SoC03 Rasilimali za Umma sio za kudharauliwa

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
RASILIMALI ZA UMMA
Rasilimali zinazoonekana za umma ni rasili¬mali zinazoshikika (kama vile miundombinu ya kuonekana, majengo, vifaa, mali na mali¬asili) ambazo zinamilikiwa na/au kusimamiwa na serikali.
Rasilimali hutoa huduma kwa watumiaji, wamiliki na jamii. Hii inaitwa thamani ya huduma. Rasilimali pia zina thamani ya kifedha; ili kupatikana zinahitaji fedha. Jambo la msingi la kuzingatia katika hatua hii ni kwamba thamani ya huduma na tha¬mani ya kifedha zinachangia katika utajiri wa jumla wa jamii.
Usimamizi wa rasilimali ni mfululizo wa shughuli zinazoratibiwa ambazo zinahusu kufuatilia na ku¬tunza vitu vyenye thamani na vya umma. Shughuli hizi zinajumuisha kuwianisha vihatarishi, gharama, fursa na utendaji madhubuti na kubainisha kwa ufanisi thamani ya rasilimali katika kipindi cha maisha yake.
RASILIMALI ZA UMMA NI KAMA IFUATAVYO KWA UCHACHE: -
• Ardhi na maliasili kama vile ardhioevu, misitu na uotoasili.
• Majengo kama vile shule, vituo vya afya, vituo vya jamii, magereza na ofisi za serikali.
• Miundombimu kama vile: Barabara na alama za barabarani na taa za barabarani
• Miundombinu ya maji (usambazaji wa maji, mifumo ya majitaka na maji ya mvua) Mifumo ya kudhibiti mafuriko kama vile mifereji na kingo/malambo
• Mifumo ya usambazaji nishati (uzalisahaji, usafirishaj, usambazaji na uhifadhi)
• Bustani na maeneo ya vivutio
• Miundombinu ya kiutamaduni na kihistoria
• Mifumo ya mawasiliano
• Bandari na miundombinu ya bandari (magati, chelezo, winchi)
• Mifumo na teknolojia ya mawasiliano
• Vifaa kama magari ya kubebea taka, magreda, kompyuta na mashine za kitabibu.
Bila kujali nani anamiliki rasilimali za serikali, lengo la rasilimali hizo ni kutoa huduma. Huduma gani inatolewa, kwa nini inatolewa na kwa namna gani inatolewa ndiyo masuala ya uwajibikaji na utawala bora yanapoonekana na pale yanaposhindwa kutiliwa maanani ndipo sintofahamu nyingi kwa jamii hujitokeza na kudhorotesha maendeleo.
MANUFAA YA USIMAMIZI WA RASILIMALI
I. Usimamizi mzuri wa rasilimali una manufaa kwa mamlaka za serikali za mtaa, serikali kuu na jamii:
II. Uimara wa uchumi unaochangiwa na kupun¬gua kwa gharama za kutoa huduma.
III. Kupata usawa na manufaa ya kijamii kwa sababu jamii ina rasilimali nyingi za huduma na ustawi wa maisha.
IV. Uendelevu na utegemezi wa mazingira ni imara kwa sababu rasilimali zinatunzwa na uzingativu unawekwa katika masuluhisho ya muda mrefu kuliko upatikanaji au urahisi wa muda mfupi.
V. Uthaminishaji mzuri wa rasilimali za asili kama vile ardhi, maziwa, mito na maji ya ardhini una¬saidia kuhamasisha utafutaji wa rasilimali na utayari wa kisiasa wa kuzilinda na kuhakikisha zinahudumia kizazi cha sasa na cha baadaye.
VI. Serikali inaweza kuimarisha uhimilivu wa huduma za umma katika majanga mbalimbali ikiwamo mabadiliko ya tabianchi na dharura zinazohusiana na afya.Wananchi wanafurahia vizuri, huduma endelevu bila kutarajia kushindwa au kukatiwa huduma kusiko mpangilio.
VII. Kujitosheleza kifedha kwa serikali za mitaa kunaimarishwa kwa sababu gharama za baa¬daye zinatabiriwa na akiba hutengwa. Matokeo makubwa katika kuimarika kwa thamani ya fedha ambayo yanasaidia uanzishwaji wa uwekezaji mpya.
VIII. Rasilimali zinazosimamiwa na kutathminiwa vizuri (kwa mfano, ardhi ambayo imepatiwa hati, kusajiliwa na kutathminiwa kwa usahihi) inaweza kutumika kama dhamana kwa ajili ya uwekezaji wa baadaye na usalama wa mmiliki.
IX. Uwazi wa serikali unaimarishwa unaosababisha mawasiliano mazuri na umma na imani kubwa ya umma kwa serikali.
X. Mawasiliano na walipa kodi, maofisa walioteuli¬wa, taasisi za ukadiriaji kodi, taasisi za udhibiti na wawekezaji muhimu wa umma na binafsi yanakuwa madhubuti kwa sababu mipango na matokeo yanarekodiwa na kusambazwa.
XI. Kuongeza thamani ya uwekezaji wa mi¬undombinu kupitia rasilimali na huduma zinazochangia kufanikisha ajenda na malengo ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa ikiwamo Malengo ya Maendeleo Endelevu.
XII. Manufaa haya yanaweza kuonekana katika uchumi na katika ngazi nyingi za serikali. Kwa mfano, kadiri mamlaka za serikali za mitaa zitaka¬vyoimarisha usimamizi wake wa rasilimali chache, nchi nzima itaweza kupata fedha na kuwekeza kutoka katika vyanzo vya ndani na nje ya nchi kutokana na kuimarika kwa thamani ya fedha

