Meitinyiku L. Robinson
JF-Expert Member
- Aug 29, 2011
- 412
- 90
Katika hali ya kushangaza Mkoa wa Arusha umeonekana kugubwikwa na sintofahamu baada ya Chaguzi zinazoendelea ndani ya Chama kuonekana ama kuingiliwa au kutishiwa na vyombo vya dola.
Haya yamebainika leo baada ya Mkuu wa Mkoa anayemwakilisha Raisi katika Mkoa kuonekana kuingilia chaguzi hizi hasa uchaguzi wa kesho wa Vijana Mkoani Arusha baada ya kukutana na genge la wahuni wa katika Mkoa huu na kuwalipa fedha za wapiga kura ili kesho wafanye fujo na hatimaye kuvuruga uchaguzi huo.
Hili limesemwa na mmoja wa kijana aliyelipwa fedha hizo akisisitiza kuwa RC kawaahidi vile vile fungu jingine pale watakapokamilisha zoezi hilo akidai kuwa hayo ni maagizo kutoka ngazi za juu.
Baada ya kupatikana kwa habari hizi Vijana Mkoani hapa wameonekana wakiwa katika makundi wakiapa kuwa kama RC katumwa Mkoani kwa kazi ya kuwachagulia viongozi basi hayo yatajulikana kesho hata kama ni kwa damu. Mtoa habari kasisitiza kuwa kuna mtu ambaye system inamuhitaji ambaye ni lazma ashinde na asiposhinda basi fujo zifanyike.
Haya si ya kushangaza manake hata majuzi katika chaguzi za Wilaya hasa Wilaya ya Arumeru DC mmoja alisikika akisema kuwa asiposhinda yule anayehitajika basi kuna watu atawaweka rumande.
RC; katafadhalishwa yafuatayo,
Mosi, ofisi ya Mkoa ni mahala pa kumwakilisha Raisi na kutatua kero za Wananchi na si pango la wahuni na vikao vya magendo visivyo na msingi wowote kwa wananchi
Pili, awasiliane ba hao aliowapa kazi hiyo na asitishe mara moja la sivyo tutajikoki ipasavyo na Arusha hapatakuwa sehemu salama kwa kesho
Tatu, katumwa kuiwakilisha Serikali na si Chama
Nne, Awaachie vijana jukumu la kuamua manake hao ndio wajuao ni yupi atakaye wafaa
Tano, hela za wapuga kura zitumike kwa namna ambavyo imeidhinishwa na si vinginevyo
Sita, Akumbuke spidi aliyokuja nayo na aliyonayo sasa
Saba, Kama anadhani kukamata baadhi ya Vijana ni suluhu usiku ashauriane na mkewe juu ya usahihi wa jambo hili
MWISHO; Kiongozi alishapangwa yeye yu nani hata abatilishe????