Divele Dikalame
Member
- May 4, 2010
- 77
- 12
RASIMU YA KATIBA MPYA
MAONI NA MSIMAMO BINAFSI WA AWALI KUHUSU RASIMU
- Rasimu haijibu kero za mungano na wala ki mantiki haiimarishi muungano. Ni njia ya kisayansi ya kuua Muungano na sijui atakeye wanadganya wa Tanzania kuwa kuimarisha muungano ni kuwa na serikali tatu ni nani na anatupa insurance gani? Watanzania hawakuwa na lengo la kudai serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Rasimu hii, lakini tatizo kubwa la muungano lilikuwa utata wa utekelezaji wa mambo makuu ya kimsingi ya muungano.
- Kuna kila dalili kuwa Tume inayoongozwa na Mh. Jaji Warioba imezidiwa ujanja na makundi maalum ambayo ni hatari katika jamii yetu ya watanzania. Itakumbukwa kuwa kabla ya serikali kuamua kuunda tume tayari genge la wasomi wakiongozwa na Issa Shivji wa Kigoda cha Mwalimu, Kitila Mkumbo aliyekuwa makamu mwenyekiti UDASA na wengine wanaojiita waumuni wa Azimio la Arusha walikwisha anza kutu brainwash wakitumia mijadala ya kisomi iliyoonyeshwa moja kwa moja kwa wananchi kupitia TV, mijadala iliyofanyika kwenye ukumbi maarufu wa Nkrumah, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (live coverage pale Nkurumah Hall). Mambo yote waliyokuwa wanaropoka pale yameingia kwenye hii rasimu. Swali kwa nini yameingia kirahisi bila hata kuchujwa? Kweli mabilioni ya pesa yaliyotengwa kwa tume kufanya kazi ndo yameishia kunakili taarifa zilizokuwapo na kutuletea wananchi tuzijadili?
- Rasimu haijatimiza kiu ya wananchi wa Tanzania. Rasimu hii imetimiza kiu ya makundi ya watu wachache hususan Kigoda cha mwalim, CHADEMA, LHRC, Haki Elimu, MCT na MTF na Tanganyika Law Society. Kwa uhakika zaidi ya asilimia 90 ya Watanzania hawajasikika na wamepigwa butwaa na matokeo ya Rasimu.
6. Tume hii ilipewa takribanshilingi bilioni 50 ili kufanya kazi, kuhoji watu na kutafsiri maoni yaokisayansi. Haitegemewi maoni yakeyatokane na taarifa ambazo ziliwahi kuandikwa hapo Zamani mfano NyalaliCommission au Kisanga Commission au Warioba Commission au Tanganyika LawSociety au Midahalo ya Katiba iliyokuwa ikiandaliwa pale Nkrumah Hall chuokikuu cha Dar-es-Salaam. Kufanya hivyo ni kuwanyima wa Tanzania waliowengikusikika. Kwa mshangao Tume imekiri kuwakuna wa Tanzania walitaka serikali mbili wengine nne wengine tatu. Lakiniyenyewe ikaamua kuchukua serikali tatu. Hii ni kosa kisayansi. Ilibidi kwanzaiainishe ni watu wangapi walisema tatu wangapi walisema nne wangapi walisemambili. Kamani kweli wanayotushauri basi wawe na ujasiri huo huo wa kunakiri maoni ya tumeya NYALALI NA KISANGA NA WARIOBA CORRUPTION COMMISSION WATUELEZE KWA NINI HAYOMAWAZO HAYAKUCHUKULIWA. Mbona hawatuelezi yaliyojiri wakati wa Jumbe na NjeruKasaka maana ilikuwa ni suala nyeti sana kama hilowaliloleta juu ya serikali tatu. Si busara kutumia taarifa ambazo zilitolewa na serikali hiyo hiyozikakataliwa hii ni kuleta kiburi cha kutaka kuilazimisha serikali mambo ambayoina sababu za msingi kuyakataa wakati huo ilipopewa hizo taarifa za Nyalali naKiasanga. SEHEMU YA PILI: · SERIKALIYA TANGANYIKA NA SUALA NYETI LA MUUNDO WA MUUNGANO WA SERIKALI TATU HAYAYANATOKEA WAPI?Tumeilisheheni wataalamu wengi wanaoheshimiwa sana nchinikutokana na umilisi wao mkubwa katika maeneo ya elimu waliyobobea. Lakini inaelekea hawakujisumbuakufanya utafiti wa kina juu ya sehemu hii iliohusu serikaliya Tanganyika na muundo mpya wa serikali tatu walioupendekeza. Hii inaonyesha wamekujana mawazo yao na mawazo ya vikundi ambavyo vimetajwa hapo mwanzo na kutaka kutulazimisha jamii yote ya wa Tanzania tuyaamini. Kwamfano;