NAMNA YA USIMAMIZI WA RASILIMALI KWA BAADHI YA MAENEO YA TANZANIA
1. Kufanya matengenezo ya mara kwa mara kama vile kuweka mafuta kwenye mashine, kupaka majengo rangi au kupandisha hadhi barabara,mitaro ya marabarani kusafishwa, kuhakikisha kwamba rasilimali zinadumu muda mrefu. Kutokutengeneza rasilimali kwa kiwango kunapunguza thamani ya huduma na kunahitaji gharama kubwa za kubadilisha rasilimali.
2. Kuendeleza tena au kuuza ardhi isiyotumika ili ku¬ongeza thamani na fedha kwa jamii.
3. Kuwa makini katika mauziano ya ardhi ili kuepuka miogoro inaayokwamisha maendeleo ya uendelevu wa ardhi husika.
4. Kutokujali uharibifu wa miundombinu ya maji na huduma za maji safi na maji taka kunakosababisha madhara ya kiafya na usumbufu kwa wanajamii
5. Manunuzi na mikataba ya wazi na ushindani yana¬ongeza imani kwa jamii. Kuanza ujenzi kwa fedha zisizotosha kunahatarisha ukamilishaji wake. Shule zinazojengwa na wananchi zinachukua muda bila kukamilika na kuchakaa na hivyo kupoteza matumaini ya umma.
CHANGAMOTO ZA USIMAMIZI WA RASILIMALI
A. Taarifa chache za rasilimali, kwa mfano, usajili usiokamilika na usio sahihi unazuia ufanisi na umadhubuti wa usimamizi.
B. Uelewa mdogo kuhusu rasilimali unaweza kusababisha kutokutumiwa, au kutumiwa kimakosa na matokeo yake kupunguza muda wake wa kuishi au kuziongezea gharama.
C. Kutokuwa na wajibu, majukumu na uwajibi¬kaji bayana wa usimamizi wa rasilimali kati ya ngazi za serikali au kati ya taasisi, maofisa na wafanyakazi kunaweza kuzuia ufanisi na kusa¬babisha kuongezeka kwa gharama au kasoro.
D. Kukosekana kwa michakato ya wazi ya kuanzi¬sha na kueleza sera na mwongozo wa usimamizi wa rasilimali kutoka katika ngazi ya taifa hadi ngazi ya jamii kunaweza kusababisha utumiaji na usimamizi mbaya wa rasilimali zilizopo na upataji holela wa rasilimali mpya. Jambo hili linaweza kusababishwa na kukosa uelewa wa mapengo na changamoto za mazingira wezeshi kwa ujumla.
A. Uhaba wa fedha mara nyingi unaweza kusa¬babisha mipango ya uwekezaji isiyokamilifu, kusababisha upatikanaji hafifu wa rasilimali na uendeshaji na utunzaji mbovu wa rasilimali.
B. Ukosefu wa vifaa na vitendea kazi muhimu kama vile miundombinu ya kuhifadhia inaweza pia kukwamisha usimamizi wa rasilimali.
C. Kutokuwa na uhakika kuhusu athari za mabadi¬liko ya tabianchi, dharura katika afya ya umma

Yamkini, Upangaji wa usimamizi wa rasilimali ni mchakato wa uamuzi mzuri kwa kadiri iwezekanavyo kuhusiana na ujengaji, uendeshaji, utunzaji, utengenezaji upya, ubadilishaji na utupaji wa rasilimali za miundombinu. Lengo ni kuongeza manufaa, udhibiti wa vihatarishi na kutoa huduma za kiwango kinachoridhisha kwa umma katika hali endelevu
 
Back
Top Bottom