Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,598
Kufuatia hukumu ya Jaji Masati ambaye amewaachia watuhumiwa wote kwamba hawana hatia ya mauaji, na kwamba hakuna mtu ambaye ameithibitishia mahakama bila kuacha chembe ya shaka kwamba watuhumiwa waliua; na kwamba ushahidi wa Lema (ungamo) ni batili kwa kuwa hakupata nafasi ya kuutetea mbele ya mahakama. Na kutokana na maoni ya utetezi kuwa Lema alikufa na ushahidi wake ambao ndio ungethibitisha wapi mauaji yalifanyika, nani aliyafanya na kwa amri ya nani. Kwa mazingira ya kesi hii, kifo cha Lema kilikuwa cha kawaida au ni mpango maalumu wa kuinyima ushahidi mahakama? Na je haiwezekani kuanzisha ujunguzi maalumu kuhusu kifo hicho sambamba na kumtafuta muuaji? Nimepata maswali mengi sana ila nahofia sasa kwamba kwa mwenendo wa kesi nyingi katika mahakama zetu itakuwa ngumu kupata watu wakaojitolea kuwa mashahidi.