Rasimu ya pili ya katiba

Pendesha

Member
Apr 18, 2013
99
60
Kama kuna mtu amekielewa vizuri kipengele kinacho elezea bunge La jamhuri ya muungano wa Tanzania. Nilitaka ufafanuzi kwani kinasema Tanganyika itatoa wabunge 70 je, nikutoka majimbo yapi? Au n utaratibu gani utatumika?
 
Natazama Chanel Ten kwenye kipindi cha 'Je tutafika' na Mzee Makwaiya.
Wapo wageni wawili mwl. Sabato na mwl Bashiru toka chuo kikuu cha UDSM. Siwaelewi kama kweli wazalendo au wametumwa au wameagizwa au ------------ na maccm kutetea hoja ya serkali mbili?
Naomba mrejesho kwa mnaofuatilia.
 
Wadau wa Jf,

Katika rasimu ya pili ya katiba kunakipengele sijakifahamu ki undani wenye uzoefu wa mambo hebu ni fafanulieni,

Kwa kumbukumbu zangu za haraka haraka suala la katiba mpya limekuja baada ya baadhi ya wananchi kulalamika juu ya muungano wa Zanzibar na Tanganyika na hata kufikia kipindi wengine kudani muungano hauna manufaa na kutaka kuvunjwa na kila nchi ijitegeee jukumu la kujadili katiba likaibuka.

Katika rasimu hiyo ya pili sura ya sita kipengele cha kwanza "a" kinasema " Muundo wa jamuhuri ya muungano utakua wa serikali tatu yaani serikali ya Tanganyika, serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya muungano" Je, kipengele hicho kinamaanisha muundo wa serikali tatu umepitishwa? hebu nifafanulieni.
 
,

Kwa kumbukumbu zangu za haraka haraka suala la katiba mpya limekuja baada ya baadhi ya wananchi kulalamika juu ya muungano wa Zanzibar na Tanganyika na hata kufikia kipindi wengine kudani muungano hauna manufaa na kutaka kuvunjwa na kila nchi ijitegeee jukumu la kujadili katiba likaibuka.

Katika rasimu hiyo ya pili sura ya sita kipengele cha kwanza "a" kinasema " Muundo wa jamuhuri ya muungano utakua wa serikali tatu yaani serikali ya Tanganyika, serikali ya mapinduzi ya Zanzibar n

a serikali ya muungano" Je, kipengele hicho kinamaanisha muundo wa serikali tatu umepitishwa? hebu nifafanulieni.[/QUOTE]
 
Nijuavyo mm yale ni mapendekezo tu ya waanchi na bado hatujajua yatapita au la maana maccm hawataki huo mpango
 
Heshima kwenu Wakubwa,
Nimepitia kwa makini sana Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya hasa Ibara ya 32 ambayo inaelezea juu ya Uhuru wa Imani ya Dini.

1. Ibara ndogo ya (1) ya Ibara hiyo inasema kwamba kila mtu ana uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya Imani ya dini na uhuru wa kubadilisha dini, n.k.
2. Ibara ndogo ya (2) ya Ibara hiyo inaelezea kwamba uhuru wa kutangaza dini usikiuke sheria za nchi.
3. Ibara ndogo ya (3) inaelezea kwamba shughuli za kueneza dini zitakuwa nje ya Shughuli ya Mamlaka ya Serikali.

Hebu tuangalie IBARA NDOGO YA (4) ambayo imenifanya niandike Thread hii:
4. Hifadhi zilizotajwa katika Ibara ya 32 zitakuwa chini ya TARATIBU ZILIZOWEKWA NA SHERIA AMBAZO NI MUHIMU KATIKA JAMII YA KIDEMOKRASIA KWA AJILI YA USALAMA, AMANI, MAADILI NA UMOJA WA JAMII NA WA KITAIFA NA VITASIMAMIWA KWA UTARATIBU ULIOAINISHWA KWENYE SHERIA ZA NCHI!

Ni maoni yangu kwamba Ibara ndogo ya (4) ambayo imeweka mwanya wa kutunga Sheria nyingine, huku Ibara ndogo ya (3) inasema kwamba Shughuli za kutangaza dini zitakuwa nje ya Mamlaka ya Serikali inatupa wasiwasi kwamba Sheria hiyo itakuwa ni ya nini?

