizaazaa kwenye ujengaji

Mkuu nimerejea labda nieleze kwa kifupi juu ya masuala machache uliyoyataja;

Swala la Ofisi Kijitonyama.

Hili kwa sasa ni eneo zuri kwa kujenga ofisi kwa kuwa kuna node imeanza kuota maeneo hayo. Ni vema kuzingatia pattern ya office properties ya eneo husika. Eneo lile ofisi property zinaegamia barabara kubwa ya Al~Hassan Mwinyi natumaini nawe eneo lako lipo usawa huo. Kujenga jengo la Ofisi mbali na barabara hiyo kunaweza kukuathiri hasa kama utajenga upande huu ndani wa eneo la Makumbusho kwa kuwa eneo hilo kwa kadili unavyoenda mbali na barabara kuu lina miundo mbinu mibovu na linazidi kujitenga na ofisi nyingine kitu ambacho si kizuri. Majengo ya ofisi yanafaa yawe karibu karibu kwa kuwa huduma zinategemeana kati ya ofisi moja na nyingine.

Kuna risk kubwa ya kuangalia hapa. Iwapo serikali itaamua kuhama kweli kutoka Dsm, majengo mengi ya katikati ya mji yatakuwa wazi. Hivyo kuna uwezekano ofisi nyingi za pembezoni mwa mji hasa hapo Kijitonyama wakarudi Posta. Iwapo watarudi, majengo mengi hapo yatakosa wapangaji na wewe ambaye ndie kwanza umejenga unaweza kujikuta kwenye wakati mgumu.

Kama utajenga nyumba za kuishi (eg apartments) kuna hitajika umakini mkubwa. Wateja wengi wa apartments sio graduates wa chuo wala waswahili ni professionals kama ulivyosema. Ila kama umefanya research utagundua biashara ya apartments nayo imeanza kuyumba. Bei za kupanga na kununua zimekuwa changamoto kwa Watanzania wa kawaida.

Watanzania wenye hali nzuri kidogo na foreigners ambazo ndio wadau wakubwa nao ni kama wameanza kuwa wachache ukizingatia supply ya properties mpya.

Hata hivyo kama utaweza kumarket vema bidhaa yako na kuibrand vizuri soko bado lipo.

Swala la Mikopo Bank
Bank watahitaji vyote collateral na business proposal kwa kuwa pesa ya kudevelop property sio ndogo. Kwa mantiki hiyo watafanya valuation ya mali unayoweka kama collateral ili kujua unakopesheka hadi kiwango kipi. Pia kama ni mkopaji mzuri bank na una biashara nyingine unaweza kukopesheka zaidi juu ya kiwango cha collateral yako.

Bank tofauti zina sera na riba tofauti. Ni vema ukatafiti hasa riba na masharti ya kila bank kabla hujaamua kukopa bank yoyote.

Swala la kutumia vijana ni cheaper option ila ina complications zake. Kuna swala mathalani la vibali, mfano Architect kwa project unayokusudiwa lazima awe amesajiliwa, QS na Engineer vilevile ili upate vibali vya ujenzi.

Hata board husika nazo hufanya ukaguzi wa kushtukiza kuangalia kama engineer amesajiliwa au la.

Lakini hili si kusajiliwa si kikwazo zipo namna za kutatua changamoto hizo. PM kujua unavukaje hapo.

Kuhusu bei mara nyingi QS ni 2% ya gharama ya mradi na Architect huwa 3~5%. Hata hivyo hizo bei ni muongozo tu, bei halisi hukubaliwa kwa majadiliano.

Mkuu nakutakia kila la heri katika kudevelop property yako.
 
Nashukuru sana kiongozi nitaku pm my number tuongee zaidi
 
Back
Top Bottom