- Suala nyeti la muungano. Inabainishwa katika tafiti mbali mbali ambazo tulitegemea Tume inayoongozwa na Jaji Warioba wazisome na kutupa mwongozo wa nini tujadili. Kwa watanzania wengi ambao hawakuwapo wakati muungano ukiasisiwa wangeweza kuelewa kuwa kuna kitu kinaitwa Article IV ambacho kwenye machapisho mbalimbali kinasema;
- Suala nyeti la Muundo wa Muungano: Muungano ni suala nyeti na tukufu ambalo ni lazima lilindwe kwa gharama yeyote ile kwa usalama wan chi yetu tukufu. Kwa kweli na mtu yeyote aneonekana kutaka kutikisa nguzo zake haina budi kumtolea uvivu ili kusambaratisha nguvu zake na kundi lake kwa kutumia rasilimali zenye gharama yeyote ile kwa maslahi ya taifa hili. Kama ilivyotanguliwa kuanishwa kwenye maandiko haya kuwa mifano ya mataifa kadhaa ambayo yamefuata serikali za shirikisho zimeenda na maji kwa kushindwa kusonga mbele kutokana na shida za utawala wa serikali za shirikisho. Hivyo Tume ilitakiwa kuwa ubunifu wa hali ya juu katika kufanya tafiti na uwasilishaji wa wanayoyaota mawazo ya watanzania ya kutaka serikali tatu. Udhaifu mkubwa katika taarifa ya rasimu ya katiba ni kushindwa kuwa wabunifu na kuchambua kwa kina muundo wa serikali. Kwa kiwango kikubwa uamuzi wao hautokani na maoni ya watu waliowahoji. Hii inatokana na ukweli kuwa mara baada ya kuchapisha taarifa kila mtu aliyehojiwa ameshangazwa na serikali tatu. Waliokataa sababu kubwa zaidi ya asilimia 90 ikawa ni kwamba Muungano utavunjika mara moja, ni gharama ambayo watanzania walipa kodi wata twikwa kuendesha serikali tatu badala ya kuelekeza fedha hizo kwenye barabara, shule na hospitali. Onyo hapa kuna wale wakosaji wanasema bora nchi iharibikiwe tukose wote. Hawa wanasaidiwa sana na coverage ya vyombo vya habari na ni hatari kwa usalama wa nchi hii. Wengi ni wapinzani na wana harakati ambao wanaishi hapa Tanzania lakini mishahara yao yote inatoka Ulaya. Hao wanasema bora Tanganyika ije na kwenye huu msafara kuna wanasiasa, kuna maprofessa walioshiwa hoja ambao wamekuwa wakiranda randa kwenye korido za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujikosha kwa vijana wa kizazi kipya wasiowafahamu. Wengi wanatumia kofia ya kumnadi Mwalimu Nyerere. Lakini Nyerere gani angependa serikali tatu? Ni vinara wa makongamano na Majukwaa ya wahariri, katiba nakadharika LHRC kupitia live coverage ya vyombo fulani vya habari.
- Tume haikuzingatia athari za mapendekezo yake: Pamoja kuwa tume ina majaji na wasomi waliobobea na wanafahamu yaliyotokea juu ya Muungano wa Serikali za Shirikisho kama hii ya Warioba Model itakuwa ni sababu kubwa muungano kufa kama ilivyotokea kwenye baadhi ya nchi duniani, hapa kuna mifano michache.