RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa


Hii rasimu ya Katiba naweza kusema ni ya kimapinduzi -- yaani imefumua mfumo mzimo wa utawala ambao CCM waliufanya kama mbeleko yao kubwa ya kujibeba.

Ndiyo, siyo waliitumia tu kung'ang'ania madarakani, lakini pia CCM walikuwa wanaipigia debe sana eti ni the best! Wameumbuka! Utakisifiaje hadi mbinguni kitu kilichokaa kihovyo hovyo tu eti tu kwa sababu inakubeba wewe? CCM haitadumu ndani ya hii katiba mpya!
 
Mbona kama nashawishika kuuunga mkono ushauri wako wa jina Tanzanite. Jina lenyewe linashiria Tanzanite nchi ya madini Tanzanite. hebu tusubiri tuone kama wataunga mkono wengine.
 
Japo kimsingi yaweza kuwa mwelekeo mzuri,lakini si wakati wa kushika glasi ya wine au wisky kujipongeza.kuna watu wanapongeza wakiwemo waandishi wa habari kama akina majid mjengwa,rasmu ni hatua ya pili baada ya ukusanyaji na uchambuaji maoni.kuna mabaraza ya katiba,bunge la katiba na mwisho kura ya maoni.katika ngazi hizi zote rasmu hii yaweza kubadilishwa ibara na kuweka nyingine na maoni mapya.nani anayejua kwa mabaraza haya ya kata yaliyotengenezwa kirushwa,kiudini na kisiasa kama alivyokubali mzee warioba,serikali tatu itarudi,maadili na misingi ya taifa viatapita hai kwenye mabaraza haya.je kwenye bunge la ktiba ambapo wabunge wa sasa ni wajumbe kwa mjibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba na wao ndo watakuwa wengi,ikijumlishwa pia kwamba nyongeza ya wajumbe itakuwa kwa uwiano wa vyama vya siasa na uwakilishi bungeni.rushwa,umaslahi umetamalaki ndani ya bunge letu nini tutegemee.huu si wakati wa kusherehekea ndo wakati wasisi wananchi kuongeza juhudi ili mamlaka yetu ijulikanf kwa watakaojadili rasmu.
 
Hili lenyewe la Tanzania ukiwa nje ya nchi mtu akauliza unatoka wapi ukasema Tanzania swali linalofuata hama ni Where is Tanzania au Is Tanzania near Nigeria. Njia rahisi huwa ni kusema Tanzania is near Kenya. Sasa ikiitwa hiyo Tanzanite si ndo watasema, Is Tanzanite one of the Caribbean Islands? Hapo ndo tutachoka kabisa. Bora tubaki na hiyo Tanzania kiugumu ugumu
 
Hodi hodi washikadau..........Rasimi rasimu rasimu.......Lamgambo likilia kuna jambo......ile rasimu mliokuwa mnaisubiria sasa imetoka.......nawaombeni muisome kwa umakini ili muweze kuchangia hoja vizuri
 
Hili ni swali nyeti sana Mr. Aweda, na kwa kweli watu wengi hawajaliona hili!. Ngoja mijadala ianze ndo watu watajua ni nini unaulizia. Hakika, natamani sana kumsikia Prof. Issa Shivji kwenye hili suala!.

Ila mkuu KAZIMOTO katoa maelezo mazuri, inaweza ikawa ndo sulushisho?? Natamabi sana GTs waje kwa hii thread kuchambua hii mada, hii mtego sana mkuu Mikael P Aweda
 
Wakuu Kuwepo kwa serikali 3 Tanganyika, Zanzibar na Shirikisho pamoja na kupungua mambo ya muungano ni dalili tosha za muungano huu kupungua nguvu kiutendaji. Wabunge watakuwa 25 Tanganyika ambayo ni sawa na mikoa ilivyo na Zanzibar 10 vivyo hivyo. Utendaji wa kazi wa mbunge wa shirikisho kwa kuhudumia mkoa utakuwa hauna ufanisi ukizingatia jiografia ya mikoa husika. Wananchi wengi hususani wa vijijini hatapata uwakilishi makini wa mbunge anayehudumia mkoa mzima. Inawezekana kabisa wabunge wa Muungano wakakosa kabisa maana kwa wananchi na Wawakilishi ndo wakawa bora zaidi. Na mbaya zaidi maraisi wakawa wa vyama tofauti mfano Tanganyika ikawa CDM Zanzibar ikawa CUF na Shirikisho ikawa CCM. Hapo kazi kwelikweli kwa muungano. Ni maoni yangu tu.
 
