RC Hapi abaini madudu manispaa ya Iringa

MASIGA

Senior Member
Aug 29, 2015
130
281
~Udhaifu, upigaji kwenye miradi inayosimamiwa na manispaa vyabainika

~Migogoro ya ardhi Kihesa yateka mkutano

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amefichua madudu katika miradi ya machinjio mapya ya Ngelewala yaliyojengwa na fedha za serikali kwa milioni 900 takribani miaka 9 bila kukamilika huku manispaa wakihitaji shilingi bilioni 1.3 kukamilisha.

Tukio hilo limetokea jana wakati alipotembelea machinjio hayo ambapo kwenye taarifa iliyosomwa na afisa mifugo imetoa maombi kwa serikali kuwaongezea shilingi bilioni 1.3 kukamilisha machinjio hayo huku fedha za awali shilingi milioni 928 zimetumika machinjioni hapo bila kukamilika mpaka sasa.

Mkuu huyo wa mkoa akanusa harufu ya upigaji baada ya kuomba BOQ kutoka kwa mhandisi wa halmashauri manispaa ya Iringa Michael Sakala na kuikosa hivyo kuagiza uchunguzi kufanyika kwa mradi huo wa machinjio na endapo itabainika yeyote amehusika kwenye upugaji wa mradi huo basi achukuliwe hatua.

Aidha mkurugenzi Mpya wa manispaa Iringa ameeleza mbele ya RC kuwa naye alishtushwa na Fedha hizo zinazoombwa wakati kwa tathmini Mpya waliyofanya wamebaini kuwa ikipatikana shilingi milioni 300 hadi 400 tu machinjio hayo yataanza kufanya kazi na kuingiza mapato.

Katika hospitali ya Frelimo, mkuu wa mkoa amezindua jengo la kufulia nguo na kukausha pamoja na mashine mbili za kufulia kwenye hospitali ya Frelimo lililojengwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Iringa lenye thamani ya shilingi milioni 32 na kuwapongeza kwa hatua hiyo ya kuisaidia jamii yake hivyo kujenga mahusiano mazuri.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa hakuridhishwa Na taarifa ya ujenzi wa maabara na jengo la uchunguzi kwa shilingi milioni 560 unaotaka kufanywa katika hospitali hiyo. Mkuu wa Mkoa ametaka maelezo ya kina na nyaraka zote za ujenzi akidai pesa hizo ni nyingi sana.

”Tunajenga vituo vya afya vilivyo na majengo matano hadi sita ikiwemo wodi za kulaza kwa milioni 400 hadi 450 kwenye Mkoa wetu. Leo hii majengo mawili madogo inakuaje yagharimu milioni 560?Hapa kuna harufu ya upigaji." Alisema Mkuu wa Mkoa akikagua ramani za majengo hayo.

Mwisho,amehutubia mkutano wa hadhara kwa kusikiliza kero za wananchi huku kero kubwa zikiwa ni migogoro mingi ya ardhi, usimamizi mbovu wa miradi na kuwataka wahusika kutembelea kata hiyo kwa ajili ya kutatua migogoro.

”Manispaa hii imejaa ubabaishaji.Migogoro ya ardhi na dhuluma kwa wanyonge vimekithiri sana.Mradi wa machinjio umekwama miaka karibu minne,mnataka niwaombee bilioni 1.3. Mkurugenzi Mpya kaja kagundua akipata milioni 300 tu machinjio inaanza. Nyinyi mliodai mnaongoza manispaa miaka yote mmeshindwa kwasababu mmetawaliwa na upigaji mtupu. Majengo mawili ya kawaida mmebariki milioni 560, kamati ya fedha inayoongozwa na Meya inafanya kazi gani??Nawahakikishia wananchi, nitatembea kila kona na nitasimamia kikamilifu fedha za serikali ambazo ni kodi zenu. Hakuna wa kunizuia wala kunikatisha tamaa...” Alisema RC Hapi huku akishangiliwa na wananchi wa Kisesa.

”Mkurugenzi wewe ni mpya hapa,saidiana na DC simamia vizuri miradi na watendaji wako ili kero hizi zishughulikiwe.”

#ZiaraIringaMpya
IMG-20180927-WA0070.jpeg
 
Back
Top Bottom