Kwa jinsi Serikali ya sasa ya JK ilivyoanza kuweka kwenye Ilani yake Suala la Mahakama ya Kadhi na jinsi Waislamu walivyoapa kwamba wasingekubali kwa vyovyote vile Suala la Mahakama ya Kadhi kutowekwa kwenye Katiba Mpya Ibara hii ya 32 inaweka WINGU ZITO juu ya Uwepo wa Mahakama hizo baada ya Katiba Mpya kutungwa, kwa kupitia SHERIA itakayotungwa na Bunge kama Ibara ndogo ya (4) inavyosema.

Nawasilisha kwa mjadala zaidi!!
 
Mdini mkubwa wewe,

Katiba ni sheria mama, na sheria nyingine zinatungwa zifuate Katiba.

Umefosi king tu kuleta mjadala wa kadhi hapa
 
Mahakama ya kadhi si tayari ipo.

Si ndio hapo sasa,mahakama waislamu waliruhusiwa waanzishe na kuziendesha wenyewe.
Na rasimu imeelekeza wazi shughuli za uendeshaji dini zitakuwa nje ya shughuli za serikali.
Na siku zote katiba inatungwa kama mwongozo mkuu wa sheria zingine zote zitakazo tungwa.
Sasa sijui hoja ipo wapi!
 
Iwe...isiwe...tunahitaji ukombozi tumeshanasa tunahitajika kujinasua ,wazee wetu walipambana nawajerumani kwa kuyakataa hayo wakapoteza uhai wao mali zao na nchi yao ....ndg zangu mnaposikiaMAPINDUZI DAIMA...(2) chamacha mapinduzi kina wenyewe... Bara itakuwa pwani na pwani itakuwa bara mtafakari wanaopinduliwa ni WASWAHILI na imani yao sasa hivi utafurukutia wapi utasemea wapi usikilizwe sisi hatuna thamani ni daraja la watu kuvuka waende watakapo.nina mengi lakini.......
 
Iwe...isiwe...tunahitaji ukombozi tumeshanasa tunahitajika kujinasua
Mnahitaji ukombozi,kwani mnatawaliwa na nani?
wazee wetu walipambana nawajerumani kwa kuyakataa hayo wakapoteza uhai wao mali zao na nchi yao
Nchi hii wengi wa walio pigania uhuru walikuwa wa dini za asili,si muslims wala Christians,
wao labda ndio wangedai uchifu..
....ndg zangu mnaposikiaMAPINDUZI DAIMA...(2) chamacha mapinduzi kina wenyewe...
Mwalim alikuwa sahih sana kusema dhambi ya ubaguzi mbaya..
Mara CDM ya wakristo,
mara CCM ya muslims,
sasa CCM ina wenyewe.. Khaa!
mtafakari wanaopinduliwa ni WASWAHILI na imani yao sasa hivi utafurukutia wapi utasemea wapi usikilizwe sisi hatuna thamani ni daraja la watu kuvuka waende watakapo.nina mengi lakini.......

Kwa hiyo unatamani tuwe nchi ya utamaduni wa waswahili?
 
Si ndio hapo sasa,mahakama waislamu waliruhusiwa waanzishe na kuziendesha wenyewe.
Na rasimu imeelekeza wazi shughuli za uendeshaji dini zitakuwa nje ya shughuli za serikali.
Na siku zote katiba inatungwa kama mwongozo mkuu wa sheria zingine zote zitakazo tungwa.
Sasa sijui hoja ipo wapi!

Hoja ipo kwenye Ibara ya 32 (4), soma vizuri!
 
Mnahitaji ukombozi,kwani mnatawaliwa na nani?
Nchi hii wengi wa walio pigania uhuru walikuwa wa dini za asili,si muslims wala Christians,
wao labda ndio wangedai uchifu..

Mwalim alikuwa sahih sana kusema dhambi ya ubaguzi mbaya..
Mara CDM ya wakristo,
mara CCM ya muslims,
sasa CCM ina wenyewe.. Khaa!


Kwa hiyo unatamani tuwe nchi ya utamaduni wa waswahili?

Utamaduni wa Waswahili ndio upi?
 
Back
Top Bottom