Haya ndio matatizo ya kutoka digital to analog,maana ninavyoona kama nane TANGANYIKA linafanywa analog ?co 2we makin na rasimu hii ya katib
 
Mh. Jioni njema, Tunaheshimu mapendekezo yako mara kwa mara na ukerketwa wako wa kiTaifa na uzalendo. Ahsante na huo ndo moyo wa kujitambia hapa nchini.
Mie kwa mtazamo hua sipendelei kuyumbayumba au kutangtanga. Lingine kwanini siye tu tuwetunabadilisha mara zote, je nchi hii inatafauti hgani na nchi zingine ambazo tangu kuwepo hadi leo hazijabadilisha jina. Sie ukoloni tulibadili na muungano tukabadili nk. (ther s something wrong)!! kwani hata TANGA NYIKA yote niyakupandikiziwa.
pamoja kujiendelza. Best of luck mkuu.
 
Hili lenyewe la Tanzania ukiwa nje ya nchi mtu akauliza unatoka wapi ukasema Tanzania swali linalofuata hama ni Where is Tanzania au Is Tanzania near Nigeria. Njia rahisi huwa ni kusema Tanzania is near Kenya. Sasa ikiitwa hiyo Tanzanite si ndo watasema, Is Tanzanite one of the Caribbean Islands? Hapo ndo tutachoka kabisa. Bora tubaki na hiyo Tanzania kiugumu ugumu
hapo fika and hope ibaki as is. Tanzania kwa watu wake ni poa na kujitambulisha inaridhia.!!
good suggestion.
 
Kwa kweli hii haikubaliki tunarudishwa kulekule. Lingine pia ni la mhimili wa mahakama (judicial pole) ni yaleyale eti rais ndo anateua how. HAYA TUYAKATAE KWA SAUTI KUBWA SANA.
 
Wakuu,sina shaka kua wanasiasa walio wengi wa upinzani na wa chama tawala wataipinga sana hii rasimu kwani imeonyesha kuwabana sana na watakosa ulaji mawaziri 15 wasiotokana na chama chochote,wabunge 75,wagombea binafsi,spika naibu spika wasiotokana na chama chochote,etc.

kwa namna fulani hii rasimu ya katiba imesimamia utaifa na si maslahi binafsi ya wanasiasa.NA WALIO WENGI WATATOKA NJE YA SYSTEM KABISAA.

C.C LUKUVI,WASSIRA,NDUGAI,GHASIA,S.SIMBA,MWIGULU,ANNA KILANGO N.K.
 
Turejeshewe Tanganyika yetu. hata kama tuliikuta Tanzania lakini kiasili sisi sote ni watanganyika na hii ni muhimi kuelewa. Nimesoma rasimu inataja kutakuwa na Serikali ya Tanganyika, Zanzibar na ile ya shirikisho la Tanzania. Sioni shida katika kurejeshewa Tanganyika maana sasa hata wale maliberali watanyamza au labda waunde jingine.
 
Lakini mkuu, ukumbuke kwamba Jaji Warioba alisema, namnukuu, "Tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza mfumo wa Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar."

Angalia vizuri ktk rangi nyengundu, tume inapendekeza serikali ya "Tanzania Bara." Imekwepa kusema "Tanganyika." Kwa nini? Labda tushauri kwanza kwamba katika rasimu warekebishe mahali hapo ili pasomeke kwamba "Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar." La sivyo, jina litakalorejeshwa kwa bara litakuwa hilo lililopendekezwa na tume.
 
mbona kuna ambao walisema bora tuitwe "Kilimanjaro" ili jina la mlima huo maarufu duniani uvutie watu kuja kutuona? #Ubinafsi
 
Jamani ninasoma mapendekezo ya kwenye rasimu, nashindwa kuelewa hao mawaziri 15 ni wa serikali ipi na je wabunge me na ke kwa kila jimbo ni wa serikali ipi na je ni kwa pande zote za muungano? Yaani mimi sielewi baada ya gharama zote hizo na hoja zote walizokusanya kutoka kwa wananchi tunaambia bado kuna kuandaa rasimu ya katiba ya Tanganyika.

Lakini ukiacha hilo mimi naona ni rahisi sana serikali tatu kusambaratika, kwani aina ya muungano tuliokuwa nao ni toauti na wa shirikisho. Na kiukweli upande mwingine utaona tumepata pa kutokea. Kama hakuna rasilimali za kimuungano kwenye rasim(sijasoma) basi bond yetu itakuwa very weak.
 
Kutakuwa na mkanganyiko sana, kwani hata wabunge 50 wa kutoka Tanzania Bara ni wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika majimbo ya mikoa 25, kwa hiyo wabunge wengi wa sasa hawataweza kugombania nafasi 25 za wanaume na 25 za wanawake, itabidi wasubiri ubunge katika serikali ya Tanganyika ambayo kwa wakati huo itakuwa haipo, na wao watakaa benchi muda wa kutosha tu!
Pia kama muungano una mambo 7 tu serikali itakuwa na nguvu zipi? Hata hilo bunge la watu 75 litafanya nn?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom