Jodeny
JF-Expert Member
- Mar 26, 2012
- 201
- 25
Wakuu wa mikoa wengi wamekuwa wakipambana kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na maisha bora na kupunguza kero zinazowakabili. Wengi wamejikita katika kusaidia wakulima kunufaika na kazi wanazozifanya, lakini kwa huyu Parseko Kone wa Singida mambo yamekuwa tofauti na yeye amekuwa akikandamiza watu wake hasa wakulima.
Mbaya zaidi ni kwamba, huyu jamaa amejikita zaidi kwenye siasa kwa kushirikiana na kundi moja la mafisadi kupanga safu za uongozi ndani ya CCM ili kutimiza malengo yao kisiasa mwaka 2015. Nikiwa mkazi wa Singida mwenye uchungu na babu, kaka, dada na ndugu na jamaa nashauri huyu jamaa atoswe hana la maana analolifanya. Pia, wadau wanaomfahamu zaidi wamwage data ili ajadiliwe hapa jamvini.